Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kutoka kuwa mtafuta kura za huruma mpaka kuwa mchochezi ambaye anaachwa avunje Sheria

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Huyu Tundu Lissu alipokuja hapa Tanzania na CHADEMA kumpa ridhaa ya kugombea ubunge kama njia ya kumpoza baada ya wao CHADEMA kupanda njama za kumshambulia ili waichafue Tanzania, amekuwa kama mtu ambae hajui nini anakifanya majukwaani. Maana amekuwa mtu ambaye anaropoka maneno ya uchochezi ambayo nia yake ni kuleta fitina ili kuleta machafuko kwa nchi yetu.

Mgombea Urais ambae unatafuta kuwa rais wa JMT huwezi kuongea hoja ambazo hata mtu ambae hana akili timamu hawezi kuziamini. Mfano mgombea urais unasimama jukwaani na kusema eti Serikali inatengeneza njama za kuweka itilafu kwenye ndege unayosafiria ili upate ajali. Sasa kama una hakika na hili kwa nini usichukue hatua stahiki. Maana ndege unayosafiria ni ya kukodi. Sasa hao wamiliki wa hiyo ndege kwa nini usiwashitaki kwa kushiriki kupanga njama kubwa kama hizo? Maana hilo sio jambo dogo.

Unaenda Zanzibar bila aibu na bila kutumia busara unatamka kuwa, upinzani umekuwa unashinda uchaguzi wa Zanzibar tokea mwaka 1995. Je, unao ushahidi juu ya hili? Unaenda Zanzibar unadai kuwa eti Tanganyika inapeleka ubabe wake wa kijeshi Zanzibar je hiyo Tanganyika unayoisema ni ipi? Maana ibara ya pili ya katiba ya JMT ilifuta kitu kinachoitwa Tanganyika.

Sina mengi ya kusema ila wewe mgombea wa urais wa CHADEMA hakuna unachotafuta. Hii ni kwa sababu wewe unajitambua hufai kuwa rais wa JMT bali unaeneza siasa za chuki ili kuleta mifarakano na chuki ambayo matokeo yake ni vurugu.
 
Tukiwa wakweli mkuu, kati ya Lissu na Magufuli nani mpaka sasa amevunja waziwazi kanuni za uchaguzi?

Unafuatilia kwa makini mikutano ya kampeni ya mgombea wako kanda ya ziwa?

Kuna chuki kubwa sana anaimwaga kule na makosa na ukiukwaji mkubwa unafanyika mule.
 
Yapi hayo, fafanua ukiwa na ushahidi. Maana hili la ndege kufunguliwa nati ili afe hata kiziwi analijua
 
Narudia tena, hiyo 28/10 hakuna uchaguzi, bali ni kilele cha maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Sasa wewe mpiga debe hata ukisema hivyo mambo yataendelea kama kawaida!
 
Narudia tena, hiyo 28/10 hakuna uchaguzi, bali ni kilele cha maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Ahaaaa. Sasa kwa nini Lissu anahangaika kupanda ndege ambazo zimefunguliwa nati ili afe?
 
Ukiona hizo sera/hoja hazifai, basi mwambie mgombea wako akazipinge kwenye majukwaa wakati wa kampeni.

Hivi kati ya yeye na wale wanaowapigia magoti wapiga kura ili wachaguliwe tu, je ni nani anatafuta kura za huruma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…