- Thread starter
- #21
Ndio maana tunasema, kama kweli Samia ana dhamira ya kufanya maridhiano aanzie huko nyuma, isangaliwe tu nani alidhuriwa na serikali awamu ya 5.
Tuangalie na watu kama kina Kasanga Tumbo kama kuna madhara walifanyiwa, serikali itoe fidia kwa familia zao.
Serikali inaweza kuanzisha dawati ofisi ya waziri mkuu litakalokuwa na jukumu la kupokea malalamiko kwa wananchi waliodhulumiwa na serikali kwa namna yoyote, kuyachambua malalamiko hayo na kuona namna gani mlalamikaji anaweza kupata unafuu/fidia.
Haiwezi kuwa kazi ngumu wala mzigo kwa serikali kwani malalamiko yatakayoshughulikiwa ni yale yatakayokuwa na ushahidi uliokamilika/unaojitosheleza.
..inawezekana Samia hana dhamira ya kweli kuhusu maridhiano na haki, au hana uelewa wa jambo hilo kwa mapana yake.
..kabla hujamfikisha kwa kina Kasanga Tumbo walioteswa huku Tanganyika, kuna wakina Abdulah Kassim Hanga, Mdungi Ussi, na wengine waliopotezwa Zanzibar.
..Sasa kama hayo ya Zanzibar ambako ni kwao hana habari nayo, haya ya Watanganyika yatamshughulisha kwa namna yoyote?
..Kwa mtizamo wa Samia, nini maana ya RECONCILIATION? Unaweza kufanya reconciliation huku unateua watu kama Ramadhan Kingai kuwa DCI?
..Ngoja tuone Samia atatufikisha wapi. Nahisi amepoteza nafasi nzuri ya kuliponya taifa na kufungua ukurasa mpya wa kijamii, kisiasa, na kiuchumi, hapa Tanzania.