"Dkt. Slaa ndiye aliyemleta Edward Lowassa CHADEMA, ndiye aliyeanzisha hilo wazo, ndiye aliyeongoza timu zote majadiliano za CHADEMA kujadiliana na timu ya Lowassa na ndiye aliyeitisha kikao cha Kamati Kuu cha kumkaribisha Lowassa na ndiye aliyenipigia mimi simu nikiwa jimboni kwangu Singida, Mashariki tarehe 26, 27 kama sikosei ya Julai 2015 na kuniambia njoo tuna Kamati Kuu ya dharula kesho
"Na usiku wakati nasafiri kuja Dar es Salaam akanipigia simu kunambia kwamba Chama kimeuzwa alafu nilipokutana nae kesho yake na Mwenyekiti na Askofu Gwajima…mshenga alikuwa Gwajima wa Edward Lowassa…."
17 January 2025 Odero Charles Odero aibuka kidedea katika mdahalo dhidi ya Tundu Antipas Lissu
View: https://m.youtube.com/watch?v=FfS5cmy-nSk
Mwanachama mwandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Odero Charles Odero leo alikabiliana vikali kwa hoja dhidi ya kiongozi wa juu wa CHADEMA makamu mwenyekiti (bara) Tundu Antipas Lissu.
Odero Charles Odero alihoji staili ya uongozi wa sasa wa CHADEMA ambao Tundu Lissu ni miongoni mwao...
Pia maswali kutoka nchi nzima yalimiminika studio katika kipindi mdahalo ulioongozwa na Chief Odema ambapo ni wagombea wawili tu kati ya wanne yaani Odero Charles Odero na Tundu Lissu ndio walijitokeza leo katika mdahalo ... mwenyekiti Freeman Mbowe na mwanachama Romanus Romanus Mapunda hawakuweza kujitojeza.
Romanus Romanus Mapunda mgombea nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA
Tarehe 19 Desemba 2024 Romanus Romanus Mapunda alifika Makao Makuu ya Chama yaliyopo Mikocheni Dar Es Salaam Tanzania kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa Chama ngazi ya Taifa CHADEMA kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa Chama Mhe. John John Mnyika
Odero Charles Odero endapo akifanikiwa kuwa Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), amesema atafanya mabadiliko ya mchakato wa uchaguzi wa nafasi hiyo na kwenda mikononi mwa wanachama kuanzia ngazi za mashina.Odero amezungumza hayo leo, alipofanya mahojiano maalum na #MorningTrumpet kuelekea Uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa