Uchaguzi 2020 Tundu Lissu sio Mzee Lowassa, asipuuzwe!

Andiko zuri sanaa, sioni popote pa kuongezea, muhimu ujumbe ufike kwa wote waliokusudiwa...

#Lissu sio Lowassa.

Lowasa alikiwa ma washabiki na wapiga kura, ila Lisu ana washabiki wapigakura hana.
 
Safi sana, uchambuzi mzuri sana. Umenikumbusha zama za Pascal Mayalla akiwa kwenye form.

Nimependa zaidi kwenye paragraph ya Wanawake, umegonga 100 kwa 100. Mwanamke anapoanza kujitafutia ndio anaelewa mfumo ulivyo, ila akikaa tu nyumbani wakija kumpa kanga na dera la bure basi.
 
Kipindi Lowasa anagombea uchumi wa mtu mmoja mmoja ulikuwa nafuu, hata mimi nilikuwa na akiba kwasasa mmm! ni hataree! yaani hakuna muelekeo
 
Lowassa alikuwa na ushawishi sana ila aligombea akiwa mgonjwa. Pankisonism anayougua inaathiri akili na kumbukumbu. Msikilize hotuba zake kabla hajaugua, utagundua kuwa ni mjenga hoja mzuri.
 


Iko hivyo Mkuu, najua wenye vyama watapata vya kupata, wataacha vya kuachwa
 
"Mimi ningekuwa ndio CCM, ningehakikisha Tundu Lisu hapitishwi na NEC, pengine hiyo ndio ingekuwa Figisu figisu ya kumuondoa Mchezoni, najua sio haki lakini ni bora ningepambana naye kwenye masuala ya NEC, Kuliko kukimbizana naye kwenye kampeni"

Andiko lako ni zuri lakini hapo kwenye kuhakikisha hapitishwi na NEC ....NO!
 
Kipindi Lowasa anagombea uchumi wa mtu mmoja mmoja ulikuwa nafuu, hata mimi nilikuwa na akiba kwasasa mmm ni hataree! yaani hakuna muelekeo


Lowasa hata sasa hana uwezo wa kushawishi, lowasa anabebwa na jina lake. Ila kushawishi mtu kwa maneno hawezi.

Lowasa bila pesa ni kama mbwa asiye na meno
 


Na mimi mwenyewe nimeandika najua sio haki lakini ili nishinde pande zote bara na visiwani lazima mmoja aenguliwe.Vinginevyo lazima mwaka huu upande mmoja utachukuliwa na Upinzani.

Lisu na Maalimu seif wataungana kwenye Kampeni, usijesema. Seif akishinda Lisu atampa nguvu ya kutokukubali kuuza mechi
 
Kwa haraka haraka hiyo ndio njia ya kufanya kwa CCM hii mpya, otherwise kina Kinana na Mzee Makamba warudi kwenye first 11. Ila kwa CCM ya Bashiru Lissu atawasumbua sana na hawana hoja za kumjibu zaidi ya kumwita kibaraka.

NEC isipomlima basi Polisi watakuwa busy sana kwenye hizo siku 60.
 
aisee..

leo hupewi buku 7

utakula hukohuko unakosifia
 
MBONA TAYARI WAMESHAMTUMIA MEMBE KUPUNGUZA NGUVU ZA UPINZANI kwa kugawa kura zao. Mtu wa kitengo usimuamini hata siku mwenga
 
Kwaninj aenguliwe nec nasisi tumejenga reli madaraja tumenunua meli muachenj mushindane kwa hoja ktk ulingo wa siasa mulijidai mukasema hakuna mtu wowote duniani kama magufuli sasa tunataka hoja hakuna point 3 mezani nakama mwataka kuchafua amani ya nchi hii mkateni lisu bora mumshinde ktk sanduku la kura kuliko kumkata NEC mumeshindwa kumuua sasa mwataka kumzulumu kwenye kupitishwa kugombea
 


Duuh! Mkuu mimi nimesema. kama ningekuwa CCM(Kumaanisha sio) ningefanya figisu figisu Lisu aenguliwe na NEC.

Mimi sina Chama, sinufaiki na chama chochote. Naangalia maslahi ya nchi hilo tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…