Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu A.M. Lissu amesema kuwa ana hofu kubwa juu ya mustakabali wa CHADEMA baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika juma lijalo.
Lissu ameyasema hayo katika kipindi cha runinga cha Crown Media kijulikanacho kama Kasri la Kikeke kilichoongozwa na Salim Kikeke. Lissu amesema kuwa kulingana na yanayoendelea kuelekea uchaguzini, mtu yeyote timamu lazima awe na hofu.
Lissu ameongeza kusema kuwa kwasasa CHADEMA imegawanyika katika pande mbili-ya Mbowe na Lissu...mgawanyo unaotishia mustakabali wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Alipoulizwa iwapo atashindwa uchaguzini atafanya nini na kama atahama au la, Lissu amesema akishindwa atakuwa hajawahi kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA na HATAHAMA chama hicho na atabaki kuwa mwanachama wa kawaida wa CHADEMA.
Kuhusu dawa ya kuzuia suitafahamu inayoweza kujitokeza baada ya uchaguzi, Lissu amesema kuwa dawa pekee ni kuwa na uchaguzi mkuu wa CHADEMA huru, wa haki na wa wazi.
Yetu macho na masikio!