Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Maandalizi yamekamilika kwa ajili ya kumpokea Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Tundu Lissu, leo Ijumaa Februari 14, 2025, katika Manispaa ya Morogoro.
Lissu, ambaye yuko njiani kuelekea Ikungi, Singida, atasimama katika eneo la Msamvu kuwasalimia wananchi kabla ya kuendelea na safari yake. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Devota Minja, Mwenyekiti Lissu pia atapita na kusalimia wananchi katika maeneo ya Magubike (Kilosa) na Gairo Stendi.
Baada ya mapumziko Dodoma, Lissu ataendelea na safari yake kesho Februari 15, ambapo atafanya mkutano wake wa kwanza wa hadhara katika Jimbo la Ikungi tangu achaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa.
Minja amesema kuwa Lissu ameanza ziara yake Ikungi kama ishara ya heshima, kwani ndipo aliposhinda ubunge kwa mara ya kwanza, pia ni nyumbani kwake.