Pre GE2025 Tundu Lissu: Viongozi wa dini msiwaombee wezi wa uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu amesema kuwa katika kutimiza ajenda ya "No Reform No Election' chama hicho kimelenga kuwajumuisha viongozi wa dini ili nao wawe sehemu ya mabadiliko ya kisiasa nchini ikiwamo mfumo wa uchaguzi.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Lissu amesema hayo alipokuwa jimbo la Kibamba Februari 21, 2025 katika kikao cha ndani.

"Mnaambiwa msishiriki kwenye mambo ya siasa, wakiiba uchaguzi wanawaita kwenda kuwaapisha, wanawaita kwenda kuwaombea ili muwape upako kwa wizi wao", amesema Lissu.

Soma, Pia
 
kwamba kibaka na tapeli wa kisiasa ndio anawafundisha kazi maaskofu, kweli?

labda aache kuomba omba kuchangiwa pesa na afanye kazi na kujitegemea kiuchumi :pedroP:
 
Hili ni kati ya mambo Muhimu sana
Lisu akili hazimo kwa hiyo wamuombee yeye ambaye alimdhalilisha Mbowe Mwenyekiti wake bila ushahidi wowote kuwa mwizi na kapokea hela za Abdul mzee wa watu

Halafu viongozi wa dini waliopokea hela ya sadaka kutoka kwa Raisi kujenga majengo ya dini anawaita wamepokea rushwa kwa Raisi utafikiri hizo pesa ziliingia mifuko binafsi na akaunti binafsi za Mufti na maaskofu katoliki,Lutheran, Pentecoste nk

Toka siasa za vyama vya siasa zianze Tanzania toka hata kipindi cha chama kimoja nchi haijawahi pata mwanasiasa yeyote mdhalilishaji viongozi wa dini openly kama Tundu Lisu

Kiongozi wa dini yeyote akiitisha mchango wa jengo kutoka kwa yeyote mwenye mapenzi mema na huo mradi Raisi akitoa ooh huyo kiongozi wa dini kalamba asali za pesa za Abdul wakati hata yeye ilikuwa ruksa kuchangia

Nasema Lisu mwehu na mbinafsi mno mfano alipochangisha pesa yake binafsi kununua gari yake CCM waliposema tutakuchangia alikubali haraka kuwa anapokea mchango kutoka kwa yeyote mwenye mapenzi mema na yeye apate gari CCM kweli wakampa hela milioni tano na ushee hakusema cha ohh hizi hela za Abdul sitaki mnilambishe asali kama mlivyolambisha viongozi wa dini alizipokea a

Viongozi wa dini wamuombee yeye kwa lipi ? Kwa matusi aliyowaporomoshea kuwa wamelamba asali kula pesa za Abdul kuchangia michango ya project za makanisa na misikiti yao?

Watamuombea maombi yapi kwa mfano?
 
Viongozi wa Dini wawe upande wa Wananchi.
 
Waiombee jamii yetu ya kanyaga twende, mafuvu yao yarudishiwa akili, jamii ambayo haiwezi kuchakata fikra chanya na hasi pia unaweza kuisafisha ubongo ikafikiri unavyotaka wewe

Jamii ambayo wanaopewa dhamana huahirisha kufikiri Kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga wa kuigiza kwa viongozi wao, (unafiki), a.k.a kujizima data, tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo, (uchawa)
 
Hili ni kati ya mambo Muhimu sana
Lisu akili hazimo kwa hiyo wamuombee yeye ambaye alimdhalilisha Mbowe Mwenyekiti wake bila ushahidi wowote kuwa mwizi na kapokea hela za Abdul mzee wa watu

Halafu viongozi wa dini waliopokea hela ya sadaka kutoka kwa Raisi kujenga majengo ya dini anawaita wamepokea rushwa kwa Raisi utafikiri hizo pesa ziliingia mifuko binafsi na akaunti binafsi za Mufti na maaskofu katoliki,Lutheran, Pentecoste nk

Toka siasa za vyama vya siasa zianze Tanzania toka hata kipindi cha chama kimoja nchi haijawahi pata mwanasiasa yeyote mdhalilishaji viongozi wa dini openly kama Tundu Lisu

Kiongozi wa dini yeyote akiitisha mchango wa jengo kutoka kwa yeyote mwenye mapenzi mema na huo mradi Raisi akitoa ooh huyo kiongozi wa dini kalamba asali za pesa za Abdul wakati hata yeye ilikuwa ruksa kuchangia

Nasema Lisu mwehu na mbinafsi mno mfano alipochangisha pesa yake binafsi kununua gari yake CCM waliposema tutakuchangia alikubali harakq kuwa anapokea mchango kutoka kwa yeyote mwenye mapenzi mema na yeye apate gari CCM kweli wakampa hela milioni tano na ushee hakusema cha ohh hizi hela za Abdul sitaki mnilambishe asali kama mlivyolambisha viongozi wa dini alizipokea a

Viongozi wa dini wamuombee yeye kwa lipi ? Kwa matusi aliyowaporomoshea kuwa wamelamba asali kula pesa za Abdul kuchangia michango ya project za makanisa na misikiti yao?

Watamuombea maombi yapi kwa mfano?
 
Lissu angejikita kwenye sera za chama chake badala ya kuanza kuwanyooshea vidole viongozi wa dini. Hapo anakosea mno. Huo ni udikteta wa kipuuzi mno.
 
Back
Top Bottom