Vita vya Iraq, Marekani na washirika wenzake walikuwa wamepania kumtoa Sadam, na kweli walifanikiwa, lakini hawakuwa na plan ya maana juu ya Iraq baada ya kumuondoa Sadama, nini kimetokea Iraq? Vivyo hivyo Libya, nini kimetokea baada ya kumuua Gadaffi?
Turudi Tanzania, kwa miaka 20 sasa CHADEMA wamekuwa wanatueleza jinsi ufisadi unavyotuangamiza. Na ni miaka 7 saba tangu Dr Slaa ataje majina ya watu aliowaita vinara wa ufisadi. Leo hii wanatuambia kuwa wanataka kuondoa CCM kwa sababu ndiyo imelea ufisadi, lakini hapo hapo wanaanza kusajili watu wale wale waliowaita vinara wa ufisadi kutoka chama kile kile wanachokiita cha mafisadi. Tena wanasijili walioawaita vinara wa ufisadi. Hivi CHADEMA wana mpango gani ni hii nchi baada ya kuiondoa CCM? Post Sadam era or Post Gadaffi style?
Jambo la pili, Watanzania tuendelee kuamini kuwa CHADEMA wanaweza kuwamudu 'vinara wa ufisadi? Nasema hivyo kwa sababu, ndani ya wiki mbili, Lowassa ameweza kubalisha karibu kila kitu cha CHADEMA, amebadili mgombea, amebadili misingi ya waliyokuwa wanajivunia (anti ufisadi) na mbaya zaidi hata ndimi za viongozi wa CHADEMA kazibadilisha, sasa hivi wanamuita mtu shupavu, kiongozi safi! Kama amefanikiwa hayo ndani ya wiki mbili tu, kwanini tusiamini Lowassa atawapigisha deki na kuwapangia zamu ya kuosha vyombo hao CHADEMA?