Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,187
Tundu Lissu akipelekwa Nairobi
Mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lissu amedai kuwa mvutano kuhusu Bunge kukataa kulipia gharama za matibabu yake kwa kukiuka taratibu za matibabu ya Wabunge na kupelekwa Nairobi badala ya Muhimbili ni mgogoro wa kutengenezwa na kwamba, utaratibu huo hautambuliki kisheria. Lissu amedai kuwa, uamuzi wa kumpeleka Nairobi badala ya Muhimbili haukufanywa na Uongozi wa juu wa CHADEMA peke yao bali ulihusisha Viongozi wengine wa Bunge na Serikali.
Hata hivyo, katika mahojiano na Mwananchi jana, Lissu amedai kuwa, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ndiye aliyelazimisha yeye kupelekwa Nairobi badala ya Muhimbili. "Msimamo wa Mwenyekiti Mbowe kwamba lazima nipelekwe Nairobi ama Afrika Kusini, ndio uliookoa maisha yangu."
Kwa hali hiyo, Lissu anakiri wazi kuwa, uamuzi wa yeye kupelekwa Nairobi haukufuata taratibu na baraka za Serikali bali Viongozi wa Bunge na Serikali waliridhia msimamo wa M/kiti wake Mbowe aliyetaka apelekwe Nairobi ama Afrika Kusini. Hata katika maelezo ya Spika Job Ndugai, Ndege ya kumpeleka Lissu Muhimbili tayari ilikuwa imeshaandaliwa lakini ilikataliwa na CHADEMA na wao kuamua kukodi ndege nyingine kwa gharama zao.
Hakuna anayefurahia majanga kwa mwenzake lakini siyo vizuri pia kutumia majanga kutafuta umaarufu tena kwa njia ya kuwadhalilidha Viongozi wengine waonekane kuwa, hawakuwa na nia njema. Nadhani kama kuna mtu muhimu ambaye hajapongezwa inavyotakiwa ni Spika wa Bunge kwani yeye ndiye aliye-organise Kikao cha Kamati ya Uongozi haraka pamoja na kufanya uratibu wa kupata ndege ya kunsafirisha huku wakifuatilia matibabu ya Lissu kwa karibu. Nafikiria kuwa, endapo Ndege aliyoiandaa Spika Ndugai ingempeleka Lissu Muhimbili, tungekuwa tunaongea nini?
Spika Ndugai, akiwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge wakiwasili Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.