Anaandika Dotto Bulendo.
Ukimsikiliza Vizuri Tundu Lissu kwenye mahojiano yote alivyofanya na vyombo vya Habari vya ndani na nje tangu apigwe Risasi,kilio chake ni .....
1.Kwa nini waliompiga Risasi mpaka sasa hawajakamatwa?analalamika hata watuhumiwa tu hawajakamatwa na kuhojiwa.
2.Lissu analalamika ipo wapi CCTV Camera ili isaidie kuwabaini kwa sura wale waliompiga kwa sababu anasema alipingwa Risasi akiwa ameshaingia ndani ya fensi ya nyumba za viongozi wa Serikali ambamo na yeye anaishi.
3.Lissu analalamika Serikali haijawahi mpatia pesa za matibabu zaidi ya michango kutoka kwa watu mbalimbali.
Haya ndiyo mambo makubwa anayoyalalamikia Lissu tangu nianze kumsikia kwenye vyombo vya ndani na nje vya habari.
Kinachoniweka njia panda,kwa nini Lissu akiyalalamikia haya baadhi ya watu wanamkebehi na kusema anaichafua nchi?
1.Hivi ni kweli Lissu akihoji kwa nini mpaka sasa hakuna aliyehojiwa kutokana na tukio la yeye kupigwa Risasi huko ni kuichafua nchi na kukosa uzalendo?
2.Hivi ni kweli Lissu kuuliza zilipo CCTV Camera ili zisaidie upelelezi na hata kumkamata/kuwakamata waliompiga Risasi napo ni kuichafua nchi ama kukosa uzalendo?
3.Hivi Lissu kuiulizia haki yake ya matibabu kutoka Serikalini napo ni kuichafua nchi?
Kwa mtu ambaye alibahatika kumuona Lissu akiwa kitandani Hospitalini Dodoma ama akiwa kitandani Nairobi-Kenya,ama kama uliona jinsi alivyofanyiwa oparesheni nchini Ubelgiji anaweza elewa kwa nini Lissu anaongea haya.
Haya mambo matatu ndiyo yamekuwa hoja kubwa ya Lissu,Familia yake na hata baadhi ya Watanzania wanahoji iko wapi CCTV ili iwezeshe kuwabaini waliompiga Lissu,Kwa nini mpaka leo waliompiga Lissu(watuhumiwa),hawajakamatwa na kuhojiwa,Je kwa hali aliyokuwa nayo Lissu baada ya kupigwa Risasi Dodoma kweli Lissu angeweza kuanza kusaka vibali vya Wizara ili akatibiwe Nje ya Tanzania?
Bado naiona ipo nafasi ya kulimaliza hili kwa sheria kufuatwa na nina amini anayoyalalamikia Lissu yapo ndani ya uwezo wetu kuyashughulikia.
Nachokiona sasa tatizo la msingi ambalo ni nani alimpiga Lissu,gharama za matibabu ya Lissu inataka kutokuwa ajenda na sasa tunataka kuanzisha mjadala mpya wa ....
1.Kwa nini Lissu aongelee nje?sasa sijui suala la kuongea lina mipaka?labda mimi sijui!
2.Kwa nini analalamika kupigwa Risasi,sasa sijui Lissu alitakiwa kukaa kimya hata kama anaona haoni matumaini ya juhudi za kuwakamata waliompiga Risasi,hajapata haki yake ya matibabu kama mbunge,sijui aliyakiwa akae tu kimya?
Lissu mara zote hajawahi mtaja aliyempiga Risasi bali kilio chake ni kuitaka Serikali iwakamate waliompiga Risasi akiamini CCTV Camera zinaweza saidia kuwabaini waliompiga,sasa hapa kosa la Lissu ni nini?
Kuna mambo yanatafakarisha sana.
MY TAKE;
Ni kweli yana tafakarisha sana Mwl Bulendo! Yaani hats viongozi wa juu ndani ya ccm wenye elimu wameshindwa kuliona na kulitambua hili?
Sent using
Jamii Forums mobile app