Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli asitufanye wote wajinga, jipya ni kujenga uwanja na mbuga Chato

Nimetafuta sana hiyo hotuba nashukuru nimeipata ni nzuri amejaribu kuelezea vitu vingi kwa muda na kafanikiwa ujumbe uko wazi
Shida moja CDM wajipange kuratibu hizi hotuba zake ziwafikiaje wananchi maana naona tunatumia nguvu kuzipata naona kuna nguvu nyingi zinatumika kuzuia Habari zisisikike
 
Duh!
By paskali
 
Katika Marais wote waliotangulia hakuna Rais aliyemuweka mpwa wake kuwa Paymaster General. Haya ndiyo mapya ya utawala wa awamu ya tano.
Aliyekuwa Governor wa BOT Nyirabu aliteuliwa na Mwl.Nyerere na hiyo benki kuu iliungua akiwa gavana. Sishangai JPM kumteua paymaster general ndio siasa za Tanzania.
 

Maendeleo ya Vitu na Maendeleo ya watu ni vitu tofauti
Kazi nzuri ya kutekeleza miradi aliyobuni Kikwete na akuitafutia pesa
Credits za mradi aliousimamia kwa juhudi zake ni wa Rufiji Huu ni wa zamani Lakini ukiacha Nyerere aliyekaribia kuujenga mwaka 1980 yeye ndie kapambana kutekeleza

Ajifunze kukubali kusifia na wenzake sio kusema huko nyuma hakuna kilichofanyika
 

Kama una nia ya Lissu awe Rais wa Serikali ya awamu ya Sita, wewe na washambiki/wafuasi wake, mpeni/mfikisheni ushauri ufuatao:-
1) Arekebishe lugha anayotumia kuwasilisha hoja zake, kutoka ya matusi na kimahakamahakama na kuwa ya kisiasa.
2) Aheshimu mamlaka, kwa kauli na matendo yake, ili akiingia madarakani naye aheshimiwe.
3) Rais Magufuli amesimamia vizuri utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa chama chake. Yawezekana kuna mapungufu. Haya yabainishwe ni ya Sera (zilivyoainishwa kwenye Ilani) au ya utendaji wake. Kumlawaumu Magufuli, kwa ujumla, ni upofu wa uhalisia ambao unaweza kumgharimu Lissu na kundi lake. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe
4) Serikali ya awamu ya tano imefanya mambo mengi ya maendeleo, katika kipindi kifupi, ikilinganishwa na awamu zilizotangulia. Marais wastaafu na viongozi wengi Afrika na duniani kote, wanakiri hivyo hadharani. Ni kiongozi "mpumbavu" na "lofa" tu ndiye anaweza kusimama hadharani na kukebehi. Lissu akiendekeza lawama na kejeli dhidi ya Magufuli, hakuna shaka wananchi hawatasita kumwajibisha kwa kura.
5) Amekaa nje ya Tanzania kwa kipindi kirefu wakati mengi yamefanyika, hivyo afanye tathmini kabla ya kukurupuka kwa lawama na ahadi ambazo anaamini ni mpya, zitampa kukubalika na wapiga kura wakati hana jinsi ya kuthibitisha utekelezaji wake.
6) Akumbuke M/Kiti wa chama chake anatuhumiwa kufisadi fedha ya chama, ikiwa ni pamoja na ruzuku, kiasi cha kushindwa kujenga ofisi na kuwalipa wafanyakazi haki zao. Je, atawezaje kukabili na kubadili ufisadi huo wa "Boss" wake akiingia Ikulu?
7) Anaamini anapambana na CCM tu, je, amejiandaaje kwa ushindani wa wagombea Urais wa vyama vingine? Hadi sasa hajaonesha nia thabiti ya ushirikiano ikizingatiwa kuwa Uchaguzi Mkuu, 2015 CHADEMA ilivuna ushindi kupitia UKAWA na baadaye kuwatosa washirika wake. USALITI kamwe siyo mtaji katika maisha.
 
Kwa miaka mitano kakopa trilioni ngapi?
Kwa miaka mitano CHADEMA imepokea ruzuku mabilioni mangapi? Wamezifanyia nini cha kuonesha jamii ya walipa kodi? Je, wakipewa nchi wataweza kufanya nini? Toeni boriti kwenye jicho lenu kwanza
 
Hela za kulipa madai ya wafanyakazi hakuna, ila za kujenga uwanja wa ndege Chato zipo!!
Hela za kujenga ofisi za Chama zinatumika kwa ulevi wa kupindukia, nani kati ya viongozi wawili hao wa kuaminika?
 
Hyo makubwa wanayotuaminisha nayo ni yepi ukiachilia Dar,DODOMA NA CHATO wapi kwingine tza wanayo ya kujivunia na utawala huu
 

Hayo maendeleo ya tanzania yalitakiwa yawekwe wapi na wapi yasiwekwe?

Je anapotoka raisi wa nchi hapo hapahitaji maendeleo kwa kuwa sio ndani ya nchi?

Hao watu wa chato huyo tundu lisu hataenda kuwaomba kura?

Je siku akifika hapo chato atawambia wao hawastahili kuwa na kiwanja wala maendeleo kwa sababu sio watanzania?

Je hao watu wa chato hawahitaji kuendelezwa kwa kuwa hawana hadhi?

Je huko kungine palipo na viwanja au vinajengwa wao ni wa maana kuliko chato?

Tundu bado anakwama na atakwama saana
Kama atapenda kutumia maneno ya mashabiki wake kwenye Sera, hatatoboa hata kura laki tano.
 
Population ya kipindi hicho na sasa iko sawa? Mahitaji ya leo na miaka hiyo
Population ya kipindi hicho na sasa iko sawa?
Mahitaji wa kipindi hicho na sasa yapo sawa?
Mlikuwa na shule ngapi kipindi hicho na sasa zipo ngapi? Ili tujue namna ya kufanya licha ya kutolewa elimu tuboreshe zaidi?
Wazazi wako walilipa kodi kuiwezesha serikali kuhudumia wananchi wake kipindi hicho? Au ndio ilitegemea hissani kila kitu kukuhudumia wewe na wenzako?
Watumishi walilipwa mishahara kutoka vyanzo vipi vya mapato? Misaada au kodi ya mtanzania?

Kumbuka taifa linakuwa na mahitaji yanaongezeka na mifumo ya uendeshaji lazima ibadilike baba angu, kukwepa madeni lazima UNYWE MAJI YA KUTOSHA Mzee wangu

Hitimisho JPM ana mapungufu yake kama wengine lakn kafanya KAZI KUBWA SANA kuiweka tanzania ijulikane kimataifa haijalishi kwa mazuri au mabayaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Samahani hivi national park inajengwa asee..... Fanya uchunguz kabla ujaandika basi ile ilikuwa game reserve imepandishwa na kuwa national park tuu.... Kama nyerere national park ilivyotokea under selous game reserve.... Na nyingine nne
 
Unaijua burigi game reserve hiyo ndo imepandishwa hadhi na kuwa burigi national park ubaya uko wapi... Nyingine mbili zipo kagera huko na nyerere national park from selous game reserve..... Kwa. Mbuga ni mpaka wazungu tuu ndo waende kuna watanzania watatembelea na ni uhifadhi pia
 
Ninamkumbuka marehemu mzee kingunge alisema ""huyu alistahili kuwa mnyampala wa Barabara na si vinginevyo"" sasa yametimia.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Mungu amlaze mahala pema, haya maneno kila nikiyaona nachekaga sana.
 
Kwahiyo unaamini bado kuna umasikini nchini??? si mnasema hii nchi tajiri??? sasa hiyo miaka 5 iliyopita mmefanya nini??
 
Hivi yule mume aliyelipa mahali ya jogoo keshahamia chato??!!
 
Kuna wengine uraisi utabakia Kama ndoto kwao, baada ya kuelezea sera zako umekaa kupiga porojo, majungu hayana nafas katika zama hizi, jikite kwenye sera pls otherwise you will loose to the point you can't imagine, hata nafas ya pili unaweza ukaisikia kwenye bomba Kama sera Ndio magufuli, repeating the same issues over time inafika Mahala unachosha hadhira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…