Benson Mramba
JF-Expert Member
- Oct 29, 2013
- 648
- 1,485
Lissu na Mbowe mara kadhaa nimewasikia wanamshambulia Mbatia na NCCR hadharani. Pia jana nimemsikia Mbowe akiwaita wabunge waliohamia NCCR kutoka CHADEMA kuwa ni wasaliti.
Pia Lissu anawaita wanaCCM wote MaCCM sasa kauli hizi za kiubaguzi zinawaunganisha wanaobaguliwa kuliko kuwagawa. Nyerere alisema bila Muungano hakuna Watanganyika wala Wazanzibar.
Wazanzibar ni wamoja sasa hivi kwasababu kuna watanganyika ndani ya Muungano. Muungano ukivunjika hakuna watanganyika bali kuna makabila mbalimbali pia hakuna wazanzibari bali kuna waunguja na wapemba.
Sasa kama Lissu anataka Urais agenda yake namba moja ilipaswa kuwa kuwaunganisha watanzania na kutokuwabagua ili aweze kupata kura za wanaCCM, WanaNCCR n.k wenye msimamo wa wastani lakini kwa ubaguzi wake huu na chama chake ni ngumu kupata kura za wanachama wa vyama vingine. Ila kama wanatafuta kura nyingi kwa ajili ya ruzuku au kupata wabunge wengi kwa ajili ya kambi ya upinzani basi waendelee na ubaguzi huo. Lissu usirithi maadui wa Mbowe hawakuhusu.
Lowassa pamoja nguvu zake alisimamia agenda ya kuunganisha watu wa vyama vyote na makundi mbalimbali hapa nchini ndio maana kila mtu alijiona sehemu ya Lowassa.
Sasa ili kushinda Urais unapaswa kuunganisha makundi mbalimbali. Lissu anahitaji kura za Vunjo za watu wanaoiunga mkono NCCR Mageuzi na Mbatia. Halikadhalika Moshi vijijini, Rombo na maeneo mengine.
Lissu abadili kauli na mindset yake. Kitabu cha Dr. Slaa kinanukuu kauli ya Lissu wakati wa kumpokea Lowassa CHADEMA wakati ule 2015 kuwa " Hata kama watalazimika kushirikiana na shetani ili kuitoa CCM madarakani watafanya hivyo" Je NCCR, CHAUMMA, CCM, NGO,CSO ni mbaya kuliko shetani? Je Lissu hawahitaji hawa kwa ajili yake?
Sasa endeleeni kulewa na nyomi la watu elfu 10 uwanjani kwenye jimbo lenye wapiga kura laki 2 na ushee halafu mje kulia mmeibiwa.
Lema mwenyewe haamini kama Lissu atashinda Urais kadhalika kikundi chake ambacho ni Mbowe, Regy, Mrema n.k sasa Lissu acha usifungue macho wakati wenzio walimtaka Nyalandu