Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unataka kutuaminisha kuwa Ikulu imegeuka mgahawa?.
Hahahaaaaa mkuu, umenikumbusha ya uzinifu wa Dr Slaa. Yaani kwa tafsiri yako ni kuwa chadema wote ni wazinzi kwa vile katibu mkuu wao ni mzinifu na mwenyekiti amesababisha mimba isiyokusudiwa na mtoto wa haramu.Ukiona mtoto anakuwa muongo, mwizi wa mboga, halafu maneno mengi jua ukubwani atakuwa kada wa ccm, usimtie moyo piga sana, charaza viboko.. Na chukua hatua mapema ....... !
Hahahaaaaa mkuu, umenikumbusha ya uzinifu wa Dr Slaa. Yaani kwa tafsiri yako ni kuwa chadema wote ni wazinzi kwa vile katibu mkuu wao ni mzinifu na mwenyekiti amesababisha mimba isiyokusudiwa na mtoto wa haramu.
Inaelekea unawaza tumbo sana!. Kama Chabruma ni wa kike sawa. Samahani lakini.
"Chadema bado siyo imara"
By Dr. Slaa
Wapinzani tunaitaji wawepo lakini kwa maneno ya kina LISU watapeleka nchi siko ccm sikivu sana na tunataka aman
mKUU, alichozungumza Lisu kwa maneno ya Mbowe ni msimamo wa kambi ya upinzani. kutokana na hali hiyo, huwezi kusema kuwa huo ni msimamo wa umma. chadema hawawezi kuwasemea watanzania kwani kila mtu ana utashi wa kufikiri na kutambua. tatizo kubwa chadema wamelifanya suala la katiba kuwa ni suala la kisiasa
Ok japo sikuona mantiki ya kuwakrimu wageni katika mjadala huu, woote wanachangia hapa ni juu ya rais J. Kikwete kuwaita wapinzani ikulu kuwasikiliza kama wawakilishi wa wananchi.Mkuu Kyaiyembe, mie nimeandika juu ya umuhimu wa kuwakirimu wageni wanapokuja kwako. hayo nilikuwa najibu hoja ya Ikulu kuwa mgahawa. kama kwenu hamkarimu wageni hilo sikulazimishi na wala halina uhusiano na jinsia ya mtu
Sikubaliani kabisa na maneno ya MBOWE kuwa, Rais JAKAYA KIKWETE kumshambulia TUNDU LISSU wakati wa hotuba yake kuwa alimuonea kwa madai kuwa maneno ya LISSU hayakuwa yake bali ni ya kambi rasmi ya upinzani.
Nadiriki kusema kuwa wanachokifanya hivi sasa CHADEMA ni kujaribu kumusafisha LISSU na tabia yake ya siku nyingi kutoa maneno ya kizushi, dhihaka kwa serikali na mbwebwe nyingine nyingi ambazo kwa uhakika wanaolitakia amani taifa letu, ndani ya Bunge(wale wa chama tawala na upinzani), nje ya bunge, wasomi na hata wananchi wa kawaida walishaanza kuingiwa wasiwasi na utimamu wa akili ya Mbunge huyu.
Siku chache zilizopita , LISSU amepambwa sana kwenye vyombo vya habari, wapambe wake, kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni mtu tishio, lakini hakuna aliyesimama na kusema siyo yeye aliye tishio bali ni chama kwa ujumla, ila leo ambapo Rais ameonesha kukerwa na pengine sasa kama mkuu wa nchi anaona anakoelekea LISSU ni hatari kwa amani ya nchi yetu ndipo wanaibuka akina MBOWE na kusema kuwa yale yalikuwa maneno ya Kambi ya Upinzani na kwamba Rais hajamtendea haki na kwamba amuombe msamaha, kwa lipi mpaka rais amuombe msamaha LISSU kama siyo kumkosea adabu mheshimiwa Rais na kuendelea kulea ugonjwa kwa vile LISSU ataona kama amepewa go ahead na mkubwa wake kuendelea kusema hovyo.
MBOWE anasemaje Rais amuombe radhi LISSU wakati huo wanampongeza kwa hotuba yake huku wakisema amewaaibisha wana CCM ambao walionekana kuunanga muungano wao vyama vitatu, muungano ambao kimsingi umekosa mashiko hasa baada ya hotuba ya Rais JAKAYA KIKWETE. Wanamtaka Rais awaite kwenda ikulu kufanya nini kama kweli wanaona LISSU ameonewa?
Ni bora Dr Slaa awe raisi kuliko Tundu Lisu kuingia bungeni----JK, 2010