Wakuu, hotuba ya Kamanda Lissu Bungeni jana nina uthubutu wa kusema, tena kwa ujasiri kwamba tangu Tanganyika huru iwepo hatujawahi kushuhudia hotuba kali kama ile. Ni hotuba ya kisomi iliyojaa kila aina ya vielelezo na ushahidi, zaidi ya vielelezo 70 (footnotes), sio mchezo.
Ili kukata mzizi wa fitna nawaomba advocates wa Serikali 2 waje na ushahidi na vielelezo visivyo na shaka kukanusha paper ya Kamanda Lissu na sio kupayukapayuka bila mpango wala hoja za maana. I can see kwanini jamaa wanang'ang'ania Serikali 2 kwa udi na uvumba lakini bahati mbaya kwao kadiri wanavyozidi uking'ang'anizi wao ndivyo wanavyozidi kuharibu na kuachwa uchi wa nyama.
Poleni watetezi wa Serikali 2 ambao mnadhani mna akili na uzalendo kuliko
Jaji Joseph Warioba, the former Attorney General of the Republic, Prime Minister and VP; kuliko
Dr. Salim A. Salim, the former Minister for Defence, Primer Minister, and OAU Chief; kuliko
Judge Brig. Gen. Augustine Ramadhan, the former high ranking member of the People's Armed Forces, NEC Chair, and the Chief Justice of the Supreme Court of the People of Tanzania; kuliko magwiji wengine lukuki waliokuwa wamejazana kwenye Tume ya Warioba. Jengeni hoja mueleweke kama Kamanda Lissu alivyofanya na sio kupayuka kama wendawazimu.
Nilistuka sana kusikia eti
Nape Nnauye,
W. J. Malecela, na Madabida eti wanazunguka huko na huko "kumjibu" Warioba na timu yake iliyojaa vichwa! Are we serious? Kafulila aliuliza Bungeni, hivi Warioba ni binadamu wa kutukanwa nchi hii? Hata kama alifanya makosa anapaswa kukosolewa kwa staha sio kwa matusi ya dhahiri au ya kificho. Kama kweli ni waungwana, CCM wanapaswa kumwomba msamaha Mzee Warioba na watanzania kwa ujumla.
Nakala:
Pasco,
Chris Lukosi, et. al.