Lissu ni kati ya watu wachache sana hapa duniani wenye IQ kubwa, watu hawa hutokea kwa nadra mno. Sasa IQ yake kuchanganya na ujasiri alionao inakuwa ni ngumu mno kushindana na yeye kwa hoja, hoja yoyote ile iwe ya kijamii, kisayansi, kisiasa, kisheria ..ni lazima ujipange vilivyo.
Kwa mfano kile kitabu cha Maadili ya Uchaguzi ni kidogo mno, lakini wakisema wakijadili yale yaliyomo ndani kwa njia ya mdahalo basi hata hao waliokitunga watabakia midomo wazi kwa namna atakavyokidadavua... na sina uhakika kama wagombea wengine ukimwondoa Maalim kama wamekisoma chote na kukielewa vilivyo.
Sasa unapopambana na mtu wa namna hii kwa hoja lazima ujipange vilivyo vinginevyo anakutimuia vumbi vibaya sana. Ana uwezo wa kukukera ama kukufurahisha !!