Tundu Lissu awataja Majaji wa Kikwete wasio na Sifa (Kazi ndio inaanza)

Uteuzi wa majaji haujakaa vizuri ndio maana kila mara kunapokuwa na uapishwaji nguvu nyingi inatumika kutetea utaratibu wa uteuzi.
Kama vile leo jaji mkuu katika hotuba yake ikulu ametumia muda mwingi kutetea utaratibu huo mbovu sana na usio wa uwazi.
Ifike mahali uteuzi wa majaji uwe ni mchakato wa wazi na unaofahamika na sio kama ulivyo sasa
 
Lissu amkomalia JK

MNADHIMU wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, ameendelea kumwandama Rais Jakaya Kikwete, akisema baadhi ya majaji aliowateua hawana sifa, na kwamba viongozi wa serikali waliojitokeza kumpinga wameshindwa kujibu hoja.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana katika ofisi ndogo ya Bunge, Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), alisema kuwa alishatoa maelezo hayo hata katika Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Brigedia mstaafu Hassan Ngwilizi.

"Nilieleza jinsi rais alivyofanya uteuzi wa baadhi ya majaji pasipo kupata ushauri wa Tume ya Utumishi wa Mahakama. Wamekuwa wakijibu kiujumla, mimi niliwataja kwa majina yao na hata hili nilieleza katika Kamati ya Ngwilizi ambayo taarifa yake haikuwekwa hadharani pasipo sababu za kueleweka," alisema.

Alisema wanaotaka kujibu hoja zake wanapaswa kuweka hadharani orodha ya majina ya majaji waliopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama kuanzia mwaka 2005 wakati Rais Kikwete alipoingia madarakani.

Lissu aliwataja baadhi ya watu waliowahi kujitokeza kumjibu kuwa ni Naibu wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki, ambaye alisema kuwa serikali ina taarifa hizo na itazifanyia kazi.

Alisema kuwa msimamo huo ulikubaliwa na waziri wake, Mathias Chikawe na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ambao kwa nyakati tofauti walisema kuwa, endapo serikali itachukua hatua ambazo alipendekeza watakuwa wanaingilia uhuru wa mahakama.

Wengine waliojitokeza kujibu hoja yake ni Jaji Mkuu, Othman Chande na Jaji Kiongozi, Faki Jundu ambao walisema kuwa tuhuma zilizotolewa bungeni si za kweli.

Pia Rais Kikwete naye alikaririwa hivi karibuni akiwa jijini Arusha ambapo bila kumtaja Lissu kwa jina, alisema kuwa majaji wanateuliwa kwa kufuata utaratibu na wana sifa zinazostahili.

Ni kutokana na kauli hizo, Lissu alifafanua kuwa, katika hoja zake alisema kuna baadhi ya majaji waliteuliwa bila kuwa na sifa maalumu kama zilivyobainishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 109, kipengele cha 6, 7 na 8.

"Ibara hiyo ya 109 kipengele cha 6-8 kinasema; mtu anaweza kuwa Jaji iwapo tu ana shahada ya sheria kutoka katika chuo kinachotambuliwa kisheria, awe ameshakuwa hakimu, awe ameshakuwa wakili na kusajiliwa na sifa zote hizo ziambatane na utumishi wa miaka kumi mfululizo.

"Lakini sifa zote hizo lazima mtu anayeteuliwa kuwa Jaji awe nazo kwa miaka kumi mfululizo. Sasa badala ya kuzungumzia masuala hayo kwa ujumla jumla, ningependa wanaonijibu watamke wazi wazi Jaji Mbaruku Salumu Mbaruku alisoma chuo kipi na akapata shahada ya sheria iliyompa sifa ya kuwa jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar kabla ya kuteuliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Rufaa hadi sasa," alisema.

Alishangaa viongozi wanaojitokeza kumjibu akisema hata Katiba ya Zanzibar 94 (3) inasema; ili mtu achaguliwe kuwa jaji, ni lazima awe na shahada ya Chuo Kikuu.

"Huyu jaji ambaye anasoma sasa alipataje kuwa jaji kabla ya kuwa na shahada ambayo ndiyo sifa ya msingi?" alihoji.

Lissu aliwataja majaji wengine ambao wameteuliwa bila kuwa na sifa kuwa ni Fatuma Masengi, ambaye kwa mujibu wa Lissu alikuwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Singida na baadaye akawa Hakimu Mkazi kisha akaanza kujisomea Chuo Kikuu Huria na kuhitimu mwaka 2003 na kuteuliwa kuwa jaji mwaka 2006.

Alihoji kuwa kama katiba inaelekeza mtu awe jaji ni mpaka awe amekuwa hakimu kwa miaka 10, huyu alipataje kuwa jaji?

Majaji wengine waliotajwa ni Latifa Mansoor, ambaye pamoja na kuwa na shahada ya sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliyotunukiwa 1993, lakini alifukuzwa kwa udanganyifu na ubadhirifu akiwa mfanyakazi katika Manispaa ya Ilala.

Kwamba baadaye alipoibuka mwaka 2008 aliteuliwa kuwa jaji wakati hajawahi kuwa wakili, na kwa kuwa alifukuzwa katika utumishi wa umma.

Lissu pia alimlalamikia Rais Kikwete kwa kutumia vibaya madaraka yake kwani anateua majaji wa mikataba, ambao wameshastaafu na kulipwa mafao yao.

Aliongeza kuwa, majaji wengine waliteuliwa na Rais wakiwa wagonjwa ili waweze kupata fursa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi, ambapo alimtolea mfano Jaji Mwendwa Malecela kuwa tangu ateuliwe mwaka 2006 hajawahi kusikiliza kesi hata moja. Badala yake Lissu alidai kuwa jaji huyo huenda matibabu India tu.

Kufuatia utata huo, Lissu emeendelea kushikilia msimamo wake kuwa anakusudia kupeleka hoja binafsi bungeni ili Bunge liweze kuchunguza utendaji wa rais kuhusu uteuzi wa majaji.

Lissu alisema Bunge litaangalia kama rais ameteua majaji kwa mujibu wa katiba au ameikiuka, na kwamba yeye ana uhakika kuwa rais amekiuka katiba.

Chanzo: Tanzania Daima | Nov 29, 2012
Enzi hizo kukiwa na vyombo vya habari maana siku hizi kuna magazeti ya kufungia vitumbua
 
Huyo ndo Kikwete. Jamani, tufanyie kazi katiba mpya hata tukiwa na Rais boga imuongoze na kumuwajibisha katika utendaji wake. Imagine vyeo vingapi Vasco anavigawa namna hii...tutaangamia bandugu...!
  1. Jaji Mbaruku Salumu Mbaruku
  2. Jaji Fatuma Masengi
  3. Jaji Latifa Mansoor
  4. Jaji Mwendwa Malecela

Tafadhali mwenye CV za hawa jamaa aziweke tung'arishe macho.
tundu lisu hakukosea kabisa kusema kwamba kuna baadhi ya majaji hawana sifa za kuteuliwa kwao kushika nyadhifa hizo. mfano mzuri zaidi huyo jaji Latifa Mansoor, kwa kweli ana makandokando mengi sana, tangu alipoteuliwa kwa mara ya kwanza takribani miaka 12 bado anaonekana hafai kwenye nafasi hiyo. jaji Latifa Mansoor kwa kweli ana makandokando na uchafu mwingi sana, hakufaa kuteuliwa kuwa jaji.
 
WildCard, kama kuna kiini macho basi ni haya madudu yaliyomo ndani ya katiba yetu hii. Kwa mfano ibara ya 112 (1) ndio inayounda Tume ya utumishi wa mahakama, ambayo imepewa jina la tume ya ushauri wa uteuzi wa majaji na ajira ya mahakimu wa mahakama Tanzania bara.

Ibara ndogo ya (2) ya ibara hiyo inatamka kuwa:
Wajumbe wa tume hiyo watakuwa;
a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa mwenyekiti Mteule wa Raisi angalia Ibara ya 118(2) ya katiba
b) Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mteule wa Rais angalia ibara ya 59(1) ya katiba
c) Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufaa
atakayeteuliwa kwa ajili hiyo na Rais Mteule wa Rais angalia ibara ya 118(3) ya katiba na bado anateuliwa
baada ya kushauriana na Jaji Mkuu na Rais kuwa mjumbe wa Tume angalia ibara 112 (2) (c)
d) Jaji Kiongozi Mteule wa Rais angalia ibara ya 109(1) ya katiba
e) Wajumbe wawili watakaoteuliwa na Rais Wateule wa Rais angalia Ibara 112(2) (e)

Kwa vile hawa wote wameteliwa na Raisi kutokama na nyadhifa zao lazima kwa hali yoyote hiyo hawatampinga. Mtu yoyote mwenye akili akiona hii lazima atasema uteuzi wa majaji pamoja na kuwa anatokana na mapendekezo ya tume ya mahakama, kiukweli mapendekezo hayo ni ya Rais kwani tume yote ni ya Rais.

Tuache kuwa wabishi bila sababu, tuionee huruma nchi yetu, muundo huu haufai hata kidogo katika kuendeleza utawala wa sheria.

Tatambishia sana Tundu lakini kwa muundo huu wa tume ni vigumu sana kusema vinginevyo.

Kama waungwana tukubali maneno ya Tundu lissu na kutafuta njia mbadala ya kupata majaji kwa uwazi zaidi sio huu utaratibu wa sasa uliogubikwa na umangimeza.
rushwa imegubika mchakato wa uteuzi
 
Huyo Tindu Lissu ni Mdini tu.Amewalenga waislamu ili awachafue.Christian Democratic Movement in Action
uwongo
kuna ukweli kwenye suala hili.
jaji Latifa Mansoor hakufaa kuteuliwa kuwa jaji, hii si kutokana na yeye kuwa muislamu bali ni kwa sababu hana sifa za kuweza kuteuliwa
Huyo Tindu Lissu ni Mdini tu.Amewalenga waislamu ili awachafue.Christian Democratic Movement in Action. Sio aliyewateua ndio mdini. Hatahivyo kuna waislam wengi wenye sifa zilizotajwa na Mh. Tundu Lissu.
uwongo
kuna ukweli kwenye suala hili.
jaji Latifa Mansoor hakufaa kuteuliwa kuwa jaji, hii si kutokana na yeye kuwa muislamu bali ni kwa sababu hana sifa za kuweza kuteuliwa kuwa jaji, pia ana makandokando mengi sana, hafai kabisa kuwa jaji
 
Lissu amkomalia JK

MNADHIMU wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, ameendelea kumwandama Rais Jakaya Kikwete, akisema baadhi ya majaji aliowateua hawana sifa, na kwamba viongozi wa serikali waliojitokeza kumpinga wameshindwa kujibu hoja.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana katika ofisi ndogo ya Bunge, Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), alisema kuwa alishatoa maelezo hayo hata katika Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Brigedia mstaafu Hassan Ngwilizi.

"Nilieleza jinsi rais alivyofanya uteuzi wa baadhi ya majaji pasipo kupata ushauri wa Tume ya Utumishi wa Mahakama. Wamekuwa wakijibu kiujumla, mimi niliwataja kwa majina yao na hata hili nilieleza katika Kamati ya Ngwilizi ambayo taarifa yake haikuwekwa hadharani pasipo sababu za kueleweka," alisema.

Alisema wanaotaka kujibu hoja zake wanapaswa kuweka hadharani orodha ya majina ya majaji waliopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama kuanzia mwaka 2005 wakati Rais Kikwete alipoingia madarakani.

Lissu aliwataja baadhi ya watu waliowahi kujitokeza kumjibu kuwa ni Naibu wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki, ambaye alisema kuwa serikali ina taarifa hizo na itazifanyia kazi.

Alisema kuwa msimamo huo ulikubaliwa na waziri wake, Mathias Chikawe na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ambao kwa nyakati tofauti walisema kuwa, endapo serikali itachukua hatua ambazo alipendekeza watakuwa wanaingilia uhuru wa mahakama.

Wengine waliojitokeza kujibu hoja yake ni Jaji Mkuu, Othman Chande na Jaji Kiongozi, Faki Jundu ambao walisema kuwa tuhuma zilizotolewa bungeni si za kweli.

Pia Rais Kikwete naye alikaririwa hivi karibuni akiwa jijini Arusha ambapo bila kumtaja Lissu kwa jina, alisema kuwa majaji wanateuliwa kwa kufuata utaratibu na wana sifa zinazostahili.

Ni kutokana na kauli hizo, Lissu alifafanua kuwa, katika hoja zake alisema kuna baadhi ya majaji waliteuliwa bila kuwa na sifa maalumu kama zilivyobainishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 109, kipengele cha 6, 7 na 8.

"Ibara hiyo ya 109 kipengele cha 6-8 kinasema; mtu anaweza kuwa Jaji iwapo tu ana shahada ya sheria kutoka katika chuo kinachotambuliwa kisheria, awe ameshakuwa hakimu, awe ameshakuwa wakili na kusajiliwa na sifa zote hizo ziambatane na utumishi wa miaka kumi mfululizo.

"Lakini sifa zote hizo lazima mtu anayeteuliwa kuwa Jaji awe nazo kwa miaka kumi mfululizo. Sasa badala ya kuzungumzia masuala hayo kwa ujumla jumla, ningependa wanaonijibu watamke wazi wazi Jaji Mbaruku Salumu Mbaruku alisoma chuo kipi na akapata shahada ya sheria iliyompa sifa ya kuwa jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar kabla ya kuteuliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Rufaa hadi sasa," alisema.

Alishangaa viongozi wanaojitokeza kumjibu akisema hata Katiba ya Zanzibar 94 (3) inasema; ili mtu achaguliwe kuwa jaji, ni lazima awe na shahada ya Chuo Kikuu.

"Huyu jaji ambaye anasoma sasa alipataje kuwa jaji kabla ya kuwa na shahada ambayo ndiyo sifa ya msingi?" alihoji.

Lissu aliwataja majaji wengine ambao wameteuliwa bila kuwa na sifa kuwa ni Fatuma Masengi, ambaye kwa mujibu wa Lissu alikuwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Singida na baadaye akawa Hakimu Mkazi kisha akaanza kujisomea Chuo Kikuu Huria na kuhitimu mwaka 2003 na kuteuliwa kuwa jaji mwaka 2006.

Alihoji kuwa kama katiba inaelekeza mtu awe jaji ni mpaka awe amekuwa hakimu kwa miaka 10, huyu alipataje kuwa jaji?

Majaji wengine waliotajwa ni Latifa Mansoor, ambaye pamoja na kuwa na shahada ya sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliyotunukiwa 1993, lakini alifukuzwa kwa udanganyifu na ubadhirifu akiwa mfanyakazi katika Manispaa ya Ilala.

Kwamba baadaye alipoibuka mwaka 2008 aliteuliwa kuwa jaji wakati hajawahi kuwa wakili, na kwa kuwa alifukuzwa katika utumishi wa umma.

Lissu pia alimlalamikia Rais Kikwete kwa kutumia vibaya madaraka yake kwani anateua majaji wa mikataba, ambao wameshastaafu na kulipwa mafao yao.

Aliongeza kuwa, majaji wengine waliteuliwa na Rais wakiwa wagonjwa ili waweze kupata fursa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi, ambapo alimtolea mfano Jaji Mwendwa Malecela kuwa tangu ateuliwe mwaka 2006 hajawahi kusikiliza kesi hata moja. Badala yake Lissu alidai kuwa jaji huyo huenda matibabu India tu.

Kufuatia utata huo, Lissu emeendelea kushikilia msimamo wake kuwa anakusudia kupeleka hoja binafsi bungeni ili Bunge liweze kuchunguza utendaji wa rais kuhusu uteuzi wa majaji.

Lissu alisema Bunge litaangalia kama rais ameteua majaji kwa mujibu wa katiba au ameikiuka, na kwamba yeye ana uhakika kuwa rais amekiuka katiba.

Chanzo: Tanzania Daima | Nov 29, 2012
Enzi hizo....

Hongera sana JKMK
Hongera sana TAL
 
Enzi hizo....

Hongera sana JKMK
Hongera sana TAL
hata mimi nimeshangaa kuona kwamba huyo jaji Latifa Mansoor kumbe tayari alishaanza kutuhumiwa kuwa na makandokando mengi tangu zamani kabisa, nilikuwa sijui.baada ya kufuatilia humu mtandaoni ndiyo nakuja kugundua jambo hili. mimi binafsi nimeanza kuyabaini makandokando ya jaji huyu kuanzia mwaka 2020, kumbe tayari alishaanza kuwa nayo tangu miaka mingi iliyopita
 
Mungu atusaidie tu..
 
Back
Top Bottom