Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Hakuna tafsiri yoyote ya kisheria nchini inayosema kuna kitu kinaitwa kampeni kabla ya wakati

Mkuu kwa vifungu ulivyo nukuu mwenyewe huko juu, kampeni huanza baada ya nomination ya tume. Kwa tafsiri hiyo hakuna kitu kinaweza kuitwa kampeni so far sababu tume bado haijafanya nomination.

Ukiachana na tafsiri za kisheria, kwa maana tu ya kawaida unawezaje kusema mtu anafanya kampeni kabla ya uteuzi wa tume, je asipopitishwa na tume kugombea?

Unasema Magu alikuwa akitafuta wadhamini bali Lissu anafanya kampeni, unawezaje kutofautisha kutafuta udhamini na kufanya kampeni?

Je tume imeweka utaratibu wowote wa ni namna gani mtu akutane na wadhamini wake hadi useme anavyofanya Magu ni sawa na Lissu anakosea?
 
Sipati picha anayesikiliza hiyo kesi ya kampeni kama rais au kampeni kama mgombea. Akiwepo huyo mtafuta wadhamini
 

Kweli kabisa njia nzuri kutii sheria mbovu ni kuzivunja safi ,Lissu hawa mapolisi na AG makanjanja hawawezi kumpata.
 
Hii NEC kwani lini vile ilsema kitu dhidi ya CCM na vitimbi vyao vya kuvunja sheria na Katiba ya nchi ??

Kama chama hakivunji.. yaliyowekwa na NEC.. hutawasikia. Jibu hilo.. nenda nje ya boksi sasa..
 
Anapowaambia wananchi ambao ndiyo wapiga kura kuwa msifanye tena makosa kama kipindi kile bali muwachague wanaotokana na ccm. Hiyo imekaaje??
 
Anapowaambia wananchi ambao ndiyo wapiga kura kuwa msifanye tena makosa kama kipindi kile bali muwachague wanaotokana na ccm. Hiyo imekaaje??
Unfortunately bado ni sehemu ya majukumu yake kama rais; it sounds unfair but legal.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…