Tundu Lissu yupo wapi kwenye suala la Sativa kutekwa na Mchungaji Msigwa kuhamia CCM?

Tundu Lissu yupo wapi kwenye suala la Sativa kutekwa na Mchungaji Msigwa kuhamia CCM?

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
1. Sijamsikia akisema lolote kuhusiana na kijana kutekwa, kupigwa risasi, na kutupwa Katavi National Park. Labda hajasikia au imekumbusha machungu ambayo hajapata nguvu ya kuzungumza hadi akae sawa. Nilitegemea kusikia akiongelea hili kwa sababu, ni kweli yeye alipigwa risasi ghafla na alihisi maumivu muda mrefu hadi kupona. Lakini mateso ya Sativa yalikuwa makubwa zaidi kwani alijua wanamuua ili awe chakula cha mamba na fisi, alitelekezwa porini hadi akajikokota na kufika kwa watu. Ni kitu kikubwa mno. Naamini kati ya watu waliosurvive to tell the tale ni TL na Sativa. Mlio karibu naye mshtueni kama hajasikia hili tukio.

Pia soma:
Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’

2. Alikuwa karibu sana na Msigwa, tunajua hajisikii vizuri kwa yale yanayoendelea kwenye chama chake, yeye sio mnafiki, siku zote amekuwa mkweli. Yeye ametelekezwa, hata hela kununua gari watu wamechangishwa na Mbowe hajahamasisha mchango.

Pia soma: Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM

3. Ni lini TL, mwanasheria nguli, atatengeneza nyaraka na kwenda kufungua chama kipya kabla ya uchaguzi 2025? Aone kama Watanzania hawatamiminika kwake. Hivi TL anajielewa kwamba mioyo ya Watanzania wengi sana ipo pamoja naye na Watanzania wanamuelewa sana? Hivi analitambuaga hili? Anatambua kwamba Watanzania wengi sana wapo hata Chadema kwa sababu yake tu na sio kwa sababu ya wengine wowote? Kwa sababu anaeleweka, ana uwezo na hujenga hoja na hupiga kwenye mishoni tu, hapepesi macho. Ukiaminiwa namna hii na Watanzania, kinachomshinda kuanzisha chama kipya mapema ni nini ili kieleweke? Watu wafanye siasa za kweli, zisizo za kinafiki.

Mlio karibu naye mwambieni namsalimia.
 
Yaani hata angekuwa ametukana au kufanya chochote, hakustahili kufanyiwa hayo aliyofanyiwa. kwanini msijibizane kwa hoja, yeye naye angekuwa na vitendea kazi kama vyenu si mngeona bora mjibizane kwa hoja? kwahiyo kwasababu ninyi mna dola ndio maana mkaamua kumfanyia yale?

Mioyo yenu imejaa mashetani, ninyi ni watumishi wa mashetani, na mtakula mshahara anaokulaga shetani. mark my words, Mungu aliyemwokoa yule kijana hajawahi kudhihakiwa na ukabaki salama. mwobopeni Mungu, yakimbieni mabaya, pendeni kufanya mema, jueni kuwa sote tunapoishi hapa duniani mbabe wetu ni mmoja tu, Mungu, hata uonee au kujifanya wewe mungumtu, siku yako ipo.
 
yaani hata angekuwa ametukana au kufanya chochote, hakustahili kufanyiwa hayo aliyofanyiwa. kwanini msijibizane kwa hoja, yeye naye angekuwa na vitendea kazi kama vyenu si mngeona bora mjibizane kwa hoja? kwahiyo kwasababu ninyi mna dola ndio maana mkaamua kumfanyia yale? mioyo yenu imejaa mashetani, ninyi ni watumishi wa mashetani, na mtakula mshahara anaokulaga shetani. mark my words, Mungu aliyemwokoa yule kijana hajawahi kudhihakiwa na ukabaki salama. mwobopeni Mungu, yakimbieni mabaya, pendeni kufanya mema, jueni kuwa sote tunapoishi hapa duniani mbabe wetu ni mmoja tu, Mungu, hata uonee au kujifanya wewe mungumtu, siku yako ipo.
Kujua whether amepata fundisho au la, tumsubiri apone halafu aendelee na matusi yake ya nguoni
 
Sasa kama ni mtukanaji hivyo basi alipata mshahara wa matusi yake, nazungumzia huyo kijana aliyetekwa na kupwa hifadhini awe kitoweo cha wanyama
 
1. Sijamsikia akisema lolote kuhusiana na kijana kutekwa, kupigwa risasi, na kutupwa Katavi National Park. Labda hajasikia au imekumbusha machungu ambayo hajapata nguvu ya kuzungumza hadi akae sawa. Nilitegemea kusikia akiongelea hili kwa sababu, ni kweli yeye alipigwa risasi ghafla na alihisi maumivu muda mrefu hadi kupona. Lakini mateso ya Sativa yalikuwa makubwa zaidi kwani alijua wanamuua ili awe chakula cha mamba na fisi, alitelekezwa porini hadi akajikokota na kufika kwa watu. Ni kitu kikubwa mno. Naamini kati ya watu waliosurvive to tell the tale ni TL na Sativa. Mlio karibu naye mshtueni kama hajasikia hili tukio.

2. Alikuwa karibu sana na Msigwa, tunajua hajisikii vizuri kwa yale yanayoendelea kwenye chama chake, yeye sio mnafiki, siku zote amekuwa mkweli. Yeye ametelekezwa, hata hela kununua gari watu wamechangishwa na Mbowe hajahamasisha mchango.

3. Ni lini TL, mwanasheria nguli, atatengeneza nyaraka na kwenda kufungua chama kipya kabla ya uchaguzi 2025? Aone kama Watanzania hawatamiminika kwake. Hivi TL anajielewa kwamba mioyo ya Watanzania wengi sana ipo pamoja naye na Watanzania wanamuelewa sana? Hivi analitambuaga hili? Anatambua kwamba Watanzania wengi sana wapo hata Chadema kwa sababu yake tu na sio kwa sababu ya wengine wowote? Kwa sababu anaeleweka, ana uwezo na hujenga hoja na hupiga kwenye mishoni tu, hapepesi macho. Ukiaminiwa namna hii na Watanzania, kinachomshinda kuanzisha chama kipya mapema ni nini ili kieleweke? Watu wafanye siasa za kweli, zisizo za kinafiki.

Mlio karibu naye mwambieni namsalimia.
Kwa nini umhusishe Tundu Lissu na mambo binafsi? Na wewe umeingia mkenge kuwa huyu Sativa ametekwa sababu ya ukosoaji wa viongozi wa Serikali? Hakuna kitu kama hicho. Huyu ana mahasimu wake kwenye mambo ya betting na mtaani. Ona warning aliyoitoa kwa wabaya wake kabla hajatekwa:
Screenshot_20240628_065623_Parallel Space.jpg

Ni kwamba mahasimu wake walimtaiti kabla yeye Sativa hajawapiga mshale wa jicho. He got a right pay for his actions
 
duh, ila dunia hii ina kila type wa wanadamu, wengine hakika walipaswa kuishi porini. uzuri ni kwamba hata ninyi mtakufa tu, Mungu ndiye Boss wa wote.
 
Back
Top Bottom