Uchaguzi 2020 Tundu Lissu usihame kwenye ajenda muhimu

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu usihame kwenye ajenda muhimu

jumamasy

Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
30
Reaction score
39
Kabla hujaanza kampeni, nchi ilikuwa imekata tamaa. Watu walikuwa wamekata tamaa wakijiuliza ni lini ukombozi wao utakuja. Nchi ilikuwa kilio kila mahali si wa CCM, CHADEMA, CUF wala ACT.

Ugumu wa maisha, pamoja na maendeleo yaliyoyaliyofanyika kwa awamu hii bado ukweli uko wazi, ni maendeleo yaliyoacha maumivu makubwa kwa watu. Wote tumeumizwa na maendeleo hayo sI wakulima, wafanyakazi sekta zote, wafugaji na wafanyabiasha.

Tulikuelewa sana ulipokuwa ukinadi sera zako na ndiyo maana umejikusanyia wafuasi kila mahali. Usiingie KWENYE Mtego wao ukaanza kushughulika nao kwani watakuhamisha KWENYE AJENDA ambazo wananchi sisi umetuvutia maana hatukuwa na mahali pa kuondoa maumivu hayo.

Endelea ukinadi sera zako na kusemea haya yanayochukiza;
1. Uminywaji wa uhuru, wa kusema, kukosoa, hasa kwa vyombo vya habari. Magazeti hayauziki tena.

2. Ukandamizaji wa demokrasia, hasa vyama vya Siasa. Mf kuenguliwa wagombea, Katambi vs Masele.

3. Mauaji eg Kibiti, Akwilina, Mawazo na wengineo. Utekwaji mf. Nape, MO, Clouds na kubambikiwa kesi za Jinai na Uraia ni mambo yaliyoumiza Jamii sana.

4. Kuminywa kwa maslahi ya wafanyakazi, wakulima na ukandamizwaji wa wafanyabiashara.

5. Kuvamiwa kwa uhuru wa Bunge la Jamhuri. Imefikia mahali watu tunawaza kuna haja gani kuchagua waBunge wa CCM?

6. Sheria zilizoingizwa KWENYE Bima ya afya,Bodi ya mikopo n.k ni bomu kubwa kwa CCM.

7. Mikataba tata kwenye manunuzi na miradi mikubwa ya Serikali.

8. Ahadi ya Mil 50 kila kijiji na Laptop na mishahara minono kwa walimu

9. Uhusiano wa nchi kimataifa.

10. Wasomi maelfu wanamaliza vyuo au Sekondari Ajiara hakuna.

11. Utatuzi wa tatizo la ajira kwa kujenga viwanda kila mahali n.k. Tulishia kuahidiwa tu.

Naweza andika mengi sana Ila hizi ni kero kubwa Raia tunataka kuendelea kusikia kwako. Hayo yanayoendelea ni mbinu na mkakati wa kisiasa.

Kumbuka Mapolisi na wana CCM pia ni wapiga kura wako wazuri wakiwemo akina Makamba, Ngeleja na wengineo maana kura ni siri. Wakikushambulia kwa maneno usiwajibu kwa jazba.

MAENDELEO HAYANA VYAMA.
 
Back
Top Bottom