Uchaguzi 2020 Tundu Lissu wasamehe maadui zako lakini usisahau majina yao!

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu wasamehe maadui zako lakini usisahau majina yao!

TWisheshagi

Member
Joined
May 2, 2020
Posts
14
Reaction score
209
Jina la Tundu Lissu, ndio linalotajwa sana kwa Sasa kuliko Mtazania yeyote hususan kwenye mitandao ya kijamii.

Jina hili linatajwa kwa ubaya na uzuri. Kwa kipindi cha takribani siku mbili mfululizo, Jina la Lisu limeingia kwenye orodha ya majina yanayofuatiliwa sana na watu wengi.

Katika mitandao ya kijamii ya Tanzania na hata Afrika Mashariki, Jina la Lissu limeingia kwenye orodha ya majina au matukio makubwa yanayofuatiliwa na watu wengi.

Katika orodha hiyo, lipo Jina la mwanasoka Leo Messi, hususan katika kipindi hiki anapohusishwa na kuachana na timu yake ya Barcelona. Sambamba na hilo, jambo jingine ni COVID-19.

Hii ni kwa mujibu wa uchunguzi wangu binafsi. Watakaopinga hilo wanakaribishwa kupinga. Wanaojiandaa kutukana, basi watukane vizuri. Japo wanapaswa kukumbuka kuwa hoja hazipigwi rungu!

Lissu, hatajwi wala kufuatiliwa kwa bahati mbaya. Lisu anatajwa na kufuatiliwa kwa Wingi kwa sababu ameweza kuziba ombwe la uwepo kwa wanasiasa uchwara!

Nchi yetu ina naksi kubwa ya wanasiasa makini! tuna kundi kubwa la wanasiasa wazurulaji na uchwara! Lisu, amevuka hiyo mipaka! Amekuwa mwanasiasa anayeelekea kuwa "mwanasiasa taasisi". Hii ni sifa ya kipekee na wapo wachache Duniani.

Katika ukanda wetu huu yupo MAALIM SEIF. Huyu amevuka mipaka ya kawaida, bali ni taasisi. Yupo Raila Odinga wa Kenya. Lisu anaweza kuongezeka kwenye orodha hii adhimu!

Nimesikiliza hoja alizozitoa Lisu wakati akiweka mapingamizi kwa wagombea wenzake. Nimesikia pia maelezo ya Tume ya Uchaguzi wakati wakitupilia mbali mapingamizi ya Lissu!

Katika hilo, Kuna mambo Machache ya kujadili:

Mosi, Ilitegemewa na kila mtu mwenye akili timamu mapingamizi ya Lisu kutupiliwa mbali na Tume ya Uchaguzi. Wenye akili tungelishangaa sana kama mapingamizi yangelikubalika.

Pili, mapingamizi ya Lissu, yametoa funzo kubwa sana katika siasa za nchi hii. Funzo muhimu ni kuwa katika msimu wa uchaguzi, hata Rais aliyepo madarakani ni mgombea kama wengine na siyo mteule!

Wapo baadhi ya "wajinga" wanaodhani kuwa John Pombe Magufuli, siyo mgombea kama wengine! Huo ni "Ujinga" na upofu! Pingamizi la Lissu, Walau limeanza kufuta matogotogo hayo!

Ushauri wangu kwa Lisu: Ajue kuwa ana maadui wa kificho na Marafiki wengi wa kificho!

Jina la Lissu, ni dawa ya misuli ya moyo! Awasamee maadui zake, lakini asisahau majina yao!

Ndimi, mkulima wa bamia, bonde la mto Simiyu-Magu-Mwanza.
 
Back
Top Bottom