Uchaguzi 2020 Tundu Lissu sio Mzee Lowassa, asipuuzwe!



Mbona hujasema ajira kwa vijana,
mbona hujasema wafanyakazi kutokuongezewa mishahara
Mbona hujasema uminywaji wa uhuru wa vyombo vya habari
Mbona hujasema Ukandamizaji wa vyama vingine vya siasa
Mbona hujasema ishu ya utekaji na mauaji
Mbona hujasema ishu ya pesa kutumika bila kuidhinishwa na Bunge Miongoni mwa mambo mengine

Hizo kwako sio hoja?

Zingatia; Lisu kama ataponda mambo ya JPM bila sababu za msingi basi naye ni zwazwa.

Anachokisema Lisu ni kuwa hata kama unaleta maendeleo isiwe kigezo cha kukanyaga uhuru wa unaowapa maendeleo.

Sasa wapi hujaelewa?

Ugomvi wangu na Lisu ni kushindwa kuwakemea wazungu, kuwakosoa kwa unyonyaji wao. Huo ndio ugomvi wangu na Lisu.

Na kama hatawakemea majibu atayapata hiyo october 28.

Sipo hapa kutetea chama chako boss au chama cha upinzani.
 

Great analysis

Advantage kubwa ya Magufuli mwaka 2015 ilikuwa ni kwenye kutoa ahadi kuwa nitafanya hiki, nitafanya kile na kwa kuwa alikuwa amejijengea reputation ya kusimamia mabarabara vizuri kuna watu walimuamini wakampigia kura kwa hilo. Safari hii hawezi kuja na ahadi zilezile ambazo ameshindwa kuzitimiza, na hata akiahidi nyingine watu watamwambia wewe ni msanii!

Magufuli kwenye uchaguzi huu atakuwa na hali mbaya sana!
 
Sio kulazimisha attention?

Unatukana... unamwambia mtu ntakupiga a aendelea na zake.

Sasa tunakuja na hoja ... usimpuuzie...

Tyson asumpuuzie Matumula... good point[emoji3]

Huwezi ukaelewa,

ukiona mtu kakukunjia ngumi, hata kama ni mfupi, hana nguvu, kakondeana, chunga sana.

Hupaswi kumpuuza.

Huwezi nielewa kama hujielewi
 
Chorus "tumeibiwa kura"...[emoji3]
Lisu akishinda nakuhakikishia atatangazwa.
Lisu ni zaidi ya unavyomuona, ni jasiri kuliko unavyomuona.

Nimetoa ushauri hapo, ningekuwa mimi ningemuengua hapo NEC kwa figisu figisu.

Siku 60 ni nyingi sana,
 
Hule ni mtego wametegwa NEC pale mmoja akienguliwa snasimamiswa mmoja wakipita wote membe anamuachia lisu aendelee na gurudumu
hata wasipokatwa, Membe akijitoa hatakatwa jina litaletwa kama lilivyo na hatajitoa mana hakutumwa kufanya hivyo.
 
Nimependa ujumbe wako mzr ila nakuomba ungewafikishia na hao wanaccm wasiokua na mitandao ya kijamii
 


Nimetoa sababu zaidi ya sita.

Moja ya mambo nisiyoweza kuhangaika nayo ni kubishana na mtu ambaye akili yake ipo chini ya ushabiki.

Wewe kama hujaelewa, wakubwa wako wameelewa. Hata hivyo hakuna hoja inayokuhusu
 
Hivi nikuulize swali dogo tu, kati ya Gaddafi na Magufuli ni nani kawafanyia makubwa watu wake?

Swali la nyongeza maendeleo makubwa yaliyopo South Africa yameletwa na nani? Au chama gani?

Ukiweza kujibu haya ni kipimo tosha cha upeo wa akili yako na ndio utajuwa binadamu wanahitaji nini.
 
Very interesting, yani uwakemee wazungu halafu uende kuwaomba misaada?

Bajeti ya Tanzania 40% inawategemea hao "Mabeberu" waichangie then unapata wapi moral authority ya kuwagombeza?

Hivi wewe hata huko mtaani mtu anayekununulia bia kila siku una jeuri ya kumgombeza?
 
Umechambua vizuri sana.ila pale uliposema magufuli Ni mzuri wa kujenga hoja kwamba ukimpa masaa matatu ungetamani aendelee??? Hahahahahah serious?labda Mimi sijui maana ya kujenga hoja.magufuli na hoja?mhhh Hongera lkn nimefurahi kusoma
 
Japo hatukuzidi wewe matatizo. Kama hamumuogopi mbona mna panic sana.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Don't wake them up. They are in a sleeping session. They are relaxing. Waiting for favors from the electoral commission, the police force, intelligence unit, and the judiciary at a bitter end.
 
Umeitendea haki "home of great thinkers". You make jamiiforums alive. Hongera sana
 
Leta hoja, watu wanabishana kwa hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…