Pre GE2025 Tundu Lissu: Siwezi kutoboa kuanzisha chama kipya, hawataninikubalia kukisajili

Pre GE2025 Tundu Lissu: Siwezi kutoboa kuanzisha chama kipya, hawataninikubalia kukisajili

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Tundu Lissu ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya uenyekiti katika chama hicho amesema hawezi kutoboa kuanzisha chama kipya kwa sababu wahusika wa usajili wa vyama vya siasa nchini hawawezi kukubali kutokana na kile kinachodaiwa kuwa Lissu ni mgumu na mkweli kupitiliza.

Lissu ameyazungumza hayo katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds TV ambapo mahojiano hayo yamefanyikia nyumbani kwake Tegeta jijini Dar es Salaam.

Soma pia: Tundu Lisu: Hata nikitaka kuanzisha Chama kipya Jaji Mutungi hatakisajili kwa sababu anafahamu mimi ni mpinzani wa kweli!
 
Kwa hiyo Ana Nia Hiyo Ila Anaogopa!

Tumnyime Kura!
 
Lissu tukushauri kaa chini na Mh. Mbowe Mwenyekiti wako myamalize vinginevyo hupewi chama..idadi ya kura haitafikia.
 
Bongo msema kweli anaonekana tishio na kuogopwa
CCM wametuharibia sana hili taifa. Eti watu wakweli na walionyoka ndo wanaonekana hawafai

Alafu tunauliza nani aliyeturoga???

Inaelekea hata Mungu huwa anatushangaa tukiliombea Taifa
 
Lissu tukushauri kaa chini na Mh. Mbowe Mwenyekiti wako myamalize vinginevyo hupewi chama..idadi ya kura haitafikia.
Kaa kwa kutulia najiandae tu! Lissu ndo anayeenda kuongoza siasa za kupata Katiba Mpya kama Mwenyekiti wa Chadema kuanzia January 2025
 
Mungu hawezi kukuokoa na kifo cha kikatili ukapona risasi 16, ili uwe mwanachama wa kawaida wa CHADEMA basi na uishi maisha simple tu na uendelee kukaa na mkeo na watoto wako nyumbani
 
Back
Top Bottom