Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nitabadili Katiba ili wabunge wawe na maamuzi juu ya fedha za Serikali

Lisu hajawahi kusema ataondoa kodi alisema atabadili sheria ya kodi ili sheria ilenge kwenye haki ya mlipa kodi , Tax payers bill of right ni hilo tu hakusema atafuta kodi.

SERA YA KODI YA CHADEMA HII ,Fungua link hii.

Hicho ndicho alichosema kuhusu suala la kodi, si vizuri hata kidogo kumlisha maneno yako mtu.

Sera ya kodi iko clear kama alivyo isema.

Aidha, kuwapa wabunge kuamua juu ya maendeleo yao ina maana kuwapa wananchi maamuzi juu ya maendeleo yao.

Kila siku unasikia Rais anasema usipo mchagua fulani wa chama fulani sitaleta maendeleo kwenye Jimbo lenu. Ukiliachia bunge liamue hatima ya maendeleo.ya wananchi.itaondoa huu umangi meza wa Rais.

kama wameshindwa kumhoji mbowe amabye sio rais anataka awaaminishe wajinga gani anachokifikiria??

jambo baya sio kutousena ukweli,bali ni kuusema ukweli ambao hauna uhalisia.
 
Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA amesema ni muhimu maamuzi yaweze kuwa ya wananchi na sio kwa Rais kama ilivyo hivi sasa

Amesema kwa sasa mbunge anapaswa kuomba kwa Rais kuhusu miradi mbalimbali na kama Rais atakataa basi hela za miradi hazitoki. Ni vyema kuweka mfumo ambao unaweza kufanya wabunge wakawa na sauti

Amesema masuala yote ya maendeleo yapo mikononi mwa Rais hali inayofanya wabunge wawe omba omba wa kumuomba Rais fedha za miradi mbalimbali

Hivyo amesisitiza kubadili katiba ili bunge liwe na mamlaka ya kuamua mambo ya fedha bila kumuhusisha Rais. Ameyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni Serengeti

Alishachanyikiwa kabisa huyu Lisu
 
Kilichobaki kwa huyu mwamba kutuahidi ni kutufutia dhambi zetu tu!!
Ili mbinguni tuingie wote!!

Kwa ufupi hakuna rais hapa!!
 
NIMELIANGALIA HILI PICHA LA KUTISHA KWA ZAIDI YA SAA MOJA.LISSU NI HABARI NYINGINE, NGOJA NIDUNDULIZE CHENCHI ZANGU ILI NAMI AJAPO HUKU KWETU NIWE NA SADAKA YA KUCHANGIA UHURU HAKI NA MAENDELEO YA WATU,
 
Huyu mtu kweli hana kabisa idea za uchumi! Sasa kazi ya exective ni nini kama bunge litafanya kazi ya executive?

Nchi haiendeshwi kwa mihemuko wala majaribio.

Uchumi wa Lissu hauna financial cinstraint yeye kila kitu kinaweza kufanywa na kama serikali haijafanya basi ni kwa sababu haitaki tu!

Ndio maana yeye kazi yake ni kusema ataondoa kodi huku akihadaa wasiojua kuwa atatoa huduma bora. Nchi zote zenye huduma bora za kijamii wastani wa serikali zao kukusanya kodi kwa uwiano wa GDP ni asilimia 34 Ubelgiji pekee uwiano ni asilimia 48.

Baada ya kushindwa uchaguzi tarehe 28/ Oktoba, aingie darasani asome kidogo uchumi itamsaidia huko mbeleni.

Wewe ni kiazi!! Mfumo uliopo sasa hivi ni serikali kuleta bajeti na Bunge kukubali au kukataa. Baada ya hapo bajeti katika maeneo mengine inatumika 160% na mengine 30% huku Rais akisema hiki kifanyike huku na kile huko. Na bunge lisiweze kuhoji.

Dhana ya Bunge ni kufanya maamuuzi na kisha kuisimamia serikali kutekeleza. Rais ni mkuu wa excutive na nchi lakini abachofanya kinaamriwa na Bunge. Kwa sasa serikali ndio inasimamia Bunge kiuhalisia huku ikiacha the opposite kuwa nadharia tu!!
 
Ndiyo uharo wa chakula gani sasa huu?
 
Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA amesema ni muhimu maamuzi yaweze kuwa ya wananchi na sio kwa Rais kama ilivyo hivi sasa

Amesema kwa sasa mbunge anapaswa kuomba kwa Rais kuhusu miradi mbalimbali na kama Rais atakataa basi hela za miradi hazitoki. Ni vyema kuweka mfumo ambao unaweza kufanya wabunge wakawa na sauti

Amesema masuala yote ya maendeleo yapo mikononi mwa Rais hali inayofanya wabunge wawe omba omba wa kumuomba Rais fedha za miradi mbalimbali

Hivyo amesisitiza kubadili katiba ili bunge liwe na mamlaka ya kuamua mambo ya fedha bila kumuhusisha Rais. Ameyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni Serengeti

Kwa mfano huo serikari gani ilishafanya hayo?
Na kama ndivyo raisi ana haja gani ya kuwapo?
Jevendapo bunge litatoa maamuzi mabaya ya fedha za srikari, nani atawawajibisha?
 
Hii ni nzuri,kumpunguzia mtu mmoja tu kuwa na maamuzi kwenye kila kitu
 
Wewe ni kiazi!! Mfumo uliopo sasa hivi ni serikali kuleta bajeti na Bunge kukubali au kukataa. Baada ya hapo bajeti katika maeneo mengine inatumika 160% na mengine 30% huku Rais akisema hiki kifanyike huku na kile huko. Na bunge lisiweze kuhoji.

Dhana ya Bunge ni kufanya maamuuzi na kisha kuisimamia serikali kutekeleza. Rais ni mkuu wa excutive na nchi lakini abachofanya kinaamriwa na Bunge. Kwa sasa serikali ndio inasimamia Bunge kiuhalisia huku ikiacha the opposite kuwa nadharia tu!!
Wewe ni mbumbumbu wa namna shughuli zinavyoibuliwa hadi hatua ya utekelezaji ndio maaana mnaishia kutukana.

Mradi wowote unaouona unaanzia ndani ya wizara/ idara husika ambapo wataalam huchambua na kuangalia faida na hasara (gharama) na pia kulinganisha na alternative kadhaa za kufanya kitu hicho hicho, pia huangaliwa activities zingine (opportunity cost) ndipo resources hupendekezwa zielekezwe katika activity ipi. Kisha mapendekezo huenda ngazi kwa ngazi hadi baraza la mawaziri. Baada ya hapi kama inahitaji approval ya bunge au kupitisha sheria ili utekelezwe ndipo huenda bungeni nako huanzia kamati ya bunge na kisha bunge zima.

Nyinyi maamuma endeleeni kuamini kila anachosema huyo mungu wenu Lissu, lakini kwa sisi wengine tuliosoma tukaelimika tunachambua mambo critically sio kiushabiki bila kujali kasema nani. Halafu mimi uchumi ni taaluma yangu nina uhakika ninajua kuliko wewe mambo ya uchumi na pia ni mtumishi sio mzururaji kama wewe.
 
Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA amesema ni muhimu maamuzi yaweze kuwa ya wananchi na sio kwa Rais kama ilivyo hivi sasa

Amesema kwa sasa mbunge anapaswa kuomba kwa Rais kuhusu miradi mbalimbali na kama Rais atakataa basi hela za miradi hazitoki. Ni vyema kuweka mfumo ambao unaweza kufanya wabunge wakawa na sauti

Amesema masuala yote ya maendeleo yapo mikononi mwa Rais hali inayofanya wabunge wawe omba omba wa kumuomba Rais fedha za miradi mbalimbali

Hivyo amesisitiza kubadili katiba ili bunge liwe na mamlaka ya kuamua mambo ya fedha bila kumuhusisha Rais. Ameyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni Serengeti

Kwa hiyo ana tamaa ya kuwa na nchi yenye serikali ya wajinga? Duniani aliwahi kuona wapi ujinga wa aina hiyo, au anaanzisha yeye kama sehemu ya ujinga huo? Yaani Bunge lile tunaloliona la kujua kusoma na kuandika, bila hata kuhesabu? Huyu amelewa kelele za jukwaani.
 
Lisu hajawahi kusema ataondoa kodi alisema atabadili sheria ya kodi ili sheria ilenge kwenye haki ya mlipa kodi , Tax payers bill of right ni hilo tu hakusema atafuta kodi.

SERA YA KODI YA CHADEMA HII ,Fungua link hii.

Hicho ndicho alichosema kuhusu suala la kodi, si vizuri hata kidogo kumlisha maneno yako mtu.

Sera ya kodi iko clear kama alivyo isema.

Aidha, kuwapa wabunge kuamua juu ya maendeleo yao ina maana kuwapa wananchi maamuzi juu ya maendeleo yao.

Kila siku unasikia Rais anasema usipo mchagua fulani wa chama fulani sitaleta maendeleo kwenye Jimbo lenu. Ukiliachia bunge liamue hatima ya maendeleo.ya wananchi.itaondoa huu umangi meza wa Rais.

Foolish arguments! Atakuwa rais wa mitandaoni. Serikali ipi duniani inabembeleza mlipa kodi? Ni kama CHADEMA inaendelea kukosa wagombea vile! Lissu hajui hata serikali za dunia zinavyoendeshwa. Anachojua ni maamuzi ya mahakama na ndo maana sera kuu ni kubadili sheria. Ili iweje?
 
Huyu mtu kweli hana kabisa idea za uchumi! Sasa kazi ya exective ni nini kama bunge litafanya kazi ya executive?

Nchi haiendeshwi kwa mihemuko wala majaribio.

Uchumi wa Lissu hauna financial cinstraint yeye kila kitu kinaweza kufanywa na kama serikali haijafanya basi ni kwa sababu haitaki tu!

Ndio maana yeye kazi yake ni kusema ataondoa kodi huku akihadaa wasiojua kuwa atatoa huduma bora. Nchi zote zenye huduma bora za kijamii wastani wa serikali zao kukusanya kodi kwa uwiano wa GDP ni asilimia 34 Ubelgiji pekee uwiano ni asilimia 48.

Baada ya kushindwa uchaguzi tarehe 28/ Oktoba, aingie darasani asome kidogo uchumi itamsaidia huko mbeleni.

Kakojoe ulale
 
.............................
Baada ya kushindwa uchaguzi tarehe 28/ Oktoba, aingie darasani asome kidogo uchumi itamsaidia huko mbeleni.
Hii nimeipenda lakini mtu kama Lissu hata akisoma hawezi kuelewa. Tatizo lake anaamini anajua sana! Ukweli nje ya masomo ya sheria uelewa wake ni mdogo sana na hata hiyo sheria yenyewe yaonekana anageuza mambo, ni Trick-star!
Jana kuna uzi umewekwa ukimuonesha Katambi ambaye alikuwa mwenzake huko CDM, lakini mod ameifuta sijui ni kwa nini! Ni kama kuna kampeni za kumuonesha kwamba anafaa sana!
 
Wewe ni mbumbumbu wa namna shughuli zinavyoibuliwa hadi hatua ya utekelezaji ndio maaana mnaishia kutukana.

Mradi wowote unaouona unaanzia ndani ya wizara/ idara husika ambapo wataalam huchambua na kuangalia faida na hasara (gharama) na pia kulinganisha na alternative kadhaa za kufanya kitu hicho hicho, pia huangaliwa activities zingine (opportunity cost) ndipo resources hupendekezwa zielekezwe katika activity ipi. Kisha mapendekezo huenda ngazi kwa ngazi hadi baraza la mawaziri. Baada ya hapi kama inahitaji approval ya bunge au kupitisha sheria ili utekelezwe ndipo huenda bungeni nako huanzia kamati ya bunge na kisha bunge zima.

Nyinyi maamuma endeleeni kuamini kila anachosema huyo mungu wenu Lissu, lakini kwa sisi wengine tuliosoma tukaelimika tunachambua mambo critically sio kiushabiki bila kujali kasema nani. Halafu mimi uchumi ni taaluma yangu nina uhakika ninajua kuliko wewe mambo ya uchumi na pia ni mtumishi sio mzururaji kama wewe.

Dada RMC, hakuna sehemu yoyote katika uzi wangu nilizungumzia uchumi! Nina mashaka kama wewe ni mchumi, huenda ni mtu uliyesomea uchumi tu. Hiyo haikufanyi kuwa mchumi. Umeshindwa kutambua kuwa mada hapa ni "process flow". Ukisikiliza kampeni za CCM utasikia mbunge wa upinzani akilaumiwa kwa kukosekana kwa barabara, maji nk. Na unachoeleza hapa ni kwanini vitu hivo havitapatikana iwe ni mbunge wa CCM au upinzani kwa sababu ya hiyo "process flow" uliyoieleza (na sijui kama unatambua hilo).

Unajiita umeelimika, I dispute that. Umeenda shule tu na ukatoka na tofauti kidogo sana na ulivoingia (zaidi sana umetoka na umri mkubwa, cheti na kujidai kwingi). Anachosema Lissu (na nikufahamishe mie sio muumini wa vyama vya siasa - i am apolitical) ni kuwa process flows zipelekwe chini kwenye halmashauri ambazo zina madiwani. Watafanya maamuzi locally!! Ungekuwa msomi ungejua kuwa kuna mambo mengine ni ya kitaifa na mengine ni ya kimaeneo. Jambo la kujenga reli, bwawa la umeme, ulinzi, mikopo ya wanafunzi ni ya kitaifa. Swala la kujenga shule, zahanati, madawati, barabara ndogo ni za kimaeneo!! Hayo waachiwe madiwani katika ngazi za halmashauri. Ulichoshindwa kuelewa dada yangu ni hiki - centralization vis-a-vis decentralization!!! Na bado unajiita msomi. Ikiwa hivo, inabaki kuwajibisha madiwani jinsi financial resources zinatumika na hapo ndipo diwani au mbunge anaweza kuulizwa barabara, zahanati, shule na madawayti viko wapi!!!

Ushauri. Jiepushe kujifaya unamfahamu mtu usieyemfahamu. Mimi sio mzururaji kama ulivosema na unaweza kujikuta nakuzidi mbali sana kwa kila jambo. Ni mchumi na umeajiriwa?? My sister, jiajiri na uchumi wako huo na utakuwa a better person financially. Unless ni mchumi wa benki kubwa. Kama umeajiriwa nje ya taaluma yako - wewe sio mchumi, umesomea uchumi tu! Huna experience na chochote kinachoitwa uchumi!! Na ndio maana uelewa wako wa mambo haya ni wa kiwango cha chini. Mada hii ilihusu decision-making!!
 
Magufuli anatumia kodi zetu kujenga miundombinu halafu anataka tumsujudie, what a waste of leadership
Hilo ni bepari lenye kumiliki ranchi kubwa kuliko yoyote Tanzania huku anajiita mtetezi wa walalahoi kweli timefanywa mazuzu
 
Huyu mtu kweli hana kabisa idea za uchumi! Sasa kazi ya exective ni nini kama bunge litafanya kazi ya executive?

Nchi haiendeshwi kwa mihemuko wala majaribio.

Uchumi wa Lissu hauna financial cinstraint yeye kila kitu kinaweza kufanywa na kama serikali haijafanya basi ni kwa sababu haitaki tu!

Ndio maana yeye kazi yake ni kusema ataondoa kodi huku akihadaa wasiojua kuwa atatoa huduma bora. Nchi zote zenye huduma bora za kijamii wastani wa serikali zao kukusanya kodi kwa uwiano wa GDP ni asilimia 34 Ubelgiji pekee uwiano ni asilimia 48.

Baada ya kushindwa uchaguzi tarehe 28/ Oktoba, aingie darasani asome kidogo uchumi itamsaidia huko mbeleni.

Hiyo theory yako ndio mana mpaka leo Tz ipo hapo ilipo, ni theory mgando kabisa watu wanahangaika na mlo 1 wa chakula kwa siku kwa tabu sana, nyinyi ndio mumeaminishwa hivyo hamuna idea nyengine zaidi ya hiyo. sasa kama executive ndio ifanye hiyo kazi mbona sasa toka mpate uhuru umasikini umekubuhu huko Tz?

Mumesema muko uchumi wa kati lakini mbona hali za watu kimaisha zinazidi kudidimia kila uchao? miripuko ya bei za vyakula kila rais mnayemchagua ni afadhali ya yule wa mwanzo? mbona bado kuna matabaka makubwa kati ya walionacho na wasionacho yanazidi kila uchao?

Mwacheni Lissu apambane na hiyo hali abadilishe hiyo mifumo yenu iliyofeli tokea 64.
 
Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA amesema ni muhimu maamuzi yaweze kuwa ya wananchi na sio kwa Rais kama ilivyo hivi sasa

Amesema kwa sasa mbunge anapaswa kuomba kwa Rais kuhusu miradi mbalimbali na kama Rais atakataa basi hela za miradi hazitoki. Ni vyema kuweka mfumo ambao unaweza kufanya wabunge wakawa na sauti

Amesema masuala yote ya maendeleo yapo mikononi mwa Rais hali inayofanya wabunge wawe omba omba wa kumuomba Rais fedha za miradi mbalimbali

Hivyo amesisitiza kubadili katiba ili bunge liwe na mamlaka ya kuamua mambo ya fedha bila kumuhusisha Rais. Ameyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni Serengeti

Ndiyo nchi zilizoendelea wanafanya hivi
 
Back
Top Bottom