Tundu Lissu atembelea kaburi la Balozi Christopher Kasanga Tumbo. Asema Taifa likijitambua Kasanga Tumbo atajengewa mnara kwa ushujaa wake


..inawezekana Samia hana dhamira ya kweli kuhusu maridhiano na haki, au hana uelewa wa jambo hilo kwa mapana yake.

..kabla hujamfikisha kwa kina Kasanga Tumbo walioteswa huku Tanganyika, kuna wakina Abdulah Kassim Hanga, Mdungi Ussi, na wengine waliopotezwa Zanzibar.

..Sasa kama hayo ya Zanzibar ambako ni kwao hana habari nayo, haya ya Watanganyika yatamshughulisha kwa namna yoyote?

..Kwa mtizamo wa Samia, nini maana ya RECONCILIATION? Unaweza kufanya reconciliation huku unateua watu kama Ramadhan Kingai kuwa DCI?

..Ngoja tuone Samia atatufikisha wapi. Nahisi amepoteza nafasi nzuri ya kuliponya taifa na kufungua ukurasa mpya wa kijamii, kisiasa, na kiuchumi, hapa Tanzania.
 
..Lissu amefanya jambo kubwa sana kuitembelea familia ya Balozi Kasanga Tumbo.

..sijui ni wangapi wanajua Balozi Christopher Kasanga Tumbo ni nani.

..Na kwanini Tundu Lissu ameamua kutembelea mahali alipozikwa Kasanga Tumbo.



Lissu yupo deep sana , huyu ndo ajae , naandika nikwa na akili timamu na Mungu wangu ,huyu ndie ccm naomba mnielewe kama twataka songa mbele kama taifa huyu ndie, lakini akiwa watu wenye akili toka ccm lazima chukuliwa ili kujenga nchi , huyu ndie asema Bwana, ukibisha wafaa, Mungu sio mwanadam
 
Matatizo yanayowakabili wananchi wewe na mm siyo lazimwa yasemwe na chadema ndugu. Wewe mwenyewe popote ulipo paza sauti utasikika! Kwann wale wafanya biashara pale kariakoo hawajasubiri chadema? Mbona walisikilizwa.
Mwenye soln ya matatizo ya wananchi ni wananchi wenyewe na serikali walio ichagua ili iwaongoze.sijui umenielewa?
 
..inawezekana Samia hana dhamira ya kweli kuhusu maridhiano na haki, au hana uelewa wa jambo hilo kwa mapana yake.
Dhamira haipo. Wanachofanya ni ulaghai ili wapate unafuu kwenye uchaguzi ujao.

Tumshukuru Mungu kwamba Lisu kaligundua hili na kulishikia bango.
 
Kuleni chuma
 
Umesikia alivyosema? NIMEKUJA KUOMBA MSAHAMA KWA MAOVU WALIOMTENDEA VIONGOZI BALOZI KT KWA NIABA YETU.

Hii inaassume mambo kadhaa:

1. KT alitendewa mabaya
2. Alitendea na viongozi..
3....kwa niaba yetu
4. Wamenituma niombe msahama kwa maovu....
5. ..kwa niaba yao....
 
Silioni la "kushindwa kukuelewa" wewe katika hayo uliyoandika hapo, ila ulichoshindwa kuelewa wewe katika bandiko langu ndilo tatizo lako.

Mfano wa Kariakoo ulioutolea mfano nalo inaonyesha upungufu, kwa sababu hao watu wa Kariakoo walijipanga, wakawa na viongozi wa kusimamia walichoamua kabla ya kuwasilisha serikalini.

CHADEMA ni chama cha siasa kinachofanya kazi yake ndani ya wananchi..., au hili nalo hulijui?

Acha nisikuchanganye, maana unaonyesha dalili za kuchanganyikiwa haraka sana na mambo mepesi yasiyochanganya kwa mtu wa kawaida.
 
Hayo yote aje ayaibue mika mingi ishapita ilikuwa na lengo gani zaidi ya kutafuta kiki magazetini na kwenue vyombo vya habari?

Nimemuona ana Jogi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…