Tundu Lissu, Nchimbi wawapatanisha Mr Sugu na Ruge wa Clouds FM

Tundu Lissu, Nchimbi wawapatanisha Mr Sugu na Ruge wa Clouds FM

Mbona mi siwajui wote hao,huyo Sugu,Ruge na Nchimbi ndio akina nani,mi ndio kwanza nawasikia leo,wamepatanishwa wapi na walikosana nini na lini,pia kwanini???

Punguza kuchaji kobe kijana!
 
WanaJF,
Waziri wa Habari na Utamaduni Emmanuel Nchimbi akishirikiana na mnadhimu mkuu wa upinzani bungeni Tundu Antipass Lissu wamewapatanisha mahasimu wawili Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Ruge Mutahaba.Wamekubaliana kuweka pembeni tofauti zao na kuzizika kabisa kwa maslahi ya wafuasi wao.Ikumbukwe Radio Clods mara kadhaa imekuwa ikilalamikiwa kwa kuchafua baadhi ya vyama vya siasa hususan CDM.


Picha%2Bno.%2B1.jpg
 
Hakuna marefu yasiyo kuwa na mwisho......
na mbio za sakafuni huishi ukingoni.....

Hatimaye hawa mahasimu wame patana leo.
Swali ni je,.....ni upi msingi wa makubaliano yao?
Kwamba Ruge ataachi studio walopewa na raisi?
Au ruge ataacha kuwaibia wasaniii?
Au ulikua ugomvi binafsi na sugu akauchukulia kama vile
ana tetea wasanii wenzake?

Picha%2Bno.%2B1.jpg


Picha%2Bno.%2B2.jpg

Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia) akimsikiliza
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini
Dar es Salaam kuhusiana na mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao
uliotokana na sababu za kimuziki uliodumu kwa muda wa miaka miwili.
Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu

Picha%2Bno.%2B3.jpg

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi akiongea
na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na kumalizika
kwa mgogoro wa miaka miwili uliotokana na sababu za kimuziki baina ya Mbunge wa Mbeya Mjini
Joseph Mbilinyi (Katikati) na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia).

Picha%2Bno.%2B4.jpg

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa
Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakati akiongea na waandishi wa habari
 
Sasa walivyopatana inamaanisha nini?ugomvi ndio umeisha?kwanin sababu zao za ugomvi ni nini,personal issues au mambo ya kupigania haki za wanamuziki wadogo na wale wakubwa wasiojielewa??ebu wekeni kwanza makubaliano yao tuweze kuchambua wamekubaliana nini na nini.Isiwe Sugu kaidiwa nyimbo zake zitagongwa radio ya wafu then roho yake kwatu kabisa.
 
WanaJF,
Waziri wa Habari na Utamaduni Emmanuel Nchimbi akishirikiana na mnadhimu mkuu wa upinzani bungeni Tundu Antipass Lissu wamewapatanisha mahasimu wawili Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Ruge Mutahaba.Wamekubaliana kuweka pembeni tofauti zao na kuzizika kabisa kwa maslahi ya wafuasi wao.Ikumbukwe Radio Clods mara kadhaa imekuwa ikilalamikiwa kwa kuchafua baadhi ya vyama vya siasa hususan CDM.


Picha%2Bno.%2B1.jpg
 
...Kwa hiyo Vinega ndio kwisha kabisa...nadhani ni mwanzo mzuri wa ushirikiano.Ndugu wakipatana wewe shika jembe ukalime.
 
Very good.! PAMOJA NA KUTENDWA KIASI KILE SUGU AMESAMEHE, sugu moto Chini
 
Bifu lao lingekua la kutegeneza hela,these guys culd b billionaires,zaid hata ya hivyo visent vya malaria wanavyo lilia,mwisho wa siku sugu kawauza wenzie wa vinega,ts very sad.
 
Tusubiri songi moja la korabo yao, na mapromo ya kufamtu kule Clouds.
suguruge.jpg
 


tujikumbushe mazee...
 
Last edited by a moderator:
Hakunaga uadui au urafiki wa kudumu, lakini katika muziki bifu linatengeneza soko. Safi sana
 
Nini hatima ya vinega wenzake? Kwyo nyimbo za vinega zitaanza kupigwa wafu fm?
 
Nategemea kauli ya sugu juu ya hili,na je ile movement yao ya vinega mwisho wake ni nini?
 
Nini hatima ya vinega wenzake? Kwyo nyimbo za vinega zitaanza kupigwa wafu fm?

Hili nalo neno,je zile nyimbo za vinega zitapata airtime huko kifo fm?
 
Back
Top Bottom