Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

kweli kabisa Dr.harith ghassany anaelezea mambo mengi sana mabaya yaliyofanywa na Nyerere 1.usanii kwenye muungano 2.kuzorotesa ustawi na maendeleo ya uislamu pale aliporatibu mpango wa kuua jumuiya ya waislam ya afrika mashariki 3.kuchochea vurugu mbalimbali africa mfano mgogoro wa biafra_nigeria , vita ya kagera 4.mgogoro wa burundi 5.kufukuza kazi wazanzibari waliokuwa wanahoji muungano....
nitaendelea
 


Kinachoendelea Zanzibar na mtiririko wa hoja ya Lissu kuhusu Nyerere !.Je kuna ukweli kuwa ugonjwa wa kuishi kwa Uongo unazidi au kuelekea kuambukiza kizazi kijacho?

 
Na utakaporudi utueleze jinsi Nyerere alivyochochea mgogoro wa Burundi na vita vya Kagera.
 
Ni huyu huyu Tundu Lisu na wenzake mpaka alikuwa anatoka mapovu kwenye kona za midomo yake kuipinga na kuikata Zanzibar, alifikia mahali pa kumtukana Mlm.Nyerere, leo hii maajabu ya Musa ndiyo amegeuka kuwa msemaji Mkuu wa Wazanzibari na kwamba anawapigania ndani ya serikali ya Muungano!

Kama kuna mtu ni opportunitist kwenye hii Dunia basi Tundu Lisu ni mmoja wao, maisha yote Bungeni amekuwa akingombana na Wabunge wa Zanzibar na kuwakebehi leo hii kageuka kuwa mtetezi wao, kweli Duniani kuna watu na viatu!
 

Ni bora lissu kuliko wale waliofuta uchaguzi zanzibar baada ya kuona wameshindwa.
 
Jamani huyo Toto Tundu Lissu msameheni bure tu yeye ni mtu wa mihemko tu,kaingizwa chaka na kushadidia kuwa eti Baba wa Taifa alianzisha vita na Uganda kwa sababu zake mwenyewe za kisanii labda nadhani Kipindi hicho alikuwa hajazaliwa so hajui jinsi vita ilivyoanza,hajui jinsi tulivyoanza kufundishwa namna ya Kuchimba Mahandaki ya L,Y na jinsi ya kukimbilia humo once tukisikia miungurumo mikali ya ndege za kivita,mafunzo ya ulinzi wa mgambo makazini kuchukua Tahadhali kwa mtu yeyote asiyejulikana na mengine meengi.
 

Siyo Tundu Lissu tu,hata mkapa aliwahi kusema moja ya mambo yaliyoangusha uchumi ni vita "visivyo na sababu" na nyerere alikuwepo hai.
 
zimu wa Mwalimu unamtafuna Lissu, haji aitetee nchi yake au mabwana wanaomtuma.
Haya mabomu yanarindima sasa, hata handaki hajui kuchimba!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…