nijothemaster
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 324
- 56
Wanaofikiri Nyerere ni "Mungu Mtu" hawatakuelewa, wanadhani Nyerere hajawahi kufanya makosa.
sio MUNGU lkn uwezo wake ndo phenomena......
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanaofikiri Nyerere ni "Mungu Mtu" hawatakuelewa, wanadhani Nyerere hajawahi kufanya makosa.
Hiki kipindi ni cha muda lakini nilikuwa sijakisikiliza, leo nimekisikiliza na kuanzia saa moja na dakika nane ya video hii Tundu Lissu anafunguka na kusema, "kuna mengi sana mabaya aliyoyafanya Nyerere".
Msikilize Tundu akimwaga radhi kuhusu Nyerere kuanzia saa moja na dakika nane:
[video]https://youtu.be/1m8IRbqFnb0[/video]
Swali langu; Tundu Lissu, Nyerere atakuwaje mtakatifu kama hajafanywa "Mungu Mtu"?
Wacha uongo hakuna mahala Tundu Lissu kasema hayo, Tundu Lissu kasema "mwalim ana mambo mabaya mengi tu..."
Sikiliza, "mabaya" na "si sahihi" kama utakavyo wewe ni vitu tofauti. Kwanini unajaribu kuita ndimu kuwa ni apple? kama ni ndimu ndimu tu.
FaizaFoxy, ije mvua, lije jua, Nyerere atakuwa mtakatifu tu. Naomba Mungu(sio allah) akupe uhai ushuhudie mtakatifu Nyerere atakavyoleta neema Tanzania kila tutakapomuomba Mungu kupitia kwake
Swala la kumuamini au kutokuamini halipo, swala ni kuwa anamponda Nyerere wazi wazi na katika hilo nnakubaliana nae.
Jee, wewe unakubaliana nae, kuwa matatizo ya kiutawala toka mwaka wa 62 mpaka leo hii ni ya Nyerere.
Tundu Lissu anashangaa vipi mpaka Rais wa Zanzibar anaamuliwa Dodoma na tunaitawala Zanzibar kwa mabavu anasema haukubali huu muungano uliopo.
Jamani nyerere twa mupa heshima 1.kwa 7babu ni mwasisi 2. aliongoza jingaz 3 aliongoza watu wachache 4 alikuwa na maamuz
Akili za kushikiwa hizi, halafu mnajiita wasomi. Kama Tundu Lissu akisema sasa inakuwaje? Kwani Tundu Lissu ana uhusiano gani na Mungu ambao binadamu wengine hawana mpaka ajue kuwa Nyerere si Mungu? Ulimsikia wapi Nyerere akisema yeye ni Mungu mtu?
Sasa nimegundua kwanini unamchukia sana huyu mzee wa watu. Sababu kuu itakuwa ulipokwenda Canada na kujifanya mkimbizi wa CUF unakimbia machafuko Zanzibar ili mpewe ukimbizi Nyerere aliwaumbua kuwa nyie ni njaa tu ndiyo inayowakimbiza.
Wewe ulishakwenda Canada ukajifanya mkimbizi sasa ya Tanzania yanakuhusu nini?
Nyinyi wakimbizi mnashida sana.
Mimi au Tundu Lissu? sijatia langu humo.
...nimekuelewa dada. Tunapaswa kumshukuru Mungu kutujalia mtu kama Tundu Lissu.
Lakini Lissu yeye kayasema maCCM yanayotumia jina la baba wa taifa kama hirizi.
Wakati Lissu anasema Baba wa Taifa hakuwa Mungu, Baba wa Taifa mwenyewe wala hakutaka hata kujilinganisha na mwenyezi Mungu. Nakumbuka alipokuwa akihutubia sikukuu ya wafanyakazi pale Mbeya alikiri mwenyewe kuwa wao hawakuwa MALAIKA na kwamba kama binadamu, walifanya pia makosa. Kwa hiyo kumlinganisha na Mungu kunakofanywa na magamba hata baba wa taifa mwenyewe angekuwepo angewakana.
Kwa unavyomchukia Nyerere naona leo roho yako iko kwatu kwa hiyo clip ya Lissu.
Swali kwako sasa dada faiza, hebu nipe maoni yako kwa wafuasi wenzio wa magamba wanaomponda Bw Lissu kwa hiyo kauli yake.
Utakatifu wa kupachikwa na binaadam wala haunistui, hata leo apachikwe lakini ukweli utabaki kuwa ukweli tu.
Mmepachikwa sanamu la mzungu lililoveshwa nepi na mnakubali na mnaliabudu itakuwa nyerere kupachikwa utakatifu? Unanchekesha!
Eti uwe mtakatifu Afrika mpaka ukapewe huo utakatifu Vatikano na wazungu, huo kama si kuwa kikaragosi ch wazungu ni nini? wamekichezea watakavyo wao na sasa wanakupakeni mafuta kwa mgong wa chupa waendelee kuwachezea, na nyie mmo tu mnashangilia.
Mwafrika mwenzake, na aliyekuwepo kwenye utawala wake na yupo kwenye siasa, Tundu Lissu ambae mnaamini ni msomi anasema "matatizo ya kiutawala toka mwaka wa 62 mpaka leo hii ni ya mwalim". Hamkubali. Mnanshangaza sana.
Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Hakuna mahala kaitaja CCM, wacha uongo.
Nilipokwenda Canada, hata CUF ilikuwa haijukani, nimeondoka kwa njaa kweli iliyokuwepo Tanzania, hapo mwalim wako analijuwa hilo na hajakosea.
Hata sukari ilikuwa foleni, kama si njaa nini hicho.
Tundu Lisuu anasema kuwa "matatizo ya kiutawala toka mwaka wa 62 mpaka leo hii ni ya mwalimu".
Hapana. Amesema katiba ya 1962 hadi ya sasa ni ya mwalimu
Hakuna mahala kaitaja CCM, wacha uongo.
Nyerere atafanywa mtakatifu, unabisha??
Akili za kushikiwa hizi, halafu mnajiita wasomi. Kama Tundu Lissu akisema sasa inakuwaje? Kwani Tundu Lissu ana uhusiano gani na Mungu ambao binadamu wengine hawana mpaka ajue kuwa Nyerere si Mungu? Ulimsikia wapi Nyerere akisema yeye ni Mungu mtu?
Sasa nimegundua kwanini unamchukia sana huyu mzee wa watu. Sababu kuu itakuwa ulipokwenda Canada na kujifanya mkimbizi wa CUF unakimbia machafuko Zanzibar ili mpewe ukimbizi Nyerere aliwaumbua kuwa nyie ni njaa tu ndiyo inayowakimbiza.
Wewe ulishakwenda Canada ukajifanya mkimbizi sasa ya Tanzania yanakuhusu nini?
Nyinyi wakimbizi mnashida sana.