jogoolashamba
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 348
- 71
Umesomeka mkuu Jogoo wa shamba..nisaidie machache TL aliyoongea ndivyo sivyo nami nielimike
Tatizo lako Inkoskaz unasoma "Between the Lines". Hiyo inakufanya uwe Ticha mbaya. Soma juu ya lines, nimekwambia hivi TL anapigia kelele mzunguko wa umaskini usiokuwa na dawa. Huwezi kulalamikia tatizo la Kikwete kwa Kikwete, la CCM kwa CCM. Katika lugha ya kisheria harakati zote za TL ni "Null and Void". Wakitokea kukubaliana kupeana dola huko huko WaTz tutabaki na matatizo yaleyale isipokuwa sasa yatakuwa yanatokea CHADEMA badala ya CCM.
Yachunguze yote anayobwekea TL, dawa ni TL mwenyewe, na ndiyo anatafutia dola! Huo ndiyo ujanja wa Wagumu wenye hadhara inayowasikliza bila kuelewa tatizo ni nini! Wote wanangoja TL atafute dawa wakati TL anangoja Kikwete ndiyo atafute dawa, si ujinga huo. Si umeona CHADEMA na KAF eti wametafuta dawa ya sheria ya Mswada wa Katiba kwa kwenda kukutana na Kikwete Ikulu? Eti fumbo iko katika Mwafaka.
Basi kama hujaelewa mpaka hapo usiniulize tena nisije nikaanza kusakwa na wababe wanaotembea usiku. Kibanda na Ulimboka wote wamemwachia Mungu. Kina TL hawatafuti majibu kwa Mungu, ebu achana nami Jogoolashamba nipate usingizi hata wa masaa machache yaliyobaki.