The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Soma: PICHA: Tundu Lissu aongezeka jopo la Mawakili kumtetea Dkt. Slaa Kisutu, kesi ya kusambaza taarifa za uongo
Nimeona hii issue watu wanaipost sana humu Leo kuhusu Senior Wakili Tundulisu kuwa mmoja wa mawakili waliomtetea Dr silaha huku wakati Kwenye Tovuti ya E- wakili ikionesha hauruhusiwi. Hili swala Lipo kisheria na nitalieleza kisheria inakuaje.
Kwa mujibu wa Sheria ya mawakili sura ya 341 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019, chini ya kifungu namba 38 kinayoa Grace period kwa mawakili WA chama Cha Tanganyika la society kurenew LESENI Zao Hadi tarehe 1/2.
General rule inatakiwa hadi kufikia tarehe 31/12/ wa mwaka husika basi mawakili wote wanatakiwa wawe wamerenew LESENI Zao Ili wazitumie mwaka mzima unaokuja unaanza na 1 January. Sasa basi chini ya kifungu hicho kinawapa muda mawakili kuhuisha au kurenew LESENI zao hadi tarehe 1 February mwaka unaofwata mfano mawakili wote ilitakiwa Hadi kufikia tarehe 31/12/2024 wawe wamerenew LESENI Zao, lakini kutokana na hiyo Grace Period mawakili wanaweza renew Hadi tarehe 1 February. Lakini pia wakati huo watakuwa wanafanya shughuli zote za mawakili
Hata kama bado hajarenew LESENI yake Hadi Leo hii. Na mfano akirenew kesho basi LESENI yake itasoma kuwa imeanza kufanya kazi tarehe 1 January yaani sawa na yule aliye renew 30/12/2024. Kwahiyo kwenye system ya mahakama inaonekana vile Hadi ulipie lakini haikunyimi kufanya kazi za mawakili ndio MAANA Lissu Yuko pale Leo na mawàkili wa serikali wangeweza kupinga lakini wanaijua hiyo Sheria na issue ya grace period.
Na pia Kuna Judgement nyingi zimeongelea hilo swala mfano na nyingine nyingi sana kwahiyo namalizia Kusema Lissu alikuwa pale kihalali kutokana na sheria.I stand to be corrected, lakini uje na hoja za kisheria na sio inavyotaka wewe.
Advocate Mkanji Kondele