Pre GE2025 Tundu Lissu ataka viongozi wa dini waingizwe kuwa wasimamizi wa uchaguzi wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Anatapatapa kutafuta huruma huku na kule. Kwani Katiba ya Chadema ambayo yeye ndiye alikuwa msimamizi Mkuu wa kuiandaa ina kipengele hicho?
 
yaani viongozi wa dini waache kazi na majukumu yao ya kuongoza taasisi zao za kidini, kuwahubiri neno la Mungu, kuwaombea waamini wao na kuliombea taifa kwa ujumla, waende kusimamia uchaguzi wa chadema?

huku ni kuchanganyikiwa na kuweweseka kwa kiwango cha juu mno.

ana lengo gani hasa na viongozi wa dini wa taifa hili, huyu kibaraka wa mabwenyenye ya magharibi?

anataka kuwaharubia au kuwachonganisha viongozi wa dini na serikali au anataka kuwaingiza viongozi wa dini kwenye siasa?

hii si sawa hata kidogo.
vingozi wa dini miaka yote hualikwa na chadema kama wageni waalikwa wa heshima lakini pia kama waombezi na mashuhuda wa amani katika vikao na mikutano ya vyama vya siasa ikiwa ni pamoja na chadema.

Ni muhimu sana,
viongozi wa dini wajiepushe na kujitenga na ushauri wa kibaraka wa mabwenyenye ya magharibi, kwani una nia ya kuwachonganisha na serikali sikivu ya CCM 🐒
 
Anataka na marafiki zake wabeligiji nao waingie kwenye mkutano. Huyu akiwa Rais Baraza la Mawaziri atakuwa analazimisha wazungu waingie hata 100 kama watazamaji
 
Namuunga mkono TUNDU LISSU kwa asilimia zote 100% kuna, mpinzani wa kweli vs nusu mkate. nusu mkate hana cha kupoteza iwe jua au mvua anautaka tena uenyekiti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…