Tundu Lissu ataja wabunge wafanyabiashara wakubwa wanaoshusha bei ya pamba

Mimi Huwa si muumini wa kujifananisha ili nijipime ni hatua Gani nimepiga katika kusonga mbele. Kwasababu tuna fursa tofauti, mazingira na hata changamoto. Kama tunastahili zaidi huu ulinganifu ni kutaka kuhalalisha yasiyostahili. Ingawa katika hili tupo pamoja
 
Akisema Bodi ya Pamba ndio inapanga bei ya pamba, lakini;

- Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba ni Christopher Mwita Gachuma ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na ndiye mnunuzi mkubwa wa pamba nchini.

- Bariadi mnunuzi mkubwa wa pambakatika mkoa wa Simiyu ni Bwana Njau (Mbunge wa jimbo la Itilima kwa tiketi ya CCM) na ndugu yake Gungu (Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM).

- Mwandoya Jimbo la Kisesa utaambiwa kuna mtu anaitwa Gaki lakini ukiuliza kila mtu eneo hilo anayefahamu atakwambia hiyo Jineri inaendeshwa na ndugu wa Luhaga Mpina Mbunge wa Jimbo Kisesa CCM.

- Maswa Mashariki - Mbunge Nyongondiye mnunuzi mkubwa wa pamba eneo hilo.

- Wilaya ya Kishapu, Jineri inamilikiwa na Cherehani, Mbunge jimbo la Ushetu ambaye ndiye mnunuzi mkubwa wa pamba eneo hilo.

- Ushetu kwenyewe kuna mgogoro mkubwa kwenye zao la Pamba na Tumbaku, ambako wananchi wamesema mnunuzi mkubwa wa pamba katika jimbo la Ushetu ni kampuni ya Mkwawa ambayo nyuma yake viongozi wengi wa CCM akiwepo Hussein Bashe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…