Mungu hamtupi mja wake, kwa jinsi ambavyo vichaa wamemdhalilisha baba wa taifa, Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere(R.I.P) kwa kumtukana tena tukiwa hatunaye duniani, hakika SERIKALI tatu hata kama ikitokea miujiza zikawepo lazima Marehemu atapigana kufa na kupona waasisi wake walaaniwe.
Vita hiyo ya baba wa taifa dhidi ya wanaodhani kubaki kwao hapa duniani na yeye kutangulia mbele za haki ni ticketi tosha ya kumdhihaki, kudhihaki muundo wa serikali aliouacha lazima mshindi atakuwa Marehemu tu.
Watu kutoka kona mbalimbali za Tanzania wakiwemo viongozi wa dini, wasomi na makundi mbalimbali waliojitokeza hadharani kulaani dhihaka dhidi ya baba wa Taifa ni majemadari wa vita hiyo wakiongozwa na Marehemu mwenyewe Baba wa taifa.
Tusubiri tu tuone mwisho wa kulalama kwa hawa wanaojiita jeshi la waasi lililosubiri Kamanda Nyerere atoweke duniani ndo wajitokeze kama nyoka alivyojitokeza kule kwenye bustani ya hedeni na kuwadanganya ADAM na HAWA, nyoka huyo akifikiri Mungu hayupo.
Hawa watatambaa na tumbo kama nyoka, ni suala la muda tu.