Uchaguzi 2020 Tundu Lissu; Nusu Mtu, Nusu Chuma

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu; Nusu Mtu, Nusu Chuma

Malimi Jr

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
1,287
Reaction score
2,743
Takribani miaka 60 sasa Watanzania hususani tabaka tawaliwa, tumeishi kwenye ufukara uliotopea. Wakati huo tabaka tawala wakijineemesha kupitia msamiati uzalendo.

Miaka 60 ya uhuru bado tunapewa ahadi ya jiji la Arusha kuwa kama CALIFORNIA, wakati watoto wetu wanasomea chini ya miti, maajabu haya!!!

Miaka 60 ya uhuru wameshindwa hata kutengeneza mazingira wezeshi ya vijana kuajiriwa na kujiajiri. Halafu mtu mmoja anataka kuibadilisha Tz iwe kama ulaya kwa miaka 5 ijayo. Kama tu sera ya viwanda imemshinda hilo la kuwa kama ataliweza? Lakini nisimlaumu sana make Ulaya yake ipo chattle.

Watanzania sio wajinga tuna jambo letu masaa machache yajayo. Tunaenda kumchagua Tundu Lissu, nusu mtu nusu chuma. Tunahitaji Rais mwenye uthubutu hata tukimtuma kwenda kudai haki kwenye tanuru la moto ataingia na kurudi akiwa hai.

Tundu Lissu atakuwa Rais ambaye ni mfariji, mtenda haki, mpenda maendeleo ya watu na sio vitu, mtoa misaada kwa wahanga wa majanga mbalimbali, hata tukimtuma UN ataenda bila uoga.

Watanzania tumeshaamua kuliondoa jinamizi hili la ufukara (CCM) ambalo kwa miaka 60 limetung'ang'ania. Limefeli sekta zote, UTALII, KILIMO, UVUVI, MISITU, MADINI, NISHATI, MIUNDOMBINU, AFYA, MAJI, kote ni kilio tu.

Masaa machache yajayo Watanzania twendeni, twendeni, twendeni, twendeni tukampigie kura mtu ambaye hata akipigwa risasi 38 anatoka hai. Watanzania tunaenda kuitetea nchi yetu iliyovurugwa kwa miaka 60. Si kazi rahisi ila kwa umoja wetu tutashinda.

@NIYEYE2020. Tarehe 28.10.2020 hatufanyi makosa tunaenda kuchagua nusu chuma, nusu mtu. Ameonesha uthubutu hata kupitia kwenye kampeni zake, ni mtu asiyechoka kutupigania hakika huyu ndiye mbeba maono.

Tukutane Jumatano. Usihangaike kutafuta jina lake ukipewa tu ile karatasi ya kura nenda chini mwishoni utamuona niyeye 2020. weka alama ya vema([emoji818]) kwenye kisanduku kilicho wazi kulia kwake. Usiongeze alama nyingine, kunja karatasi yako kisha kaweke kwenye sanduku lenye mfuniko wa rangi ya bluu.

HAKI, UHURU NA MAENDELEO.
 
Subiri Uchaguzi uishe msaliti wa Nchi atakutana na mkono wa sheria
Kama ni msaliti mpelekeni mahakamani; polisi, jeshi, TISS, DPP, TAKUKURU, Serikali , Bunge, CDF, mahakama vyote vyenu. Mnakwama wapi?
 
Subiri Uchaguzi uishe msaliti wa Nchi atakutana na mkono wa sheria
Rais Uhuru Kenyata wa kenya anehudhuria mara kadhaa kujibu mashtaka huko ICC akiwa tayari ni Rais wa Wakenya. Sasa mnashindwa kumkamata mtu ambaye hana hata cheo cha ubalozi wa nyumba 10 katika nchi hii. Huoni kwamba unachozungumza ni siasa za majitaka
 
Uzuri ni kwamba hata wale wazee wa toka enzi za TANU wameshaelewa na watampa kura Tundu Lissu ila ukiwauliza wapo kimya hawamwambii mtu!
 
Takribani miaka 60 sasa Watanzania hususani tabaka tawaliwa, tumeishi kwenye ufukara uliotopea. Wakati huo tabaka tawala wakijineemesha kupitia msamiati uzalendo...
Haiwezekani niwachague Ccm wakati nimelima korosho vizuri, nimepalilia kwa nguvu zangu nimevuna alafu badae wanatuma jeshi kuja kuninyang’anya na hela hawa ipi, sasa wamefanya wale waliokuwa wafanyabiashara wa korosho hawaji tena kununua korosho na nimekuwa masikini wa kutupwa.

Haiwezekani niwachague Ccm wakati mie ninalima kahawa na hapo uganda tu bei ni shs 2000-3000 alafu Magufuli na Ccm yake wananikataza kuuza kahawa yangu niliyolima kwa jasho uganda na kunilazimisha kuiuza Amicos kwa shs 800-1000

Haiwezekani niwachague Ccm wakati nimelima tumbaku yangu kwa jasho kubwa alafu serikali wananiambia nisiiuze kwa wafanyabiashara wanaonunua kwa bei Nzuri na wanalilazimisha kuiuza kwenye Vyama vya Ushirika kwa bei ndogo inayozidi kunifanya kuwa masikini

Nataka Uhuru na Haki katika kuuza mazao yangu kwa ajiri ya maendeleo yangu na ya familia yangu. Hivyo ndani ya masaa 48 yajayo nitakuwa kituo cha kupigia kura kumchagua Tundu Antiphas Lissu kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania na mbunge na diwani wa Chadema maana wao ndo wana sera ya Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu
 
Haiwezekani niwachague Ccm wakati nimelima korosho vizuri, nimepalilia kwa nguvu zangu nimevuna alafu badae wanatuma jeshi kuja kuninyang’anya na hela hawa ipi, sasa wamefanya wale waliokuwa wafanyabiashara wa korosho hawaji tena kununua korosho na nimekuwa masikini wa kutupwa...
Ndio ninyi mnaofanya Kura za Lisu kufikia 20%

Usipompigia zitapungua zaidi, tafadhari kapige kura
 
Back
Top Bottom