Mimi ni mwana CCM, Tundu Lissu anachotufanyia sio sahihi kabisa, Sasa anatuchezesha segere ya kujibu hoja zake ambazo kwenye TV hazionyeshwi na hazijibiki.
Yale maelfu ya watu wanaomfuata wanatoka wapi?
Taarifa zake zinaenea kwa style ipi mpaka viongozi wa ccm wanazipata na kuzijibu?
William Lukuvi aliwahi kutamka kuwa Tundu lissu anatumia Ngekewa au kamzizi wakati wa Bunge la Katiba kushawishi wajumbe wamsikilize na wengi kukubaliana na hoja zake, Kauli ya lukuvi ilitokana na Tundu lissu kuwazidi kwa hoja za mambo ya muungano na uwezo wa kushawishi wajumbe
Je, kwa haya yanayoendelea kwenye kampeni kwa umati unaomfuata na kusababisha kila mtu kumfuatilia ni Ngekewa au kamzizi?
Siamini katika ndumba lakini hizi video zinajieleza
Kama watu wameamua tu kumfuata bila ndumba au kamzizi basi ccm chama changu kinapaswa kubadili mbinu
Facebook huko imewekwa hoja ya Majimbo watu wanaisifia na kuponda chama cha mapinduzi vibaya sana na hii ndio imepelekea mimi kuandika hii mada hapa JF
Nashauri chama changu mbinu ya kumaliza hizi hoja ni kutekeleza mambo yafuatayo kuelekea oktoba 2020
Mosi, Kushusha kodi ya pay as you earn kwa asilimia mbili
Pili, Kurudisha riba ya mikopo ya wanafunzi mpaka kumi asilimia au nane
Tatu, Kuwaomba radhi wale ambao bado wana hasira na chama hasa baadhi ya wafanyabiashara na wakulima
Nne, Kundi kubwa la CCM linaonyesha litapiga kura za hasira hivyo linahitaji kuwa nalo makini,Hawa wanashangilia lakini ni dhahiri watakiadhibu chama kwenye sanduku la kura,Tuwe nao watu hawa makini kwenye kampeni
Ninaona leo mmejaribu kujibu hoja ya kugawa majimbo na hoja ya vitambulisho. Lakini kule kwa mtoto wa dada kuwa Paymaster General, na Mayanga Constructions hamkugusa kabisa.
Kule namtumbo na Dodoma na singida tuna uranium eti yote Ni ya mafisadi ya maccm yaliyoko Dar, Kama ilivyo gas ya mtwara na Lindi, au dhahabu ya shinyanga
Ninaona leo mmejaribu kujibu hoja ya kugawa majimbo na hoja ya vitambulisho. Lakini kule kwa mtoto wa dada kuwa Paymaster General, na Mayanga Constructions hamkugusa kabisa.
Mimi ni mwana ccm,Tundu lissu anachotufanyia sio sahihi kabisa,Sasa anatuchezesha segere ya kujibu hoja zake ambazo kwenye TV hazionyeshwi na hazijibiki
Yale maelfu ya watu wanaomfuata wanatoka wapi?....
Kafara La damu mbichi ya mwanadamu hai iliyogusa ardhi isiyosakafiwa ni kafara lenye nguvu mno
Kafara nyingi huwa na damu mbichi lakini kiumbe hufa kwa mateso mara nyingi ya kuachiwa kirukeruke mpaka roho itoke..hizi kafara za namna hii huwa zina nguvu lakini hazina double impact kama lile la Lissu
Kafara hili nguvu na mvuto wake ni zaidi ya ndele na yale mafuta ya simba kwakuwa
Damu mbichi ya moto imebusu udongo
Damu haikuwa mfu
Roho haikutengana na nafsi hai
Mwili ulijeruhiwa lakini haujaharibika
Ni nguvu mara tatu DAMU NAFSI NA ARDHI
Hii inapelekea hata wale wanaojaribu kujibu hoja zake wanaishia kukosa nguvu ...wanaishia kukosa mvuto kishapo wanaweweseka...mfano halisi ni mgombea pinzani na vijana wa lumumba mitandaoni.
Kitu kingine ni kwamba kafara hili nguvu yake ilianza kazi kipindi kilekile ndio maana likafubaza hata lile kafara maarufu la kukimbiza moto nchi nzima maarufu kama mwenge wa uhuru.
Kwahiyo nguvu na mvuto alivyonavyo TAL ni vya kiroho zaidi kuliko kimwili na ndio maana ganzi zilianzia pale airport alipotua mpaka kupitishwa na tume ya uchaguzi.
Na huu mwendo ni mpaka ikulu...hakuna majeshi wala polisi watainua silaha juu yake..ganzi itakapowaisha jamaa yuko ndani ya jumba jeupe.
Kwangu naona lissu amemhurumia sana jpm, jpm kafanya mengi ya hovyo kama uvunjaji wa katiba, kuonea watu, kutoa mikopo kiubaguzi.
Kutumia polis kunyanyasa wapinzani, kujipendelea.kushindwa kusimamia usalama wa ria na Mali zao na kusababisha kutekwa watu na kupigwa risasi mchana kweupe
Hii ni kweli kabisa. Wiki hizi mbili zijazo ni muhimu sana, tuangalie ishara fulani kutoka pande fulani. Tukiziona tu, habari imekwisha. Mimi nitakuwa macho kuziangalia.