Unko T
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 200
- 266
Katika madahalo wa Twitter Spaces wa Maria Sarungi, Tundu Lissu ameongea mambo mengi juu ya duru za siasa ya Tanzania na mistakabali wa chaguzi ya 2020 na nini kifanyike kabla ya 2025.
Likaja swali, je ni kwa namna gani tutaweza kupata tume huru ya uchaguzi na kuwa na chaguzi huru kwa maneno mengine demokrasia ya kweli. Lisu akatoa mtazamo wake kuwa mtu pekee atakayefanikisha au kukwamisha demokrasia ya kweli Tanzania ni rais SSH. Kama rais ataafiki katiba mpya, automatically tume ya uchaguzi na msajili wa vyama vya siasa hawata teuliwa na rais, vile vile wafanyakazi wa serikali hawatakua wasimamizi wa uchaguzi tena. Tume huru ya uchaguzi itaweka mazingira sawa ya kisiasa na kidemokrasia na hii tume itapatikana kwa katiba mpya tu.
Lissu akaendelea kusema kuwa Bunge la Ndugai sio kikwazo Kwani tangu enzi na enzi bunge hufuata maelekezo ya Ikulu. Bunge likiambiwa na rais kutekeleza jambo fulani, lenyewe hutii amri. Hivyo mtu wa kupambana nae ni rais na njia za kupambana nae ni mashinikizo ya kimataifa na pressure ya raia wa ndani ya Tanzania kudai katiba kwa nguvu zote.
Historia inamuangalia rais Samia kama atakua mbadilisha mchezo au na yeye atakua kama waliopita, walioogopa mabadiliko.