Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mwanasiasa na Waziri Mstaafu, Sophia Simba, amesema ni wakati muafaka kwa wanawake waliokaa muda mrefu kupitia Viti Maalum Bungeni kuwaachia nafasi vijana ili kuendeleza harakati za uwezeshaji wa wanawake katika siasa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Februari 28, 2025, kwenye kongamano la kuadhimisha miaka 15 ya Taasisi ya ULINGO na miaka 30 ya Azimio la Beijing, Sophia Simba ameeleza kuwa Taasisi ya ULINGO, ambayo imefikisha miaka 15 tangu kuanzishwa kwake, imekuwa chachu kubwa ya kuwainua wanawake katika siasa bila kujali vyama vyao.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Soma Pia: Kipindi hiki cha Uchaguzi wanawake wanapata nafasi ya kutosha kushiriki kwenye masuala ya uchaguzi?
“ULINGO imekuwa na mafanikio makubwa. Tumeona wanawake wengi wakiwa wabunge, madiwani na hata vijijini akina mama wanajitokeza kugombea nafasi mbalimbali,” alisema Sophia Simba.