Pre GE2025 Tundu Lissu: Wabunge 19 wakitaka kurudi waje wakieleze chama waliingiaje Bungeni

Pre GE2025 Tundu Lissu: Wabunge 19 wakitaka kurudi waje wakieleze chama waliingiaje Bungeni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Joined
Nov 19, 2024
Posts
94
Reaction score
307
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, ameweka wazi kuwa kama wabunge 19 waliofukuzwa chama wanataka kurejea waje wakieleze chama waliingiaje bungeni.

Lissu ametoa kauli hiyo wakati wa mahojiano na kituo cha habari cha Bongo FM siku ya Ijumaa, Januari 24, 2025, ambapo ameonesha mashaka juu ya uhalali wa mchakato uliowawezesha wabunge hao kufika bungeni, akidai kuwa kuna maswali mengi yasiyojibiwa kuhusu hatua hiyo.

Lissu amesisitiza kuwa wabunge hao wanapaswa kueleza hadharani mchakato wa wao kuingia bungeni, akitilia shaka usahihi wa hatua hiyo. Ametoa mfano wa Nusrat Hanje mmoja wa wabunge hao, ambaye alikamatwa na kuwekwa gerezani lakini baadaye alionekana bungeni kama mbunge wa viti maalum.

Kwa mujibu wa Lissu, hatua ya wabunge hao kurudi CHADEMA inapaswa kuwa na dhamira ya kweli ya kutafuta suluhu, siyo kwa sababu uchaguzi mkuu unakaribia na wanatafuta kuhalalisha nafasi zao za ubunge. Lissu ameweka bayana kuwa kurejea kwa wabunge hao kunapaswa kuambatana na uwazi wa nia na mchakato wa kweli wa kujenga chama.

Pia soma
 
Back
Top Bottom