Upekuzi101
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 221
- 542
Kuacha ushabiki wa vyama, tunaweza kukubaliana japo kwa kiasi kuwa Tundu Lisu ni mwanasiasa mzuri ila mrengo wake ni wa kiharakati zaidi tofauti na vyama vingine na kuna kiasi kikubwa tu cha watanzania wanavutiwa na siasa za namna hii.
Katika mchakato wa uchaguzi wa mwenyekiti wa CHADEMA taifa, tumeona waziwazi ni kwa kiasi gani kuna wanachama wanamuunga mkono Tundu Lisu ndani ya chama na hata wale walipo mitaani wanatambua ni kwa kiasi gani msimano na harakati za Lisu zinavyoungwa mkono. Tundu Lisu tambua siasa ni art ila ndani yake Kuna sayansi, na Ili uweze ku survive jipange at least for 15 years to come.
Kuna hazina kubwa ya vijana na unaweza kuwekeza kwa vijana kuanzia sasa kwa kuanzisha chama kipya cha siasa kwa kuangalia mahitaji ya wakati, weka dira, na malengo yako wazi kwa vijana, hakikisha malengo ya chama chako yanagusa kwa uhalisia maisha halisi na mahitaji halisi ya Watanzania, tafuta idadi kubwa zaidi ya uungwaji mkono kwenye rika zote.
Chagua kwa usahihi safi safu itakayoweza kuelewa vizuri falsa yako Ili iwe rahisi kwenye uhamasishaji. Tengeneza ushawishi pia kwa wasomi ambao hata kama hawabeba bendera ya chama waziwazi, wabebe moyoni huku ukipambana kuhakikisha unakuwa na vijana walimu, madaktari, engeneers, pilot, polisi, wanajeshi, wakurugenzi na hata makatibu tawala, hili litakuwa jeshi lako ndani ya mfumo hivyo utaweza ku influence maamuzi mwisho wa siku unaweza hata kama si wewe basi mwakilishi wa chama chako kugombea nafasi ya urais miaka ya mbeleni na kushinda.
Siasa za Tanzania zinahitaji akili kubwa ukizingatia chama kama CCM kimejenga mizizi hadi ngazi ya shina kitu kinachohitaji pia muda na strategy kuking'oa kuanzia kwenye mizizi. Kwa kusema hayo, naomba chukua muda wako kutafakari hayo huenda ukakupa mwanga kufikiria zaidi kama uliwai kufikiria jambo hili.
Ndani ya Chadema huwezi ku thrive kwakua Kuna mgongano mkubwa wa maslahi ukizingatia Mbowe anafanya kazi na system, wewe una fight against the system.
Jenga chama cha kisasa kinacho address mahitaji halisi ya wakati na utapata watu wengi sana watakaosimama na wewe. 2015 uliona watanzania walivyosimama na CHADEMA, Ilo linawezekana na kwako pia hasa kwa chama chako kipya, not necessarily you.