Bibie mimi naona hatutaelewana ila labda nikupe darasa ambalo Mohamed Said haijui ama huyo Mwenye Link kasema uongo. hakuna Sheikh alikamatwa na kutiwa ndani baada ya Uhuru hakuna.
Kuna matukio mawili makubwa abayo yalitokea nayo ni mwaka 1964 mapinduzi ya Zanzibar ambayo kuna masheikh walikamatwa kwa hifadhi yao kutokana na mgogoro wa kusaka viongozi wenye mahusiano na utawala wa Sultan.na wengi wa hawa walikuwa Wangazija ambao Nyerere aliwapa hifadhi bara hata wakaweza kuendelea na shughuli za EAMWS bara tena basi wakapewa ushirikiano na serikali ya Nyerere. wengine wakapigania mapinduzi ya Comoro ambayo walifanikiwa na wanalindwa hadi kesho. Kukawa na special bond ya utawala wa Comoro na Tanzania. Mwaka huo huo nchini walichaguliwa viongozi wa EAMWS wengine wakiwa ni wanachama wa TANU na walitambuliwa kiserikali hata wengine kuwa balozi nchi za nje. Wakapewa fedha kusafiri nje kutafuta sponsors na kadhalika.
Hivyo Link niliyokuonyesha imekuonyesha Sheikh Hassan Bin Amir akiwa huru nje mwaka 1964 na akisalimiana na Nyerere, hakuwa ndani kama inavyodaiwa na watu baada ya Uhuru ama mwaka huo. Mwaka 1968 - 69 kulitokea machafuko mengine ambayo Masheikh hao walisemekana kutaka kuipindua serikali ya Tanzania (Zanzibar) baada ya Muungano. Kwa kutokubaliana na aidha Muungano wenyewe, uongozi wa Nyerere kwa ujumla ama penigne kuvunjika kwa EAMWS wanajua wao siri hiyo. Siri ikafichulliwa ikawa kamatakamata mji mzima, Masheikh wakakamatwa na baadhi ya Viongozi kina Abdallah Kassim Hanga na kadhalika. Lakini inasemekana sababu kubwa ilikuwa ni serikali ya Karume kule Zanzibar na sio Nyerere kutokana na sheria mpya alotangaza Karume..
Kwa hiyo ni rahisi sana kumsema Nyerere dhidi ya Waislaam kama utasikia sana tungo za watu walomchukuia Nyerere kina Takadir na kundi lake. Hata siku moja hawasemi ukweli juu yao wao na mpango wao dhidi ya serikali ya Muungano ama yeye kama Mkristu kafanya lipi baya kwa Ukristu wake. Nijuavyo mimi hata kuvunjika kwa EAMWS lilikuwa pendekezo la Waislaam wenyewe wa bara ambao walikiona chombo hicho kimeshikwa na wageni. Watakata chombo chao na wazir wa sheria wakati huo alikuwa Abeid Karume. Waislaam wakapitisha wao wenyewe chombo hicho kivunjwe na sheria ikapitishwa na waislaam wenyewe. Ndio kuundwa BAKWATA in replacement ya EAMWS na sio BAKWATA kama chombo kinacho define dini au kuongoza dini, bali NGO kwa welfare ya Waislaam. Leo hii Bakwata ndio Uislaam na ndio waamuzi wa mambo yote ya Waislaam toka kufunga Ramadhan na kutangaza sikukuu za dini..