Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tundu Lissu ni mmoja kati ya viongozi wakuu wa chademaa na mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni. Kwa ufupi ni kigogo mmoja wapo wa upinzani Tanzania, tena ni mwanasheria wa chadema.

Anaponukuliwa huo ndiyo unakuwa msimamo wa upinzani rasmi, sidhani kama anawezza kusema na kuongea kwenye vyombo vya habari kinyume na sera za chadema, angeshaitwa msaliti.

Kwa hiyo anaponukuliwa "Tundu Lissu amepasua jibu ambalo wengi huwa wanaogopa kulipasua pale aliposema kuwa Mwl. Nyerere alikuwa ni "msanii wa kisiasa" (post #1 ).

Huo ni mtazamo wa chadema.

Kwa hilo naiunga mkono chadema, ni ukweli usiopingika.

Heko Tundu Lissu kwa kuwa mkweli kwenye hilo.
 
...samahani dada. Nilisahau kuwa huwa mnafundishwa kukariri.

Mwalimu alisema UMMA wa WAZANZIBAR wakisema wanataka bila USHAWISHI TOKA NJE.. na sio WANASIASA wa ZANZIBAR wakitaka na USHAWISHI TOKA NJE...

Ugumu wa lugha kuelewa uko wapi hapo...

Tundu Lissu anadai, Mwl. Nyerere hakukataa hoja ya Muungano kwa sababu safi kabisa, bali aliwaweka kizuizini wale waliohoji Muungano. Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uwongo na hakuweza kusema kweli.

Chanzo - Post #1
 
Huyo Tundu Lissu alikuwepo wakati baraza la Mapinduzi walipokataa hoja ya Jumbe? anajua kwamba Jumbe tayari alikuwa anataka kutoroka nchini kwenda.. na akanyang'anywa passport, treason maana yake nini? Kama Serikali ya Mapinduzi ambayo ndiyo iliungana na TANU wamekataa na kutaka akamatwe, Nyerere angefanya nini kuwalazimisha? Na kwa nini basi walimchagua Mwinyi baada yake wasifanye vikao ama maandamano kumpinga Nyerere!

Tundu Lissu ni mpayukaji hana hekima zaidi ya kufundishwa kubishana maana ndio kazi ya mawakili..
 
Kwanini Tundu Lissu hakujitia uchizi na kutamka haya maneno kabla Mzee hajafariki. Kutoa lugha kama hizi wakati mlengwa ameshakuwa mfu ni sawa na kupoteza muda na pumzi zako.
 
Wapinge walawitiwe? hivi hujui jinsi Wazanzibari wanaopinga wanafanywa nini? mpaka leo hii uamsho hata Zanzibar hawafungwi wala hawahukumiwi kwa "makosa" wanayoyafanya Zanzibar, tumeona Masheikh na wengineo juzi tu wakiletwa kuhukumiwa bara kwa "makosa" ya Zanzibar, mpaka wanalalamika kulawitiwa. Huyajuwi hayo?

Ukimuona Mzanzibari kaamuwa kusema ukweli ujuwe kishajitoa mhanga huyo. Kama kulawitiwa haya, kama kufa haya.
 
Kwanini Tundu Lissu hakujitia uchizi na kutamka haya maneno kabla Mzee hajafariki. Kutoa lugha kama hizi wakati mlengwa ameshakuwa mfu ni sawa na kupoteza muda na pumzi zako.
Sio tu kupoteza muda ni ukosefu wa nidhamu, jeuri na Ulimbukeni.. alistahili kuwajibishwa na Chadema kwanza kabla ya yote!
 
Wapinge walawitiwe? hivi hujui jinsi Wazanzibari wanaopinga wanafanywa nini? mpaka leo hii uamsho hata Zanzibar hawafungwi wala hawahukumiwi kwa "makosa" wanayoyafanya Zanzibar, tumeona Masheikh na wengineo juzi tu wakiletwa kuhukumiwa bara kwa "makosa" ya Zanzibar, mpaka wanalalamika kulawitiwa. Huyajuwi hayo?

Ukimuona Mzanzibari kaamuwa kusema ukweli ujuwe kishajitoa mhanga huyo. Kama kulawitiwa haya, kama kufa haya.
Kwa heshima na taadhima bibie futa maneno haya kwa sababu swala la UAMSHO limezingatia Uislaam dhidi ya Ukristu na sii haki wala njia nzuri ya kuomba kujitenga, ila ina ushawishi ambao sio tu kwamba hawa wanataka kujitenga isipokuwa kuzalisha fitna. na ya Masheikh hata bara wametendewa hayo toka kina Sheikh Kassim bin Juma kwa madai ya Bakwata tu, Rais alikuwa Mwinyi Muislaam na Mzanzibar! Nyerere alihusikaje? haya ya Ponda rais nani? naye tusubirie yalomkuta huko. Lakini bado wapo watu wanataka kumhusisha Nyerere kwa kila kitu, we do have the facts..

Swala la Jumbe nalijua vizuri sana na nashukuru Mungu mimi sii msahaulifu. Jumbe sii tu alokwenda kinyume cha Baraza la Mapinduzi toka nyuma kama unakumbuka kina HH na AB. Huyu Salim ni majuzi tu baada ya ukali wa BLM kupunguza makali lakini zamani alikuwa wanted na kina Babu, BLM walikuwa hawachezi na mtu. Nyerere kawaokoa wengi ambao kama wangepelekwa Zanzibar basi leo wasingekuwa hai. Leo watu mnasahau kwamba Zanzibar ilifanyiwa Mapinduzi na dhana ya utawala huo una nguvu kubwa hadi kesho.

Maswala mengi watu wanamsema Nyerere lakini wanashindwa kuelewa kwamba wakati ule Usalama wa Taifa ulikuwa sii mchezo wala sii kitu cha kuchezea na haswa Zanzibar. Ukipingana na AfroShiraz maamuzi wanayo baraza la Mapinduzi wala sio makamu wa rais au rais wa Zanzibar. Vikao vya BLM ndio vilikuwa na maamuzi yote na Nyerere ni mtekelezaji tu tena aidha awakimbizie Bara au akubali yaishe. Hata swala la katiba Mpya tujiulize kwa nini wajumbe wa CCM Zanzibar (BLM) hawataki serikali 3? kwa nini hawakuwa pamoja na UKAWA ikiwa kweli wanataka kujitenga kwani Nyerere bado yupo?
 
Nilipokwenda Canada, hata CUF ilikuwa haijukani, nimeondoka kwa njaa kweli iliyokuwepo Tanzania, hapo mwalim wako analijuwa hilo na hajakosea.

Hata sukari ilikuwa foleni, kama si njaa nini hicho.

Tundu Lisuu anasema kuwa "matatizo ya kiutawala toka mwaka wa 62 mpaka leo hii ni ya mwalimu".

Canada hii hii ya makafiri?
 
Lissu we tahira kweli, piga kelele kuhusu mali za nchi zinavyozidi kuibiwa. Hakuna mwanadamu atayeweza kumchafua Nyerere, matendo yake yameongea yenyewe.
 
..hebu mfuatilie Tundu Lissu kwenye hiyo link hapo chini.

..tueleze ni wapi unakubaliana naye, na ni wapi hukubaliani naye.

..ila kwa taarifa tu, Tundu Lissu ameanza hizi harakati za kupinga ufisadi zamani kidogo. Tangu yuko chuo kikuu na huenda kabla ya hapo. Hata kwenye lile sakata la mradi wa kamba kule Rufiji delta, Tundu Lissu alikuwa mstari wa mbele kupinga mradi ule.

MAHOJIANO YA TUNDU LISSU na MKASI TV: https://www.youtube.com/watch?v=TSGp_DXdBDM

cc Tetty, Sikonge, Mkandara, FaizaFoxy, Mzito Kabwela
 
Last edited by a moderator:
Canada hii hii ya makafiri?

Wanasilimu kwa makundi North Amerika yote, ngoja tukianza South America ndiyo basi, Ukristo kwishnei, makanisa yanauzwa huko kama njugu. Mnabaki Waafrika tu kuabudu mwanasesere wa kizungu aliyevishwa nepi. Wenzenu wamestuka wanaingia kwenye ukweli makundu kwa makundi.
 
Kwa heshima na taadhima bibie futa maneno haya kwa sababu swala la UAMSHO limezingatia Uislaam dhidi ya Ukristu na sii haki wala njia nzuri ya kuomba kujitenga, ila ina ushawishi ambao sio tu kwamba hawa wanataka kujitenga isipokuwa kuzalisha fitna. na ya Masheikh hata bara wametendewa hayo toka kina Sheikh Kassim bin Juma kwa madai ya Bakwata tu, Rais alikuwa Mwinyi Muislaam na Mzanzibar! Nyerere alihusikaje? haya ya Ponda rais nani? naye tusubirie yalomkuta huko. Lakini bado wapo watu wanataka kumhusisha Nyerere kwa kila kitu, we do have the facts..

Swala la Jumbe nalijua vizuri sana na nashukuru Mungu mimi sii msahaulifu. Jumbe sii tu alokwenda kinyume cha Baraza la Mapinduzi toka nyuma kama unakumbuka kina HH na AB. Huyu Salim ni majuzi tu baada ya ukali wa BLM kupunguza makali lakini zamani alikuwa wanted na kina Babu, BLM walikuwa hawachezi na mtu. Nyerere kawaokoa wengi ambao kama wangepelekwa Zanzibar basi leo wasingekuwa hai. Leo watu mnasahau kwamba Zanzibar ilifanyiwa Mapinduzi na dhana ya utawala huo una nguvu kubwa hadi kesho.

Maswala mengi watu wanamsema Nyerere lakini wanashindwa kuelewa kwamba wakati ule Usalama wa Taifa ulikuwa sii mchezo wala sii kitu cha kuchezea na haswa Zanzibar. Ukipingana na AfroShiraz maamuzi wanayo baraza la Mapinduzi wala sio makamu wa rais au rais wa Zanzibar. Vikao vya BLM ndio vilikuwa na maamuzi yote na Nyerere ni mtekelezaji tu tena aidha awakimbizie Bara au akubali yaishe. Hata swala la katiba Mpya tujiulize kwa nini wajumbe wa CCM Zanzibar (BLM) hawataki serikali 3? kwa nini hawakuwa pamoja na UKAWA ikiwa kweli wanataka kujitenga kwani Nyerere bado yupo?

Wewe wacha porojo, hakuna Sheikh wakati wa Nyerere ambae hajashikwa au kuhamishwa, kuanzia kina Sheikh Hassan Bin Ameir, Badawi, Sheikh Nurdin, Sheikh Hashim na wengine wengi nimekutajia hao maarufu tu, amma walishikwa wakawekwa ndani kwa vitisho amma walihamishwa makazi yao kwa nguvu.

Labda wewe unayajuwa ya wakati wa Mwinyi tu. Jisomee:

[SIZE=+2]Alichokifanya Nyerere baada ya uhuru[/SIZE]
Kilichofuata baada ya kupatikana uhuru ilikuwa ni kukamatwa, kuwekwa kizuizini na kuhamishwa kwa masheikh na Waislamu wengine waliodhaniwa kuwa wanapinga utawala wa Nyerere.

Mashuhuri miongoni mwao walikuwa: Abdillah Schneider Plantan, Sheikh Abdulkarim Abdulwahid, Maalim Popo Saleh, Suleiman Masudi Mnonji, Ali Migeyo, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sharff Hussein Badawiy, Shariff Mwinyibaba na Shariff Adnan

Wengine ni Bilali Rehani Waikela, Sheikh Jumanne Bias, Maalim Matar, Abdalah Mwamba, Sheikh Hashim Haji Abdallah, Sheikh Nurdin Hussein, Salum Abdallah Popo, Sheikh Mzee Ali Comoriam, Sheikh Al Amin Maftah, Rajab Kiguu cha Mbuzi na wengine wengi.

Lakini ukweli ulikuwa kwamba si wote katika wale waliokamatwa na kuwekwa kizuizini walijihusisha na siasa. Baadhi yao walikamatwa kwa sababu tu walikuwa wakishirikiana na wale waliodhaniwa ni wapinzani wa Nyerere.

Maalim Matar na Shariff Adnan walifungwa jela kwa sababu tu walihusika na msikiti wa Badawiy mjini Dar es Salaam ambako Sheikh Hassan bin Amir, wakati huo akichukuliwa kuwa ndiyo roho ya waumini wa Tanganyika, alikuwa ikiendesha madrasa yake kila magharibi pale msikitini.

Shariff Hussein na nduguye Mwinyibaba walihamishiwa Kenya, walikotoka si kwa sababu walikuwa wamejishughulisha katika harakati za kuipinga serikali, ila lakini kwa sababu walikuwa waangalizi wa msikiti wa Badawiy.

Sheikh Mzee Ali Comorian alitiwa kizuizini kwa sababu kila mara alikuwa akifuatana na Sheikh Hassan bin Amir kama vile alikuwa kivuli cha sheikh. Huenda kile kilichomfanya Nyerere kuwatia kizuizini masheikh na wengine kuhamishwa ni kufuata ule msemo wa Biblia usemao, 'yule ambae hayuko nasi basi ni dhidi yetu'.

Jinsi siasa na za Tanzania zilivyobadilika na jinsi Nyerere alivyoanza kuonesha uadui dhidi ya Waislamu kulimsikitisha sana Abdulwahid. Alishindwa kuelewa uhasama huu ulikuwa unatoka wapi. Alihisi kuwa anahusika na yale yaliyokuwa yanawapata Waislamu. Mawazo haya yalimzonga kama jinamizi. Kwa ufahamu wake alikuwa akidhani matatizo yote ya udini walikuwa wameyashinda toka miaka ya 1950. Mwaka 1953 Abdulwahid akiwa Muislamu na akiungwa mkono na Al Jamiatul Islamiyya aligombea kiti cha urais wa TAA na Nyerere, Mkatoliki.

Abdulwahid alishindwa uchaguzi ule. Waislamu hawakuuchukulia uchaguzi ule kama uchaguzi kati ya Muislamu na Mkristo. Kilichotazamwa ni uwezo wa wagombea.
Nyerere alikuwa amemzidi Abdulwahid na kwa ajili hii alichaguliwa kuiongoza TAA. Abdulwahid alikumbuka ugomvi wa Sheikh Suleiman Takadir wakati ule Mwenyekiti wa Baraza La Wazee wa TANU. Sheikh Takadir aliwaonya Waislamu wachukue tahadhari kwani Nyerere atakuja kuwapendelea Wakristo wenzake pale atakaposhika madaraka. Kama walivyofanya Waislamu wengi, Abdulwahid alimuunga mkono Nyerere na kumpinga Sheikh Takadir.
Wakati ule Abdulwahid aliamini kama Waislamu wengi walivyoamini kuwa Sheikh Takadir alikuwa anataka kuleta siasa za kibaguzi ambazo alikuwa anaziegemeza katika dini. Abdulwahid aliona udini aliokuwa anataka kuuleta Sheikh Takadir lilikuwa jambo ambalo lingeiletea hatari Tanganyika.
Abdulwahid alikufa mwaka 1968 wakati nchi ikiwa imegubikwa na hasama za chinichini kati ya Waislam dhidi ya serikali ya Nyerere ambae sasa alikuwa amehodhi madaraka yote katika serikali.
Umoja wa kitaifa, moja ya maadili ambayo yeye(Abdulwahid ) aliyapigania katika maisha yake yote katika siasa ulikuwa unahatarishwa. Halikadhalika umoja wa Waislamu ulikuwa unaelekea kuvunjika. Kulikuwepo na kuwekwa kizuizini kwa masheikh chini ya Preventive Dentation Act of 1962.
Baadhi ya masheikh waliotiwa gerezani walikuwa watu waliomuunga yeye mwenyewe mkono wakati anaunda TANU. Baadhi yao aliwashawishi kumuunga mkono Nyerere na TANU katika kile kipindi kigumu cha harakati za kudai uhuru. Mwanakamati wa Kamati Ndogo ya Siasa ya TAA, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, kiongozi wa ngazi ya juu kabisa kwa Waislamu alikuwa amekamatwa na kuondolewa nchini na kurudishwa kwao Zanzibar kwa amri ya Nyerere. Sababu iliyotolewa ya kukamatwa kwa Sheikh Hassan bin Amir ilikuwa alikuwa ati 'akipanga njama ya kupindua serikali'.
Sheikh Hassan bin Amir alikuwa kati ya Waislamu wachache ambao walithubutu kusimama kidete dhidi ya serikali na kutoa mawazo yake kuhusu jinsi serikali ilivyokuwa ikiwakandamiza Waislam. Kabla hajafa Abdulwahid alikuwa akifikiwa na habari kuwa Nyerere alikuwa alikuwa akiendesha kampeni makini sana ndani ya chama kuwafuta Waislamu ndani ya TANU.
Abdulwahid alikuwa anafahamu matokeo ya kuvunjika kwa umoja wa Waislam. Yeye alikuwa anajua vyema nguvu ya umoja wa Waislamu wakati walipokuwa wanapigania uhuru wa Tanganyika.
Abdulwahid halikadhalika alikuwa anafahamu nguvu ya wale waliokuwa nyuma na njama zile za kuwagawa Waislamu katika makundi hasimu. Vilevile alikuwa anatambua hofu na watu wote waliokuwa nyuma ya njama zile.
Alifahamu kuwa wale aliowapokea na kuwatia katika harakati za kudai uhuru sasa walikua na hofu na Uislam. Kama Uislamu ulitumika kuwaondoa wakoloni Uislam hautashindwa kuwatoa wao madarakani. Uislam ikiwa itkadi ya kupinga ukoloni sasa ilikuwa ni tishio kwa Ukristo katika Tanzania huru.
Kabla hajafariki dunia Abdulwahid alifanya mazungumzo na Nyerere. Mazungumzo haya baina ya Abdulwahid na Nyerere yalifanyika katika miezi ya mwisho ya mwaka 1968 wakati mashekhe na Waislamu mashuhuri wanasombwa na kutupwa gerezani. Abdulwahid na Nyerere walikuwa wametoka mbali. Watu hawa walikuwa marafiki wa zamani. Huenda kama isingelikuwa kwa msaada wa Abdulwahid historia ya TANU na ya Nyerere mwenyewe zingechukua mkondo tofauti.
Mazungumzo haya yalikuwa muhimu kwa Abdulwahid kwa sababu kwa kiasi fulani alihisi anahusika na yale yaliyokuwa yakiwasibu Waislamu, wale kutoka Dar es Salaam. Taarifa za Waislamu kukamatwa usiku na kuwekwa kizuizini zilikuwa zikimfikia karibu kila siku. Abdulwahid hakuweza kujifanya kuwa haathiriki na matokeo yale. Baadhi ya watu ambao Nyerere alikuwa anawatupa gerezani walikuwa watu ambao yeye Abdulwahid binafsi walimuunga mkono wakati anaanza siasa na watu ambao aliwashawishi wamkubali Nyerere wakati wa kuundwa TANU.
Abdulwahid alimwambia Nyerere huenda yeye akawa hana hisia wala uhusiano wowote na watu ambao yeye anatia sahihi wakamatwe na kutupwa gerezani. Lakini kwake yeye hao ni jamaa zake anaokutananao ama msikitini au mitaani. Yeye kama mtu anayeishi miongoni mwa Waislamu na zile familia zao alikuwa anaelewa majonzi yao.
Abdulwahid alimwambia Nyerere kwamba watu wale wanajua kuwa yeye, Abdulwahid ndiye aliyesamsaidia Nyerere wakati akiwa mgeni mjini Dar es Salaam, watu wakamjua na kumkubali na hivyo kuja kuweza kufika hapo alipofika.
Abdulwahid alimwambia Nyerere kuwa ndugu na jamaa za wafungwa wale wanamjia wakimbembeleza amsihi Nyerere awatoe ndugu zao jela. Abdulwahid alimwambia Nyerere kwamba kule kuwatia watu kizuizini ni uonevu kwa sababu wale watu hawana uwezo wa kupindua serikali yake.

Kwa sauti ya masikitiko Abdulwahid alimaliza maelezo yake kwa kumwambia Nyerere 'Naondoka hapa nikiwa nataka kuamini kuwa wewe Julius Nyerere, leo hujatugeuka.' Kwa maneno hayo Abdulwahid aliaga na kuondoka.

Alichosikia Nyerere kuhusu Abdulwahid baada ya maneno yale ilikuwa taarifa ya kifo chake jioni moja Jumamosi tarehe 12 Oktoba, 1968. Mkewe Mama Maria Nyerere, alizirai aliposikia habari zile za msiba. Alikuwa Abdulwahid ndiye aliyewapokea yeye na mume wake mara ya kwanza walipokuja Dar es Salaam.

Mazishi ya Abdulwahid Sykes yalifanyika siku ya Jumapili tarehe 13 Okrtoba. Mazishi yake yalikuwa makubwa yasiyo kifani. Ukitoa mazishi ya mwaka 1950 ya Sheikh Idrissa bin Saad, muasisi na Khalifa wa Tariqa Askariya na mazishi ya Sheikh Kaluta Amri Abeid mwaka 1963, Dar es Salaam ilikuwa haijapata kushuhudia mazishi kama hayo. Gerezani yote ambako Abdulwahid aliishi katika utoto wake na mahali ambapo alianza harakati zake dhidi ya Waingereza ilikuwa kama vile imesimama hakuna kinachoendelea ila maziko ya Abdulwahid. Hii ilikuwa pamoja na sehemu nyingine zilizozunguka Kariakoo kama Misheni Kota na Kisutu.

Gerezani kwa hakika ilikuwa na mwito wa pekee. Ilikuwa ni kutoka Gerezani ndipo walipotoka wanaharakati wa mwanzo waliounda TANU ukimtoa John Rupia. Siku hiyo Gerezani ilikuwa imekuja kumzika shujaa wao. Watu walianza kukusanyika nyumbani kwa mama yake, Abdulwahid Bibi Mluguru bint Mussa mapema asubuhi ambako maiti ilipokuwa imepelekwa. Ilipofika adhuhuri ikawa kama vile Dar es Salaam nzima imekusanywa pale. Chifu wa Unyanyembe Abdallah Said Fundikira, ambae Abdulwahid alisomanae darasa moja katika shule ya serikali mjini Dar es Salam katika miaka ya 1930 na mtu ambae walikwenda wote kuhiji Maka alikuja Dar es Salaam kwa ndege kutokea Nairobi kuja kuhudhuria mazishi.

Inasemekana Nyerere hakutaka kuja kwenye mazishi ya Abdulwahid kwa kuwa wakati ule ndiyo kulikuwa na lile tatizo la EAMWS na masheikh walikuwa wakikamatwa nyakati za usiku na kutupwa jela. Usalama wa Taifa unasemekana ulimshauri Nyerere kwa usalama wake kutohudhuria mazishi yale kwa sababu mazishi ya Abdulwahid yatahudhuriwa na Waislamu wengi. Chuki za Waislamu dhidi ya Nyerere kwa wakati ule zilikuwa juu sana.

Rashid Kawawa aliyekuwa Makamo wa Rais alipopata habari zile kuwa Nyerere hatofika mazishini haraka alimwendea Nyerere na kumwabia kuwa kabla hajachukua uamuzi wa kutokwenda yeye atakwenda kuangalia hali ya mambo yalivyo pale msibani kisha atarudi kumpa habari kamili.

Aliporudi kwa Nyerere Kawawa alimwambia Nyerere kuwa umma uliokuja kumzika Abdulwahid haujapata kuonekana. Chifu Fundikira amekuja kutoka Nairobi kuja kumzika Abdulwahid. Watu wa Dar es Salaam hawatamwelewa kama yeye Nyerere yupo Dar es Salaam na ashindwe kwenda kwenye mazishi yake. Watu wa Dar es Salaam wengi wao wanakumbuka kwa mara ya kwanza kumuona Nyerere akiwa amefuatana na Abdulwahid na wanafahamu hisani aliyomfanyia Nyerere. Nyerere aliona busara ya Kawawa na palepale ikatoka amri kuwa ulinzi katika mazishi ya Abdulwahid uimarishwe na Nyerere atakwenda kumzika rafiki yake aliyempokea na kumuunga mkono wakati ule wa kipindi kigumu cha kuasisi TANU.

Rais Nyerere akawa mmoja wa watu waliokwenda kuomboleza kifo cha Abdulwahid. Akitembea kwa miguu Nyerere alilifuata jeneza la Abdulahid nyuma kutoka Mtaa wa Lindi, Gerezani hadi Msikiti wa Kitumbini maiti ilipokwenda kuswaliwa swala ya jeneza kama ilivyo ada ya Kiislamu.

Pale Kitumbini, Nyerere alisimama nje ya msikiti pamoja na Wakristo na wananchi wengine kungojea maiti ilitolewe nje. Mfanyabiashara mmoja wa Kiasia kuona rais amesimama wima, kwa ajili ya heshima alileta kiti na kumuwekea Nyerere akae. Nyerere alikataa kukaa na akawa amesimama pamoja na watu wengine. Kutoka Kitumbini msafara wa maziko ulielekea makaburi ya Kisutu kwa ajili ya mazishi.

Chifu Fundikira alikuwa mmoja wa watu walioingia kaburini kuupokea mwili wa Abdulwahid. Wakati huu wote wakielekea makaburini, Nyerere alikuwa nyuma ya jeneza kichwa chake amekiinamisha na kila wakati alionekana akifuta macho yake na kitambaa.

Nyerere alikuwa analia. Ilikuwa mwaka 1952 Abdulwahid alipofahamiana na Nyerere na yeye Abdulwahid akamjulisha kwa watu mashuhuri wa Dar es Salaam - Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Mwinjuma Mwinyikambi, Mohamed Jumbe Tambaza, Omar Londo, Rajab Diwani, Mshume Kiyate, Bibi Tatu bint Mzee, Bibi Asha Ngoma, Bibi Titi Mohamed, Bibi Hawa bint Maftah, Bibi Khadija bint Kamba, Said Chamwenyewe na wengi wengine. Ilikuwa na kutokana na msaada wa Abdulwahid na Waislam hawa ndiyo uliomuwezesha Nyerere kuwa katika siasa na kuchukua uongozi wa nchi miaka tisa baadae.

Hakuna aliyeweza kukisia ni mawazo gani yalikuwa yanapita katika fikra za Nyerere. Lakini ni wazi kuwa alikuwa akimfikiria Abdulwahid na jinsi pamoja walivyoweza kuanzisha harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Ilikuwa miaka kumi na tano iliyopita katika Ukumbi wa Arnatouglo, si mbali na pale alipokuwa, Nyerere aligombea urais wa TAA na rais aliyekuwa madarakani, Abdulwahid Sykes. Abdulwahid akiwa na umri wa miaka thelathini na Nyerere akiwa na miaka thelathini na mbili.

Soma zaidi: Alichokifanya Nyerere baada ya Uhuru

Wapinge walawitiwe? hivi hujui jinsi Wazanzibari wanaopinga wanafanywa nini?

Nasikia wanataka wenyewe kulawitiwa. Wakikosa wa kuwalawiti wanakulana wenyewe kwa wenyewe. Kama mijiti iko jirani basi itageuzwa Dhakar
 
FaizaFoxy,

Wewe wafuata maneno ya Mohamed Said, hapa kafika na anajua. Muulize hao alowataja hawakuwa na mpango wa kuipindua nchi kwa udini? na aloitonya serikali ni Sheikh Kassim Bin Juma wakati Nyerere akiwa ktk mkutano Arusha.. Muulize kama yeye ni msema kweli akane maneno haya.
 
Katika mwendelezo wa kupinga mawazo na mfumo wa utawala wa Mwl. Nyerere. Tundu Lissu amepasua jibu ambalo wengi huwa wanaogopa kulipasua pale aliposema kuwa Mwl. Nyerere alikuwa ni "msanii wa kisiasa" kwa sababu aliyokuwa anayasema siyo yale aliyokuwa anayatenda kuhusiana na suala la Muungano. Haya ameyabainisha wakati akitoa hoja kwenye Bunge Maalum.

Mh. Tundu Lissu ameenda mbali na kusema, Mwl. Nyerere alizoea vya halamu na vya halali hakuviweza. Katika kuthibitisha maneno yake, Mh. Tundu Lissu alisema, mwaka 1968, Mwl. Nyerere aliudanganya ulimwengu pale aliposema kupitia gazeti la Observer la UK, “Iwapo umma wa Zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona kuwa Muungano una hasara kwa uhai wao, sitawapiga mabomu kuwalazimisha......Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea iwapo washiriki wake wataamua kutathmini na kuthibitisha jambo hasa tukio la kihistoria kama Muungano'.

Mwaka 1984, Wazinzibari walipohoji Muungano, Alhaji Aboud Jumbe akafukuzwa kazi kwa amri ya Mwl. Nyerere na amewekwa kizuizini Mjimwema mpaka leo. Wolfgang Dourado akawekwa kizuizini, Bashiri Swanzy akapakiwa kwenye ndege ya kwanza akapelekwa Ghana.

Mh. Tundu Lissu aliendelea kusema, kwa vile Mwl. Nyerere alizoea vya kunyonga, kwenye Kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Mwl Nyerere alisema, 'huko nyuma baadhi ya viongozi wapinzani wa Muungano wameishawahi kusema tufanye referendum kwa Zanzibar kuhusu Muungano, tukakataa kwa sababu safi kabisa'.

Tundu Lissu anadai, Mwl. Nyerere hakukataa hoja ya Muungano kwa sababu safi kabisa, bali aliwaweka kizuizini wale waliohoji Muungano. Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uwongo na hakuweza kusema kweli.

Kitu muhimu kabisa cha kujiuliza na kufikiria. Kama kweli Mwl. Nyerere alikuwa anaishi kwa uwongo na udanganyifu, ina maana hata hati ya Muungano haipo na kama haipo, ina maana amewaingizwa 'mkenge' wananchi na hasa wanaCCM kwa kusimamia hoja ambayo kiuhalisia haipo. (Muungano wa serikali mbili).

Tukikubaliana na hoja ya Tundu Lissu, inabidi tujiulize, Kwa nini Baba wa Taifa alikuwa anaishi maisha ya uwongo na udanganyifu?. Alikuwa anafanya hivyo kwa manufaa ya nani?.

Kama hoja ya Tundu Lissu ni kweli basi hatuna budi kusema, kweli uwongo hupanda lifti wakati ukweli hutumia ngazi kuwafikia walengwa!.

Hoja hii inanipeleka kwenye angalizo la sababu ya baadhi ya wajumbe wakiongozwa na Leticia Nyerere kushauri bunge kwa nguvu zote liweke mipaka kwenye kanuni za bunge zikiwataka wabunge kutowadharirisha waasisi wa Muungano. Kumbe nyuma ya hoja zao walikuwa wanaogopa ukweli usijulikane!.

Mpaka katiba mpya ipatikane, tutaona na kusikia mengi!.

Kauli mbiu ni serikali moja au kila nchi ichukue fito zake kwa sababu watu tuliowatuma kwenda kumalizia mchakato wa katiba kwa sasa wanahoji uharali wa Muungano huku wakitaka mpaka makaratasi yenye sahihi za waasisi wa Muungano. Hawa wabunge wameshindwa kufanya kazi ya kumalizia mchakato wa Katiba badala yake wanaanza kuuliza kama Muungano ni halali au batili. Yaani baada ya Miaka karibia 50 ndiyo tunaanza kuuliza Muungano kama ni halali huku waasisi wa Muungano tukiwasema ni waongo na wadanganyifu.

Ninadhani kuna kitu hakiko sawa kwenye baadhi ya hoja za Wabunge!.
[video=youtube_share;bB7BxxMepR8]http://youtu.be/bB7BxxMepR8[/video]
[video=youtube_share;jE7oTPXtpas]http://youtu.be/jE7oTPXtpas[/video]

Nani muongo kati ya Lisu Na Nyerere?
 
Back
Top Bottom