Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Kama kuna kitu CHADEMA wanapaswa kujifunza kutoka CCM basi ni suala zima la kusimamia maadili, nidhamu,sheria,kanuni, taratibu,miongozo na katiba ya chama.Ndani ya CCM hakuna aliye mkubwa zaidi ya chama,hakuna aliye juu ya chama,hakuna mwenye kusema pasipo yeye hakuna CCM au kwamba yeye ndiye CCM na hawezi kufukuzwa wala kuambiwa chochote kile.
Ndani ya CCM mtu au kiongozi yeyote yule anaweza kuitwa kuhojiwa au kupewa onyo au karipio au kusimamishwa uanachama au kufukuzwa kabisa. Ndani ya CCM Bila kujali ukubwa wa jina la mtu au umri wake au wadhifa wake au umaarufu wake au uungwaji mkono wa mtu unaweza kukatwa jina na kuenguliwa katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi fulani ikiwa itabainika umekiuka sheria, kanuni, taratibu, miongozo na katiba ya chama.
Huwezi ukafumbiwa macho ndani ya CCM ikiwa mwenendo wako utaonekana kuhatarisha umoja na mshikamano wa chama au ikiwa mwenendo wako unakigawa chama na wanachama.Mifano ipo mingi lakini sitaitaja kwa leo ili andiko lisiwe refu sana.
Sasa tangia kupulizwa kwa filimbi ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CHADEMA. na Lissu kuchukua Fomu ya kuwania uenyekiti wa chama Taifa.Imeleta aibu kubwa sana na fedheha kubwa sana kwa chama na yeye mwenyewe.ambapo watu mbalimbali wenye akili Timamu wamebaki wanajiuliza ilikuwaje Lissu akafikia hatua ya kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa?
Kila mtu ameshuhudia lissu akiongea mambo ya chama bila breki,akiongea na kutoa siri za chama hadharani bila kikomo wala breki utafikiri amekatika mishipa ya fahamu.kauli zinazotoka mdomoni pake zimekivua nguo chama na kuharibu sifa ya chama kwa kuonekana ni kama genge la wasaka Tonge na wachumia tumbo tu wasio na muelekeo wala Dira zaidi ya maslahi binafsi.
Lissu kwa mdomo wake ambao haujawahi kuwa na subira wala uvumilivu wala hekima wala busara wala staha amefanya kazi ya kuwachafua viongozi wenzake,kuwazushia uongo na ufitini pasipo ushahidi wa aina yoyote ile alioutoa hadharani.Ametoa kila aina ya siri za chama zinazopaswa kuzungumzwa kwenye vikao nyeti vya chama.
Amekuwa akiserereka tu Mdomoni pake utafikiri gari lililokatika breki mteremkoni.haelewi wala kujua kipi cha kuongea hadharani na kipi cha kuongelewa faragha.hajui kipi azungumze na kipi asizungumze.yaani yeye Maiki ikiwa mbele yake ni kama anachanganyikiwa na kupoteza balansi ya mdomo.
Hivyo kujenga nidhamu ya chama anapaswa kukatwa na kuenguliwa haraka sana pamoja na kutoa onyo kali sana kwake .na ikiwa ataendelea basi afukuzwe chamani na kwenda anakotaka.ni lazima CHADEMA ichukue hatua hizo mapema sana ili kukinusuru chama na kujenga umoja na mshikamano ndani ya chama.
Haiwezekani CHADEMA iliyojengwa kwa jasho na Damu ibomolewe kwa mwezi mmoja na Mdomo wa Lissu usio na breki wala kipimo . haiwezekani CHADEMA ambayo kuna watu wameipambania kwa jasho na Damu na wameifia, leo hii lissu aje aanze kuipeleka shimoni halafu abakie anaangaliwa bila kuchukuliwa hatua zozote zile.hiyo haiwezekani na haikubaliki na haipaswi kukubalika wala kufumbiwa macho wala kuvumiliwa.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.