Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kutoka kuwa mtafuta kura za huruma mpaka kuwa mchochezi ambaye anaachwa avunje Sheria

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kutoka kuwa mtafuta kura za huruma mpaka kuwa mchochezi ambaye anaachwa avunje Sheria

Naomba nikuulize.

Zanzibar ni NCHI au ni sehemu ya TANZANIA kama Mtwara, Mbeya, Mwanza, Kagera, Mara, Dodoma, Dar es salaam, Arusha, Morogoro, Shinyanga, Simiyu, Singida, Tabora, Kigoma, Ruvuma au Geita?

Je, Watanzania wa Bara Wenye shahada za kupigia kura wanaruhusiwa kupiga kura kumchagua Rais wa Serikali MAPINDUZI ya Zanzibar?

Je, Zanzibar kuna IKULU ambayo ni makazi ya Rais wa Serikali ya MAPINDUZI ya Zanzibar?

Zanzibar kuna ZEC na Bara kuna NEC,

Je, Viongozi wa ZEC huteuliwa na nani?

Je, WAGOMBEA wa Nafasi za Uongozi wa nafasi za KISIASA Zanzibar ni Wazanzibar tu au na Wabara wanaruhusiwa KUGOMBEA?

NINI MAHUSIANO YA ZEC NA NEC?

Kwa Nini TUME YA UCHAGUZI isiwe moja?

Je, Rais wa Serikali ya MAPINDUZI ya Zanzibar anaweza kutangaza VITA DHIDI YA ZANZIBAR?
Kasome katiba ya Zanzibar na JMT upate majibu. Maswali gani sasa haya?
 
mimi naamini uchaguzi huu ccm tutashinda kirahisi sana mpaka tutashangaa wenyewe
Lissu kila sinema anayotengeneza inagoma kutiki,mwisho atasema kuna njama za kumbaka ili tu aonewe huruma apewe urais
 
Huyu Tundu Lissu alipokuja hapa Tanzania na CHADEMA kumpa ridhaa ya kugombea ubunge kama njia ya kumpoza baada ya wao Chadema kupanda njama za kumshambulia ili waichafue Tanzania, amekuwa kama mtu ambae hajui nini anakifanya majukwaani. Maana amekuwa mtu ambaye anaropoka maneno ya uchochezi ambayo nia yake ni kuleta fitina ili kuleta machafuko kwa nchi yetu.

Mgombea urais ambae unatafuta kuwa rais wa JMT huwezi kuongea hoja ambazo hata mtu ambae hana akili timamu hawezi kuziamini. Mfano mgombea urais unasimama jukwaani na kusema eti Serikali inatengeneza njama za kuweka itilafu kwenye ndege unayosafiria ili upate ajali. Sasa kama una hakika na hili kwa nini usichukue hatua stahiki. Maana ndege unayosafiria ni ya kukodi. Sasa hao wamiliki wa hiyo ndege kwa nini usiwashitaki kwa kushiriki kupanga njama kubwa kama hizo? Maana hilo sio jambo dogo.

Unaenda Zanzibar bila aibu na bila kutumia busara unatamka kuwa, upinzani umekuwa unashinda uchaguzi wa Zanzibar tokea mwaka 1995. Je, unao ushahidi juu ya hili? Unaenda Zanzibar unadai kuwa eti Tanganyika inapeleka ubabe wake wa kijeshi Zanzibar je hiyo Tanganyika unayoisema ni ipi? Maana ibara ya pili ya katiba ya JMT ilifuta kitu kinachoitwa Tanganyika.

Sina mengi ya kusema ila wewe mgombea wa urais wa Chadema hakuna unachotafuta. Hii ni kwa sababu wewe unajitambua hufai kuwa rais wa JMT bali unaeneza siasa za chuki ili kuleta mifarakano na chuki ambayo matokeo yake ni vurugu.
Ukitaka kujuwa kuwa tundu lissu hana sera sikiliza tu hotuba zake yaani hatangazi sera ila anatangaza chuki kwawananchi ili waichukie nchi yao na viongozi wao hapo ajue kuwa hawezi kupata kura a kuonewa huruma au hawzi kupata kura kwa kusambaza chuki kwaraia atangaze sera ili watu wajue atawafanyia nini aache ujinga wake lakini anaweza kuwa anafanya hivyo akijua eti nchi haitatawalika asahau kitu kama hicho tuko makini na anajuwa urais hapati ndiyo maana anaropoka tu hovyo
 
Kasome maadili ya uchaguzi mkuu wa 2020
Umeshindwa kufanya attachment ili tusome. Ila huyu anaedai Tanganyika inapeleka majeshi yake kwa ubavu Zanzibar unaona yupo sawa? Na kama upinzani ulishinda Zanzibar akiambiwa athibitishe ataweza?
 
CCM huwa mkiona mtu anawaambia ukweli wananchi mnasema analeta uchochezi, ikiwa nyinyi mnatudanganya basi acheni Wapinzani watuambie ukweli, hakuna uchochezi hapo.
 
Narudia tena, hiyo 28/10 hakuna uchaguzi, bali ni kilele cha maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Mkuu kati ya komenti bora na fupi iliyotoka awamu hii ya tano

Hii inaweza kuwa ndio bora kuliko zoote

Embu chukua pepsii ya baridi hapo kwa mangi
 
Unatumia nguvu nyingi kumshambulia TL...

Unapoteza muda, kampeni za CCM tokea zimeanza sijaona jipya...
Kusema kweli imekuwa natumia nguvu nyingi?
Kama hujaona jipya ndio Lissu aanze kudanganya watu kuwa Tanganyika inapeleka majeshi kuwakandamiza wazanzibar? Hiyo Tanganyika anayoisema ipo wapi?
 
CCM huwa mkiona mtu anawaambia ukweli wananchi mnasema analeta uchochezi, ikiwa nyinyi mnatudanganya basi acheni Wapinzani watuambie ukweli, hakuna uchochezi hapo.
Hayo majeshi ya Tanganyika yapo wapi? Naomb unijibu maana tuna JWTZ. Huo ushindiwa wapinzani tokea 1995 anawez kuuthibitisha?
 
Narudia tena, hiyo 28/10 hakuna uchaguzi, bali ni kilele cha maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.

Huu ndo ukweli

Una akili sn mkuu.
tindo amerudia tena? Kama hakuna uchaguzi mbona mnahangaika kutaka kutuchafulia nchi yetu. Mara Lissu anataka kuwekewa sumu, mara ndege inafunguliwa nati ili ianguke, mara Tanganyika inaikalia kimabavu Zanzibar. Si mgelikalisha malio yenu nyumbani.
 
Kama wakati anajihami aligeuka na kulalia tumbo unategemea risasi zitampata kushoto tena?

Au ulimwona wakati anashambuliwa alikuwa amelala chali?
Wewe ulikuwepo? Je gari lake lilikuwa special si kama Magari mengine? Anamficha dereva ili asiseme ukweli kuwa hiyo ni hadithi ya kutunga ila alipigwa risasi nje ya gari hilo.

Si ajabu ile hadithi ya kuwa alifukaniwa ikawa ni ya kweli. Turejee katika kampeni, wewe unaona akili zake zipo Sawa hasa baada ya hotuba ya kitoto ya huko Zanzibar?

Unapinga muungano wakati unagombea kuwa rais wa muungano! Hajitambui huyu ingawa kuna wengi wanaomlamba Masaburi
 
Unakumbuka kilichotokea UCHAGUZI wa 2000 kule Pemba? Nini kilifanya Jecha afute matokeo ya uchaguzi kule Zanzibar mwaka 2015?
Mimi sipendi hearsays kama kwenye kahawa. Kama uno ushahidi tupandikiwe hapa. Jecha alifuta matokeo sababu kuna mtu alifanya makosa akajitangaza kuwa ameshinda.
Weka ushahidi wa matokeo ya upinzani kushinda Zanzibar tokea 1995.
 
Ngoja aendelee kukuchochea upate raha huko manyu
 
Umeshindwa kufanya attachment ili tusome. Ila huyu anaedai Tanganyika inapeleka majeshi yake kwa ubavu Zanzibar unaona yupo sawa? Na kama upinzani ulishinda Zanzibar akiambiwa athibitishe ataweza?
Attachment nilifuta, kwa sababu niliflash Simu
Ni kweli Maalim Zanzibar amekuwa akishinda tangu '95
 
Mimi sipendi hearsays kama kwenye kahawa. Kama uno ushahidi tupandikiwe hapa. Jecha alifuta matokeo sababu kuna mtu alifanya makosa akajitangaza kuwa ameshinda.
Weka ushahidi wa matokeo ya upinzani kushinda Zanzibar tokea 1995.
Hivi unazijua exception za hear say evidence kwenye sheria ya ushahidi cap 6?
And hata kama akiweka huo ushahidi hautakuwa na umuhimu wowote kwa sababu ya Ouster clause ya kwenye katiba inayokataza matokeo ya Urais kuhojiwa,
 
Attachment nilifuta, kwa sababu niliflash Simu
Ni kweli Maalim Zanzibar amekuwa akishinda tangu '95
Weka matokeo hapa ya Zec,tena yawe authentic. Mnashabikia uchochezi wa kipuuzi. Vurugu zikianza nyie mnajificha uvunguni
 
Hivi unazijua exception za hear say evidence kwenye sheria ya ushahidi cap 6?
And hata kama akiweka huo ushahidi hautakuwa na umuhimu wowote kwa sababu ya Ouster clause ya kwenye katiba inayokataza matokeo ya Urais kuhojiwa,
Acha kujibaraguza, najua vizuri sana nini maana ya real evidence na hearsay evidence. Wewe ulikuwepo Zanzibar wakati hayo matokeo yanajumuishwa na kusainiwa tokea 1995-2015? Lissu alikuwepo na aliona kwa macho yake?
 
Back
Top Bottom