Uchaguzi 2020 Tundu Lissu anajikoroga

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu anajikoroga

Huwezi kumuelewa Lissu na kamwe hutamwelewa kwa sababu akili zako zimekaa kimataga na ki Lumumba!

Lissu anasema wafanyabiashara wetu wadogo lazima wafanye biashara sehemu nzuri , zilizopangwa vizuri Sawasawa na thamani ya utu wao, sio kupanga biashara chini na sehemu chafu au barabarani kama nyie CCM mnavyowafanyia.

Lissu anavyosema hivi hamaanishi tu maendeleo ya vitu anamaanisha maendeleo ya mtu, Hii ni kwa sababu mtu akifanya biashara sehemu decent hata thamani ya utu wake inakuwepo.

Mataga nawaambieni hakika kamwe hamtomweza Lissu kwa upotoshaji wenu!!
 
Mlimlazimisha mama Nyerere kuongea kwenye mkutano?
 
WhatsApp Image 2020-09-06 at 14.51.56 (2).jpeg
 
Lisu ni mpango wa Mungu .
Hakuna Mgombea Urais yeyote Tangu Uhuru labda wapigania Uhuru wa Kweli akina Mkwawa na Mirambo ndio wanaoweza kulinganishwa na Lisu.
Wengine wote walipata Urais kama kuokota Dodo kwenye Mchongoma.
Wengine waliandaliwa na wakoloni kuja kuwawakilisha na dini zao.
Wengine wakapewa tu kama zawadi kwa sababu ya upole tu .
Wengine wakapewa ili tu vijana wasipate.
Wengine wakapewa kwa sababi ya kuiokoa chama hivyo ikabidi atoke mtu kwenye Ukanda na kabila Kubwa na watu wengi . Hapakua na mipango zaidi ya kupata Nafasi kama uteuzi tu kupitia Chama chenye dola.
Kugombea kupitia chama dola ni rahisi sana. Muulizeni Membe aliyeingia Tatu bora kwenye Chama dola leo upinzani anakosa hata viwanja vya kufanyia kampeni.

Ndio maana hao wazalendo wote waliunga mkono ufisadi uliofanywa kwa miaka mingi. Hwakuthubutu kujiuzulu zaidi ya kupiga makofi na kushangilia nchi ikiwa inatafunwa .

Hivi nani asiyejua kuwa Maisha ya wafanyakazi wa umma ni magumu mno kutokana na mishahara midogo . Lakini wale wale wanaotisha kuwafukuza kazi na kiwachapa viboko wakidai nyongeza ya mishahara wao wanalipwa Mara 40 ya kima cha chini cha Mshahara. Nani mzalendo hapo kati ya Mfanyakazi anayelipwa 1/40 ya Mwanasiasa anayetawala au mfanyakazi anayelipwa mshahara kwa ajili ya kununua chakula tu bila akiba huku wote wakiwa wanatumia Soko moja.
Zaidi Watawala wakiwa wanapewa usafiri,nyumba. Ulinzi,dereva na kila aina ya heshima.

Ningeamini kuwa wao ni wazalendo kama wangepunguza mishahara yao ili wote walie kilio kimoja kwa ajili ya kujenga Reli.
Wao mishahara yao na maslahi yao yapo juu na wameshika madaraka makubwa kwa miaka zaidi ya 20 lakini bado wanatafuta kura kwa vitisho na dhulma na rushwa za madaraka na fedha.

Lisu amewekwa na Mungu kama Jiwe la kujikwa kwa watawala na wapenda Dhulma na uonevu na ukabila.

Mungu alipomuumba Binadamu alimpa sheria na amri za haki ili alinde uhai na sio Majengo wala mandege ya kutembelea.

Haya mavitu ndiyo yanayovuruga amani ya dunia nzima na ndiyo yatakayoharakisha kuangamizwa kwa dunia.
Dunia bila haki ,utu na Uhuru binadamu anakua ni kiumba mbaya na wa kuogopa kulika Mnyama wa porini.
Leo hii Mwanachama wa Chadema akikutana na MTU kama Polepole au Kheri ni bora akutane na Chatu mana anaweza akaokoka.

Hii ndiyo Tanzania ya miaka mitano ya awamu ya tano. Wanaojopendekeza wanajipendekeza kwa kuwa wakatili na kuhubiri ubaya tu.
Watu wameanza kuwatisha na kusema wazo kuwa wataendelea kupeleka maendeleo kwenye maeneo ya nyumbani kwao wamapopata kura nyingi mana ndio msingi wa ubaguzi.

Hivi unaweza kweli ukawanyima maendeleo watoto,akina mama ,wazee na vijana wengi kama wale wa Arusha ,Mwanza, Mbeya ,DSM n.k walioonyesha mapenzi yao kwa upinzanani huku ukiwa unachukua kodi zao?
Hivi Ulaya unaweza ukawadharaua wapiga kura kiasi hicho.
Kwa nini asikose kura na yeye akapumzika ili ajifunze kuwa na utu na huruma na kodi za watu bila kujali vyama??

Bila shaka CCM inalindwa na ukabila na udini ndio maana inakua na kiburi namna hiyo. Ukabila na udini ndio unaowafanya watu kuwa kama vipofu vinginevyo mwaka huu CCM isingepata hata 10 ya kura kwa Maneno yao ya wazi ya kubagua watu.

Yani MTU akakwapue kodi za watanzania wote halafu apeleke kwenye maeno anayoyapenda yeye kwa sababu ya vyama.
Sio jambo la kupendeza kabisa duniani na mbinguni.
 
Kaa kimya kama huna la maana la kuandika badala ya KUBWABWAJA ujinga.
 
Lazima ku balance issues, huwezi kununua ndege watoto wakakosa mikopo wasisome! Masoko ya usiku ni kawaida,, ndio utaratibu wa ulaya!
 
hata kichaa hawez kumuelewa tundu lisu yan mkuu unakaa kabisa kusema unaitaj mda kumuelewa lissu africa tunataka kujitegemea yeye anakuja na sera za kushirikiana na ulaya a man who need to win the election unakuja na sera hiyo ya kipumbavu hivo sisi sio wapumbavu kiasi cha kutueleza ujinga huu
Wewe na Nani?

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
hata kichaa hawez kumuelewa tundu lisu yan mkuu unakaa kabisa kusema unaitaj mda kumuelewa lissu africa tunataka kujitegemea yeye anakuja na sera za kushirikiana na ulaya a man who need to win the election unakuja na sera hiyo ya kipumbavu hivo sisi sio wapumbavu kiasi cha kutueleza ujinga huu
Mpumbavu ni wewe!! Nani kakuambia Magufuli anajitegemea? Hivi unajuwa kuwa afya, elimu na miundombinu kuna fedha za wafadhili by 60%
 
yuko sahihi kabisa tukishuka stendi saa nane usiku toka shift tutakula na kuchukua mahitaji ya kwenda nayo nyumbani. machinga wataingiza hela mchana na usiku kwenye hizo malls watasaidia ndugu zao vijijini.

hayo ndio maendeleo ya watu, serikali itatoa tenda kwa kampuni binafsi za kitanzania na kuwalipa cash, pesa itazunguka mtaani.

SASA HAO WAMACHINGA KWENYE HIZO MALL WATAKUWA WANAFANYA BIASHARA BURE BILA KULIPIA CHOCHOTE? LISSU ANAONGOPEA WATU WAJINGA. WELEVU WATAMSIKILIZA NA KURA HAWATAMPA. SABABU WANAJUA NI UONGO WA MCHANA KWEUPE.
 
Kipi sasa kinawashinda msijitegemee?.Au unadhani kujitegemea ni sawa nakuota ndoto.Huna uchumi wowote imara,wataalamu,elimu duni,afya leo unajifanya ujitegemee.Hata hao unaowaona wameendelea hawakuendelea tu bila kushirikiana na wengine katika nyanja mbali mbali kuanzia nguvu kazi(ukoloni) hadi teknolojia sasa hivi ndo tunaona wanajitegemea.Sasa wewe unataka kujitegemeaje katika hali hii?
hata kichaa hawez kumuelewa tundu lisu yan mkuu unakaa kabisa kusema unaitaj mda kumuelewa lissu africa tunataka kujitegemea yeye anakuja na sera za kushirikiana na ulaya a man who need to win the election unakuja na sera hiyo ya kipumbavu hivo sisi sio wapumbavu kiasi cha kutueleza ujinga huu
 
CHADEMA kupitia Mgombea Urais wao ametamka kujenga masoko yatakayofanya kazi nyakati za usiku.

Namnukuu Lissu “Tutajenga majengo makubwa kwa ajili ya Wamachinga ili wafanye biashara kwa uhuru na sio kuwapa vitambulisho halafu wafanyie biashara kwenye mitaro ambako mvua inakuwa yao na jua linakuwa lao” -Tundu Lissu akiwa Mbeya

“Kwenye stendi za Mabasi tutajenga majengo ambayo Mama Lishe watauza vyakula, tunataka kuwa na masoko ambayo yatakuwa yanafanya kazi usiku kucha ili Mtu yeyote ambaye atakuwa amechelewa kufika kwenye mji husika apate huduma”-Lissu

Hoja kuu hapa ni kujenga masoko, watu kufanya biashara nyakati za usiku na vitambulisho vya wajasiliamali.

Lissu huyu anayesema kila siku maendeleo ni Watu na sio vitu, leo hii huyo huyo Lissu anasema atajenga masoko. Iko wapi hoja yake aliyosema maendeleo ya Watu na sio vitu? Ama soko ni Watu na sio kitu tena?

Huyo huyo Lissu na wenzake wanaosema wakiingia ikulu watauza ndege zote za nchi zilizonunuliwa na Rais Magufuli ndio hao hao wanatumia usafiri wa ndege kuzunguka mikoani. Au wanazopanda sio ndege ni mitumbwi?

Lissu huyu huyu anayepinga ujenzi wa umeme wa Mto Rufiji utakaozalisha megawatts 2115 kuwa unalifilisi Taifa, leo hii anasema atahakikisha Wajasiliamali wanafanya biashara hadi usiku. Anapinga ujenzi wa umeme wa uhakika anataka hao Wajasiliamali wafanye biashara gizani?

Alivyokuwa mkurupukaji Lissu anazungumzia vitambulisho vya Wajasiliamali kuwa havina tija kwa Wamachinga na Wajasiliamali. Lahaula!

Inawezekana "dish" limeyumba hajui kuwa hajui vitambulisho hivyo ni mkombozi kwa Wamachinga na Wajasiliamali wote wadogo. Mmachinga, Mama Lishe hapo awali walikuwa kwenye misukosuko mikubwa na Mgambo kutokana na suala la ulipaji ushuru waliokuwa wakitozwa kila siku ambapo walikuwa wakilipia ushuru wa Tsh. 500/- ama Tsh. 1,000/- kwa siku.

Leo hii badala ya kulipa Tsh. 180,000/- ama Tsh. 365,000/- kwa mwaka leo hii wanalipa Tsh. Elfu ishirini tu (20,000/-). Wanaokoa Tsh. 160,000/- na wengine wanaokoa Tsh. 345,000/- pamoja na bidhaa zao. Lissu atasemaje vitambulisho havina tija?

Inawezekana Lissu anapajua zaidi Ubelgiji kuliko Tanzania, nimkumbushe Tanzania kuna masoko kwa ajili ya Wamachinga yapo mfano hai ni soko la Machinga Complex lililopo Karume wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam.

Si hayo tu bali pia Rais Magufuli amejenga stendi mpya nyingi tu ikiwemo ya Mpanda Katavi, Morogoro, Dodoma nk na kote huko kuna majengo ya Wajasiliamali wote wakiwemo Mama Lishe.

Lissu aache kujikoroga, aelewe hizi sio zama za drama, siasa za uongo kwani Watanzania wa sasa ni waelewa sana wanajua mbivu na mbichi, hawalishwi matango pori!!

*Shilatu E.J*
Lisu kawashika vibaya marahii

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
sawa me mpumbavu ninaetaka kujitegemea binafsi bila kutumia pesa za wafahdili kama magufuli anavosema kila siku
Magufuli anakudanganya kila uchao. Salimia 80 Bajeti ya afya inatoka kwa Wafadhili. Endelea kumuamini mwongo mkubwa
 
Kama uelewi jambo si ujipe kwanza muda wakujielimisha kabla hujaja kuanzisha mada uku Jf.Sasa kama huwezi kuelewa hoja nyepesi kama hizo utaelewa nini tena sasa.
 
Magufuli anakudanganya kila uchao. Salimia 80 Bajeti ya afya inatoka kwa Wafadhili. Endelea kumuamini mwongo mkubwa
kudangwa wachwa nidanganywe lakini sio kumpinga na kumkataa kabisa utaratibu huu tunaishi nao kwa sasa naona ni bora kuliko na hata mpinzani huyu lissu hawez fanya hata robo haya aliyo yafanya maguli,
Magufuli anakudanganya kila uchao. Salimia 80 Bajeti ya afya inatoka kwa Wafadhili. Endelea kumuamini mwongo mkubwa
kudangwa wachwa anidanganywe lakini siwez kumpinga na kumkataa kabisa utaratibu huu tunaishi nao kwa sasa naona ni bora kuliko na hata mpinzani huyu lissu hawez fanya hata robo haya aliyo yafanya maguli,
 
Lissu anasema maendeleo ya vitu na watu viende pamoja. Awamu zote tulishuhudia miundombinu ikijengwa, mishahara ikipanda, ajira zikitoka, fao la kujitoa mifuko ya jamii liilikuwepo, biashara zinafanyika. Lakini kwa JPM kila kitu kime switch off isipokuwa miundombinu
 
Kama anasema kila siku mbona atekelezi.Si kaongoza miaka 5.Uko kujitegemea kuko wapi?.Chuki zenu binafsi kwa waliofanikiwa hakuwezi kuwasaidia mkajikwamua kutoka hapo mlipokwama.
sawa me mpumbavu ninaetaka kujitegemea binafsi bila kutumia pesa za wafahdili kama magufuli anavosema kila siku
 
Kama anasema kila siku mbona atekelezi.Si kaongoza miaka 5.Uko kujitegemea kuko wapi?.Chuki zenu binafsi kwa waliofanikiwa hakuwezi kuwasaidia mkajikwamua kutoka hapo mlipokwama.
ww mpka sasa umeshakamilsha mangapi amabayo umeyapanga /me naona unabishana na upepo mkuu kama ww leo huona magufli kafanya nn bas hutoweza kuona la mwingine yoyote yule atakae kuja kuongoza nchi hii
 
Back
Top Bottom