Tundu Lissu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, BAWACHA wakiadhimisha siku ya wanawake Machi 08

Tundu Lissu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, BAWACHA wakiadhimisha siku ya wanawake Machi 08

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema BAWACHA, Sharifa Suleiman, amesema kuwa tarehe 8 Machi baraza hilo linatarajia kudhimisha siku ya wanawake Dar es Salaam.

Hayo ameyasema leo tarehe 23 Februari 2024, wakati anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.ambapo amesema kuwa katika maadhimisho hayo yatakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA

Sharifa amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni 'harakisha usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu'.
 
Wakuu,

Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Tundu Lissu, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayoandaliwa na Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) tarehe 8 Machi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Februari 23, 2024, Mwenyekiti wa BAWACHA, Sharifa Suleiman, alisema maadhimisho hayo yatafanyika katika ukumbi wa Mlimani City, yakibeba kaulimbiu "Harakisha Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu."

Napingana na hiyo kaulimbiu yao, hakuna kitu kinaitwa usawa wa kijinsia. Huu ni utapeli.
 
Ina
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema BAWACHA, Sharifa Suleiman, amesema kuwa tarehe 8 Machi baraza hilo linatarajia kudhimisha siku ya wanawake Dar es Salaam.

Hayo ameyasema leo tarehe 23 Februari 2024, wakati anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.ambapo amesema kuwa katika maadhimisho hayo yatakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA

Sharifa amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni 'harakisha usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu'.
View attachment 3246348
Hii nayo ni habari? Inatuhusu nini?
 
😂😂😂 Vitu Tundu anaweza kufanya na anapenda....
 
Chadema msipojiongeza na kutafakari,uke uchaguzi wa ndani ,una kidonda ndani yake. Rekebisheni na mbuni mbinu mpya za kuendesha chama na kuisoma mifumo na muundo wa CCM, ili muweze kupambana nao.
Msipokataa Rais, kuwateua na kuwaapisha, madc,MaRc na wakurugenzi wa halmashauri ,kuchukua Dola ni ndoto.
 
4R ilikuwa ni mbinu ya Samia kuwapumbaza wafadhii na wapinzani. Kiasi kikubwa kafanikiwa
Tulimuamini kuwa ataachana na wahafidhina wa Chama chake na tukajua kuwa yeye atafuata progressive politics sasa haaminiki tena.
 
Back
Top Bottom