Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Tanzania haiwezi kuishi bila dunia ila dunia inaweza kuishi bila Tanzania

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Tanzania haiwezi kuishi bila dunia ila dunia inaweza kuishi bila Tanzania

Kwahiyo huoni Korea kaskazini kushirikiana na Urusi na Uchina ndiyo inathibitisha point ya TAL

Kwani ushirikiano ni nini mleta hoja?

Mujombha Elitwege una lipi la kusema kuhusu hili
Kwani yeye anavosema magufuli kaitenga tanzania na marafiki wetu wa ulaya na marekani ni kwamba hatuna nchi tunazoshirikiana nazo ? Rafiki siyo lazima awe marekani, uwingereza au ujerumani, tunaweza hata kushirikiana nchi za afrika kwa afrika na tukasonga mbele nnavyoamini mimi
 
Watz na ccm yenu mnashindwa kutengeneza hata toothpick tu halafu mnajilinganisha na North Korea. Pumbavuuu
[emoji23][emoji23][emoji23] kama unadhani hii nchi inaharibiwa na CCM basi umechelewa mno broo....you must think Critically
 
Issue ni kuwa Mao na Lenin kuweka closed economy ndio kulichochea kugundua

Wangejali hao wapinzani china na Russia isingekuwa ilipo kuwa tishio kwa Marekani na Ulaya sasa .Kujenga nchi namba one task ni ku deal na vibaraka wapinga step forward ndicho Mao na Lenin walifanya na ndicho Tanzania kinatakiwa kufanywa wawe ndani ya COM au nje
Wewe ni moron kabisa Tena slug head! All years in power as CCM mlikuwa wapi kufanya hayo? Unakuja na porojo za juma na uledi hapa yaani toka muanze kuweka viongozi wenu madarakani mnakuja na uongo mpya ! Now we are tired
 
Usidhani wote mburula humu! Corona tumeishinda kwa kuwa hatupimi tungeendelea kupima ungeona maajabu!! Kwanza naamini ni immunity zetu tu!!
Hatupimi? Tumepima mpaka mapapai mkuu, tukagundua janja janja zilizopo kwenye hii corona, hao wanaopima pima mbona kila siku wanahaha... wakat bongo daladala zinajaza kama kawa sasaiv tena without masks na maisha yanaenda kama kawa. Funguka duniani maigizo mengi
 
Kuna mtu anataka kuishi bila majirani..kwamba yeye na familia yake ati wanajiweza...wakati 80% ya wanafamilia hao wanakula nusu mlo kwa siku, yaani kipato cha kaya dola 2 hadi 3 kwa siku.
Unamzungumzia Magufuli ?
 
Mkuu, huwezi kufananisha Tanzania na hayo mataifa kama N.Korea na Cuba au Iran, hizo ni nchi zilizo katika ulimwengu wa kwanza(nchi zilizoendelea toka kitambo) ndo maana wana uwezo wa kusavaivo bila shida.
Sawa Tanzania hii kinchi masikini kama hiki tumekaa tunafarijiana kuwa Tupo uchumi wa kati hali ya kuwa raia wengi tuko hoi kimaisha.
Binafsi nayakubali kimtindo haya maneno ya Lissu kwani sisi bado hatujiwezi na kiburi hicho kwa mataifa makubwa hatuna.

Just emagine, taifa dogo lingeweza kuwa na migogoro na USA..? Naamini USA awezi kufanya battling na taifa lolote la kimasikini ambalo limeizidi kila kitu, So ukiona N.Korea, Iran sijui Cuba wanaweza kufanya battling na Marekana basi fahamu nao si haba(wameadvance)
Hoja yako ni msingi mkuu....ila mimi ninachopinga kwa lisu, si kweli kwamba Tanzania imejitenga na Marafiki iliyokuwa nayo....alichofanya magufuli ni kujitenga na marafiki ambao walikuwa ni wanyonyaji na wala si kweli kuwa mpaka sasa tumebaki bila rafiki....mfano : Tangu mwaka 1999 tumekuwa tukiibiwa dhahabu, tukidanganywa kwamba ni mchanga unaenda kuchenjuliwa nje ya nchi sijui japan,,, alivoingia magu akapiga marufuku wachenhjulie hapa hapa....kama hawataki wasepe wakate tu na uhusiano kama wanataka maana huu ni urafiki wa kijambazi kabisa , nafikir umenielewa aina ya urafiki ninaoumaanisha
 
NDUGU HUU UCHUMI WA MAO Ulipingwa sana China na watu kama Deng Xping,, waliamini kabisa kwamba Mao alifanya makosa makubwa kuifunga China na Dunia,,. dENG xPING ALIWEKWA KIZUIZINI na Mao kwa zaidi za ya miaka 8. Baadaye baaada ya Kufariki Mao, Deng XPING Alikuja transform huo mfumo kwa kuingiza chembe chembe nyingi za kibepari.
Na hata sasa Cuba nao wanafanya haya haya.

Hat NORTH KOREA wapo taabani kabisa ukifananisha na wenzao wa South Korea,, hata East Germany ambayo pia ilikuwa na sera hizo za closed economy hali yao ilikuwa Mbaya ukifananisha na West Germany kabla ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlin na kwa kweli CHINA wanamshukulu sana kiongozi wao DENG XPING aliyebadilisha mambo,, kwa kuiingiza sera za ubepari ambazo Mao Hakutaka hata kusikia. Na ndio maana taifa likapiga hatua kubwa sana

Na RUSSIA hii ya PUTIN siyo Russia ya Lenin, wala Stalin ,,kwa sasa wameingiza sana sera na mtazamo wa kipebari kwenye uchumi wao na waliachana kabisa na sera za closed economy.

KWAIYO NI SAHIHI KWAMBA DUNIA INAWEZEKANA BILA TANZANIA, LAKINI TANZANIA HAIWEZEKANI BILA DUNIA,,.
Closed economy = command economy ?
 
Aiseee Ujamaa ulianguka miaka mingi iliopita.Dunia sasa ni ya Kibepari, hata hao wachina, warusi ni wabepari wenye ujamaa kiasi.


Itoshe kusema ivi..sio tu Tanzania, Bali Afrika nzima inategemea Dunia ili iishi..

Kusema ukweli, Dunia haitegemei Waafrika .


Wee fikiria, Kama Uchina na Urusi saizi wanalia lia sababu Dunia imewakamata.... Sembuse Tanzani????



LISSU YUKO SAHIHI.... ALIJIFANYA MUGABE, NCHI ALIIFIKISHA WAPI???
Dunia inategemea rasilimali zilizojaa Afrika, ova
 
Tundu Lisu re uchumi
Uchumi uko wa aina mbili open economy ambayo nchi haiwezi ishi bila kutegemea nchi ingine

Aina ya pili ya uchumi ni closed economy ambapo nchi hukataa kuishi kwa kutegemea nchi nyingine kabisa
Nchi zote zilizoendelea zilianza na closed economy mfano China mwaka 1949 Mao tse Tung alitangaza mapinduzi ya kiutamaduni alifunga mipaka yote akasema kila kitu kinachohitajika china wachina wenyewe wagundue vingine wafe hakuna kuna ku mport wala kuexport chochote China iwe elimu au bidhaa au huduma

Wachina wakaingia kazini kugundua vitu kibao kuanzia dawa za kichina nk Baadaye uchumi wa china ukafunguliwa yeye ndio biggest exporter wa Bidhaa world wide anakopesha hadi marekani

Magufuli kuna vitu kufanya ni close economy ili ku save pesa za kigeni ili kujenga Maendeleo ya ndani badala ya hizo pesa kupelekwa nje kwa kisingizio cha semina,warsha na safari za Raisi na ujumbe wake ulaya na marekani
Mkuu hapa nimekuelewa vizuri mno, big up for that, hasa pale kwenye kuihusu china yani ni mbinu nzuri mno ya kuendelea na nafikiri ndo vision ya magufuli ,[emoji123]
 
Dogo we mbona bado unakaa kwa shemeji yako. Akili zako umeziazima wapi?
Una akili za kijinga mkuu kubali tu hilo!

Hivi kwa akili hizi za Lisu tuatanza lini kujitegemea?
 
Wakuu habarini za jioni,

Natumai mko salama na mnaendelea na majukumu yenu.

Nimeona niulete huu uzi wa mheshemiwa Tundu Lisu hapa tuujadili ili tuone kama kweli hoja hii ina mashiko . Nimemsikiliza huu mheshimiwa (Tundu Lisu) akiwa Shinyanga anasema kuwa Tanzania haiwezi kuishi bila Dunia ila Dunia inaweza kuishi bila Tanzania, na akasema akishinda uraisi basi atahakikisha anarudisha mahusiano mema ya Tanzania na nchi za magharabi ambazo Magufuli anaonekan a kujitenga nazo.

Je ni kweli kuwa Tanzania haiwezi kuendelea bila mahusiano mema na nchi za kibepari ? Kama ni kweli Je vipi kuhusu nchi kama Korea Kaskazini na Cuba ambazo ni kama zimetengwa na ulimwengu hasa mataifa makubwa lakini mbona wanaishi ?

Ukiangalia korea kaskazini ina uhusiano na China na Urusi pekee lakini Je mbona wanaendelea kusonga mbele na wameweza hadi kutengeza silaha za Nuclear kuwatisha hadi wamarekani, nawasilisha
Kwanza kabisa, serikali ya Magufuli haijajitenga na nchi za magharibi - hivyo kujadili huu uzi ni basi tu! Maana Lissu anaongopa kuhusu jambo hilo. Juzi juzi balozi wa marekani amewasilisha vitambulisho vyake kwa JPM. Pia nchi nyingi za EU zina wawakilishi wao hapa nchini.
Usilinganishe Korea/Cuba na Tanzania. Alichofanya JPM ni kutojipendekeza kwa wazungu kama viongozi wengi wa Afrika wanavyofanya. Lissu akipewa uraisi ataturudisha nyuma enzi za Mobutu na maraisi wengi wa nchi za Francophone.
 
Hizi akili ndio wakikuwa nazo kina Lisu kipindi hicho cha corona kwamba bila wazungu tz tutaangamia wote.
 
Kuna mtu anataka kuishi bila majirani..kwamba yeye na familia yake ati wanajiweza...wakati 80% ya wanafamilia hao wanakula nusu mlo kwa siku, yaani kipato cha kaya dola 2 hadi 3 kwa siku.
Hakuna mtu anaeweza kuishi bila majiran ila kuna majirani wa kuchagua siyo kila jirani mwema kwako, nafikiri umenielewa [emoji41][emoji41][emoji41]
 
Corona tuliishinda bila kutegemea taifa lolote duniani liwe la ulaya ubelgiji marekani au Kenya ambayo kutwa Chadema hukusifia kuwa kuko vizuri kwa matibabu

Lisu mwongo Ushahidu ni ushindi wetu dhidi ya corona kuwa taifa likiamua laweza survive bila msaada wa nchi yoyote
Well Said, na mpaka leo bado hawaamini kuwa hakuna korona TZ
 
Back
Top Bottom