RIPOTI YA TUNDU LISSU NA KESI MAARUFU YA "KIBALAGHASHIA"
Hivi karibuni, Mheshimiwa Tundu Lissu alisoma Bungeni ripoti yake ya utetezi ambayo ameipeleka kwa kamati ya maadili ya Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ambapo katika ripoti yake hiyo Mheshimiwa Lissu amebainisha mambo mbalimbali ambayo mengi ni tuhuma nzito dhidi ya Majaji wa Mahakama Kuu, tuhuma ambazo tayari zimeshasambazwa kwa umma hata kabla hazijajadiliwa na kamati husika ya maadili ya Bunge,kwa kufanya hivyo ni wazi kuwa, Majaji waliotajwa wamehukumiwa hata kabla tuhuma hizo hazijathibitika, lakini pia mhimili nzima wa Mahakama na Idara zake zimehukumiwa na kufanywa ionekane kuwa Mahakama nchini zinafanya shughuli zake kwa namna ya "hovyo" na kwa maana hiyo, ni wazi imani ya watu katika chombo hiki muhimu cha kutoa haki itashuka kwa jamii.
Ingwa Mheshimiwa Lissu kwa makusudio,ama kwa makosa ya kibinadamu ama kutokana na hulka yake ya kukurupuka ameainisha vipengele vingi ambavyo HAVIKO SAHIHI ama vinahitaji ufafanuzi wa kina, moja ya vipengele hivyo;
Katika Ripoti hiyo, inataja kuwa UAMUZI wa Jaji Kiongozi kumhamisha hakimu kwa maamuzi asiyokubaliana nayo UNATUMIKA na kukubaliwa kama HUKUMU ama ADHABU kwa Hakimu huyo. Ripoti ya Mheshimiwa TUNDU inaonesha kwamba maamuzi ambayo Jaji kiongozi hakukubaliana nayo yanahusu kesi aliyoiita maarufu ya "kibalaghashia" Kumbukumbu zangu zinanionyesha kwamba kesi hiyo iliwahi kuripotiwa kwa mshangao katika magazeti kadhaa, kwamba, hakimu mmoja amehukumu mtu kwenda jela kwa kuvaa kibalaghashia mahakamani.
Kwa nchi kama Tanzania ambako vazi la kibalaghashia ni vazi rasmi katika baadhi ya dini, haikutegemewa kwa hakimu huru na mwenye busara kumfunga mtu kwa kuvaa kibalaghashia mahakamani. Kwa namna suala hilo lilivyovuta hisia za watu wengi hapa nchini na mbaya zaidi HISIA ZA UDINI, nisingeshangaa hata kidogo kama hakimu kama huyo angechukuliwa hatua yeyote ya kinidhamu achilia mbali kuhamishwa ambako Mhe. TUNDU LISSU nakulalamikia na kuonesha kuwa JAJI KIONGOZI amekosea na alimuonea Hakimu huyo.
Mahakama kama chombo cha kutoa haki kinapaswa kujiweka katika hali ambayo kila mtu atakiona kama chombo huru kisichokuwa na muegemeo wowote wa KISIASA, KIDINI AU KIKABILA. Maamuzi mabovu kama hayo hayakupaswa kutolewa na chombo kama Mahakama. Najiuliza TUNDU LISSU analenga nini katika kutetea hili.???
Lakini pia, nijuavyo ni kuwa uhamisho kwa mahakimu na majaji ni utaratibu wa kawaida wa kazi na wala hamna hakimu yeyote mwenye hatimiliki ya kuwa Dar es salaam ama kufanya kazi Dar. Wala mahakimu walioko mikoani hawako huko kwa sababu ya adhabu wala mahakimu waliopo Dar es salaam hawako Dar kwa sababu ni weledi zaidi ya walio mikoani.
Udhaifu huu wa hoja ya Mhe. Tundu Lissu unaibua Upya HISIA ZA UDINI zilizojitokeza hapo kabla wakati wa kesi hiyo. Pia, Lissu analeta mkanganyiko mkubwa baada ya Ripoti yake hiyo ambayo inachukua sura ya kutaka kulifanya Bunge ni chombo cha kuisimamia mahakama, na hivyo kupoteza tafsir na mantiki ya mihimili mitatu ya serikali ya Tanzania. Kwa mujibu wa ibara ya 107 A, mamlaka ya kufasir sheria na kutoa haki yako mikononi mwa mahakama. Hakuna hata sehemu moja katika Katiba ambapo Bunge limepewa mamlaka yoyote ya kuisimamia na kuishauri mahakama.
Nafasi ya Bunge kuirekebisha mahakama katika mfumo wa "checks and balance" ni kwa njia ya kutunga sheria TU. Kwa kitendo cha kuisoma ripoti hiyo katika hadhara ya Bunge na kulitumia Bunge kuidhalilisha mahakama na majaji wake ni wazi Mhe. TUNDU analenga kulichonganisha Bunge na Mahakama.