Tundu Lissu yuko sahihi: Majaji wengi hawajahitimu vyuo na elimu zao ni za mitandaoni

Tundu Lissu yuko sahihi: Majaji wengi hawajahitimu vyuo na elimu zao ni za mitandaoni

Kutokana na ushahidi au utetezi mzito uliotolewa na Mh Tundu Lissu natarajia kiti kitakuwa kinapembua vizuri ni mbunge yupi anapaswa kuambiwa alete ushahidi kuthibitisha kauli yake na kwa mantiki hii watu kama kina Tundu, Zitto, Mnyika watakuwa wameshajiondoa automatically kwenye kundi la kuombwa uthibitisho maana kwa upande mmoja wanapewa ushirikiano mkubwa mno na raia mpaka wanapata na taarifa zingine ambazo hata wao hawakuzifahamu kabla. Hii inanipa hisai kuwa hata ule utetezi wa Lema utakuwa ulikuwa ni kama kaa la moto na ndio maana mpaka kesho haujawahi kusomwa hapo bungeni. Kama watataka watu makini kama Tundu Lisu alete ushahidi basi wabadili mfumo ili kuiokoa mihimili kama Judiciary otherwise itakuwa ni mwendeelezo wa kufunuana mchana kweupe!
 
Hawajifunzi hao. Wangekuwa wanajifunza JK angekuwa amejifunza mengi kutoka kwenye safari zake.
 
Wajifunze wachekwe?wale vichwa maji wanajidai wanasikia kumbe wameziba masikio,walishapata mafundisho kibao wanajishaua hawaelewi.Hadhi yao imeshuka chini ya magoti mie siwatofautishi na wavuta unga.
 
:biggrin1: ni kweli lakini majaji wako wengi na hata hatuoni wanachofanya maana kesi zote kubwa serikali ndio mwamuzi wa mwisho sa sijui wao wako pale kufanya nini
Ninachokifahamu mimi yule kihiyo wa kiagata hana integrity yoyote bali anatumia hasira za jando lao. Tusipokuwa makini kwenye kataiba ijayo atawatukana wabunge makini na kulazimisha mambo yasiyo na tija kwa Taifa hili. Kimsingi hatuna AG bali ni mzee wa kutoa matusi tu!!!
 
@fdrJunior upo sahihi sana vyuo hivi vya binafsi nashangaa sana karibu wanafunzi wao wote wanapomaliza wanapata GPA za first and second upper class na wachovu zaidi ndio wanapata second lower ,hii inatia ukakasi hasa kwenye taasisi zenye kukimbilia kuajiri wahitimu wenye GPA KUBWA KUMBE NI MAGALASA.Mfano wakati na hakiki vyeti vya watumishi waliomaliza masomo ili wapandishwe madaraja ofsiin kwangu WAHITIMU WA SAUT walikuwa na First and second Upper class na ukiwaona ni wachovu kabisa in skills,understanding and exposure.Nilipomaliza mie UDSM vichwa ni vingi lakini GPA inakuwa regulated sana.Pass Grade ya UDSM ni sawa na First class ya Tumaini na SAUT na hakuna ubishi wowote.
Katika Utafiti na kuuliza wahitimu wa UDSM law school wengi hawataki kazi za Uhakimu na kama akienda ni muda mfupi anafanya kazi hizo na baadae anakwenda Chamber-Advocate kitu ambacho ni tofauti sana na wahitimu wa vyuo vingine kama TUMAINI,MZUMBE,SAUTambao wanalilia kazi za uhakimu amabo ni ofisi za serikali na baada ya muda ndio hao wanakuwa promoted kuwa Majaji na maafisa wa idara za mahakama wakati ni Vilaza wa kutupwa.

Tungependa kuona utawala wa UDSM unafanyia kazi malalamiko haya ya sisi wahitimu wake.
Kwamba wahadhiri wake wana hulka ya kubana marks na kufanya GPA kuwa ndogo.
Bila kuchukua hatua za makusudi, watasababisha wahitimu wa UDSM kuwa phase-out ktk soko la ajira!
Watawala wa UDSM waache kujivunia ranking za kimataifa zinazokitukuza chuo wakati hapa nchini ,mara zote, GPA kinabaki kigezo kikuu kutambua uwezo wa ''a prospective employee''.Ninaelewa fika suala la GPA linawaumuza wengi wa wana UDSM kwa kuwa nami ni mhanga wa kadhia hii.
Wito wangu kwa wahitimu wenzangu wa UDSM ni kwamba kamwe tusivunjike moyo.Badala yake tuonyeshe umahiri ,weledi na umakini ktk kazi zetu.

 
Tatizo lake warema ataki kukubali kuwa TL yuko juu. Ni kawaida kwa mtu anaye jifanya anajua kuto penda kujifunza kwa kutoka wengine. Ila kimoyo moyo anamkubali anasema huyu jamaa jembe. Kutoa kauli ili umma usikie kama anakubaliana TL hapo ndiyo anashikwa kigumizi. Kama serikali ingekuwa inaifanyia kazi michango ya wataalam wetu wa fani mbali mbali basi tusingekuwepo hapa tulipo. Serikali yetu inaona siasa ndiyo kila kitu. Hata sehemu inayo husu taalumu basi serikali inaingiza siasa, na wataalam na wakisha ona kuwa taaluma imeingiliwa na siasa wanaamua kuwachia wanasia, na hapo ndipo mambo yanakwenda mrama, na kuishia kuwa nchi yenye rasilimali nyingi lakini omba omba zaidi ya matonya.
 
RIPOTI YA TUNDU LISSU NA KESI MAARUFU YA "KIBALAGHASHIA"

Hivi karibuni, Mheshimiwa Tundu Lissu alisoma Bungeni ripoti yake ya utetezi ambayo ameipeleka kwa kamati ya maadili ya Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ambapo katika ripoti yake hiyo Mheshimiwa Lissu amebainisha mambo mbalimbali ambayo mengi ni tuhuma nzito dhidi ya Majaji wa Mahakama Kuu, tuhuma ambazo tayari zimeshasambazwa kwa umma hata kabla hazijajadiliwa na kamati husika ya maadili ya Bunge,kwa kufanya hivyo ni wazi kuwa, Majaji waliotajwa wamehukumiwa hata kabla tuhuma hizo hazijathibitika, lakini pia mhimili nzima wa Mahakama na Idara zake zimehukumiwa na kufanywa ionekane kuwa Mahakama nchini zinafanya shughuli zake kwa namna ya "hovyo" na kwa maana hiyo, ni wazi imani ya watu katika chombo hiki muhimu cha kutoa haki itashuka kwa jamii.

Ingwa Mheshimiwa Lissu kwa makusudio,ama kwa makosa ya kibinadamu ama kutokana na hulka yake ya kukurupuka ameainisha vipengele vingi ambavyo HAVIKO SAHIHI ama vinahitaji ufafanuzi wa kina, moja ya vipengele hivyo;

Katika Ripoti hiyo, inataja kuwa UAMUZI wa Jaji Kiongozi kumhamisha hakimu kwa maamuzi asiyokubaliana nayo UNATUMIKA na kukubaliwa kama HUKUMU ama ADHABU kwa Hakimu huyo. Ripoti ya Mheshimiwa TUNDU inaonesha kwamba maamuzi ambayo Jaji kiongozi hakukubaliana nayo yanahusu kesi aliyoiita maarufu ya "kibalaghashia" Kumbukumbu zangu zinanionyesha kwamba kesi hiyo iliwahi kuripotiwa kwa mshangao katika magazeti kadhaa, kwamba, hakimu mmoja amehukumu mtu kwenda jela kwa kuvaa kibalaghashia mahakamani.

Kwa nchi kama Tanzania ambako vazi la kibalaghashia ni vazi rasmi katika baadhi ya dini, haikutegemewa kwa hakimu huru na mwenye busara kumfunga mtu kwa kuvaa kibalaghashia mahakamani. Kwa namna suala hilo lilivyovuta hisia za watu wengi hapa nchini na mbaya zaidi HISIA ZA UDINI, nisingeshangaa hata kidogo kama hakimu kama huyo angechukuliwa hatua yeyote ya kinidhamu achilia mbali kuhamishwa ambako Mhe. TUNDU LISSU nakulalamikia na kuonesha kuwa JAJI KIONGOZI amekosea na alimuonea Hakimu huyo.

Mahakama kama chombo cha kutoa haki kinapaswa kujiweka katika hali ambayo kila mtu atakiona kama chombo huru kisichokuwa na muegemeo wowote wa KISIASA, KIDINI AU KIKABILA. Maamuzi mabovu kama hayo hayakupaswa kutolewa na chombo kama Mahakama. Najiuliza TUNDU LISSU analenga nini katika kutetea hili.???

Lakini pia, nijuavyo ni kuwa uhamisho kwa mahakimu na majaji ni utaratibu wa kawaida wa kazi na wala hamna hakimu yeyote mwenye hatimiliki ya kuwa Dar es salaam ama kufanya kazi Dar. Wala mahakimu walioko mikoani hawako huko kwa sababu ya adhabu wala mahakimu waliopo Dar es salaam hawako Dar kwa sababu ni weledi zaidi ya walio mikoani.

Udhaifu huu wa hoja ya Mhe. Tundu Lissu unaibua Upya HISIA ZA UDINI zilizojitokeza hapo kabla wakati wa kesi hiyo. Pia, Lissu analeta mkanganyiko mkubwa baada ya Ripoti yake hiyo ambayo inachukua sura ya kutaka kulifanya Bunge ni chombo cha kuisimamia mahakama, na hivyo kupoteza tafsir na mantiki ya mihimili mitatu ya serikali ya Tanzania. Kwa mujibu wa ibara ya 107 A, mamlaka ya kufasir sheria na kutoa haki yako mikononi mwa mahakama. Hakuna hata sehemu moja katika Katiba ambapo Bunge limepewa mamlaka yoyote ya kuisimamia na kuishauri mahakama.

Nafasi ya Bunge kuirekebisha mahakama katika mfumo wa "checks and balance" ni kwa njia ya kutunga sheria TU. Kwa kitendo cha kuisoma ripoti hiyo katika hadhara ya Bunge na kulitumia Bunge kuidhalilisha mahakama na majaji wake ni wazi Mhe. TUNDU analenga kulichonganisha Bunge na Mahakama.
 
kwahiyo hapa unaongelea issue moja tu, KIBALAGHASHIA. Huna jingine.

Kati ya yoooote aliyoyasema Tundu Lisu, wewe umeoba Kibalaghashia tu baaaasi! Na umetumia mfanp huo kwa maoni na mtazamo wako wa kidini kuona kwamba Lisu amekosea saaana kuhusu madai ya ukiukaji wa taratibu katika kuteua majaji?!

Akili mchuzi wa nazi.
 
Mkuu hili sio jukwaa la mahaba na mahusiano. ni jukwaa la siasa. Jukwaa hili utani huwa haujadiliwi sana.
Kwanza kujibu hoja nzito ya Mh. Tundu Lissu kwa kumuita Tundu la ndege, kunaondoa maana nzima ya hoja yenyewe maana mtoa hoja hana heshima wala hekima.

Pili mandishi marefu hivi ukiyaunganisha bila kuwa na paragraph za maana yanakuwa hayaleti maana. ANgalau ungecopy na kupaste ile format ya ripoti ya Mh. Tundu Lissu

Ngoja wadau watakuja kukusaidia kuchngia ila sijui kama wataichambua hiyo barua yako kwa uandishi huu

Eid Mubarak
 
..nilipoisoma makala ya Tundu Lissu akiitaja kesi ya "kibaragashia" I knew this was coming.

..Tundu Lissu alitakiwa awe makini zaidi na zaidi na kuielewa hadhira anayo-deal nayo.

..ukiachilia suala la "kibaragashia," naamini hoja ya Tundu Lissu imejaa madai mazito na serikali inapaswa kuyafanyia kazi.

..Tundu Lissu hajaidhalilisha mahakama. Raisi ndiye ameidhalilisha mahakama yetu kwa kuteua majaji wenye maadili na rekodi zenye mawaa.
 
Mkuu ile report ya Tundu Lisu inahitaji vichwa kama elfu moja kuijadili.. Na mpaka sasa hawajaijibu.. Wewe huiwezi hata kidogo.. Waachie Werema & co watafute cha kujibu kama watapata.. Hakuna majibu ya "nijuavyo mie" mule..

Sent from Tora Bora
 
Kusema kweli kwa ile taarifa ya Lissu chombo cua mahakama kimeonekana ni cha ajabu ajabu na watu walioisoma wamekosa imani kabisa na chombo hiki ambacho kinatakiwa kiwe ni chombo cha haki kischo na mawaa kama aliyoyaainisha Lissu.

Lakini kama viongozi wakuu wa nchi wanakifanya kionekana hakina maana, waanwanchi watakuwa na imani nacho kiasi gani?
Serikali haiwei kuendeshwa kwa udini ua urafiki.
Kuna kikomo cha mambo ya namna hii.
Ajabu, Tanzania ni kama haina protocol ya kumwongoa raisi!
 
kwahiyo hapa unaongelea issue moja tu, KIBALAGHASHIA. Huna jingine.

Kati ya yoooote aliyoyasema Tundu Lisu, wewe umeoba Kibalaghashia tu baaaasi! Na umetumia mfanp huo kwa maoni na mtazamo wako wa kidini kuona kwamba Lisu amekosea saaana kuhusu madai ya ukiukaji wa taratibu katika kuteua majaji?!

Akili mchuzi wa nazi.

Kama kawaida na akili zetu za kawaida: kutafuta kosa moja katika mazuri kumi.
Ukisome signature yake utamwelewa ni mtu wa namna gani.
 
Tatizo mtoa mada unamchukulia kirahisi sana Mh. TL...kwa taarifa yako mkuu wa nchi anamuogopa huyu afadhali ya ukoma
 
tatizo mleta thread hujaziona "addendum" nakushauri mtafute TL atakupa baada ya hapo utaelewa vizuri
 
Watu wengine bana, wewe unajaribu kujibu hoja kwa kutumia mipasho? Wewe mpuuzi sana, tena sana.
 
Nilijua report ya Mhe. Tundu Lisu imepata mpanguaji wa hoja swaaaafi kumbe unajaribu kurudia yale yale! Those days are over, kumbuka tu kuwa sasa hivi kila unachofanya watu wanaufahamu mkubwa wa mambo mbali mbali, wanafuatilia na wanabidii ya kujua vitu kama hivyo. Ni bora kuwa makini unapojaribu kujibu au kujenga hoja yenye malengo ya kuwashawishi watu wengine.

Eid Mubarak!!
 
Huu upuzi ulishaletwa hapa na mtetezi wa dhaifu anaye jiita Tandale One, au amebadili ID?
 
Zile tuhuma alizotoa mh.Lissu ni nzito,hazipaswi kujibiwa kwa mipasho.Majaji wanatuletea aibu na elimu zao finyu na kuipendelea serikali.Mahakama imekuwa pango la wezi na wakandamizaji wa utu na haki ikiwamo serikali,mtu aliyestaafu anapandishwa cheo?au anaongezewa mkataba? Outrageous!
 
Back
Top Bottom