Tundu Lisu ana Wafuasi wengi sana, hapa Bar tulipo Wote wanamfagilia Lisu, kweli huyu TAL ni Mtu wa Mabadiliko!

Kura zinapigwa ukumbini sio bar...pale ukumbini pazito maswali watu wanagongwa vichwani upepo imekuwa mgumu kwa lisu...anaomba kura kwa kusema ishirini tosha ili yeye aingie...amerudia zaidi ya Mara tano...
 
Hivi huyu odero kwa kumwangalia harakaharaka atakuwa yuko kambi ipi kati ya kambi FAM na kambi TAL?
 
Your browser is not able to display this video.
 
Wa Mjini Team Vs Wakuja Team, kazi sasa kwa wakuja kuji mobilize rasilimali watu, rasilimali fedha kufadhili movement hii mpya ya watu wa mikoani ambao wanaamini Ofisi Ndogo ya CHADEMA Kinondoni na CHADEMA Ofisi Kuu Mikocheni kuna mabilioni ya fedha zakuokota.

MAKALA MAALUM SIASA 2025
HALI YA KISIASA TANZANIA, SIASA ZA VUVUGUGU YAANI MOVEMENT

Kinachoendelea ndani ya CHADEMA kuhusu chaguzi za ndani, chama cha people's power nguvu ya umma kitaingia mitaani siyo tena kama taasisi inayoongozwa na Freeman Mbowe au Tundu Lissu au wanasiasa wengine tajwa wajulikanao na umma bali kutatokea kundi la Movement.

Kundi hilo litaongozwa na mtu au kikundi nje ya Freeman Mbowe, nje ya Tundu Lissu wasiofuata mkondo uliozoeleka wa maandamano, matamko au press conference kibao kisha mikutano ya kuita vyama vyote vya siasa kuzungumza mustakhabali wa nchi, katiba mpya , uchaguzi huru n.k kupoteza muda ili watawala waendelee kidogo kubaki madarakani.


Movement hiyo mpya ya kihistoria itapa kwa mara ya kwanza kuungwa mkono na umma mpana, vyama vya kitaaaluma, viongozi wa kiimani, wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu, vijana wasio katika sekta rasmi za ajira n.k

Movement hii itaipa tabu sama serikali iliyopo madarakani iliyozoea kutumia msajili wa vyama, baraza la vyama vya siasa vilivyosajiliwa, viongozi wa kiroho.

Picha maktaba : Mkutano wa baraza la vyama vya siasa.

Movement hii itakuwa ina msimamo mkali wa kudai haki, demokrasia na uchaguzi huru haraka iwezekanavyo, kiasi utawala utatahayari na kukengeuka lipi lifanyike kuzima vuguvugu hili litakalo kuwa limejitokeza mitaani, mijini kwa wingi bila kuwa na hofu.

Vuguvugu la nchini Mozambique linaloongozwa na Venancio Mondlane ambaye hakuwa mmoja wa wanasiasa wa chama tajwa aliyeibuka na kuungwa mkono na PODEMOS ni mfano hai kuwa FRELIMO ilizoea siasa za kurubuni vyama vya RENAMO n.k kuzungumza yasiyoisha kila mwaka , na wananchi kubaini hilo ba kuamua kuunga mkono movement mpya ya Venancio Mondlane. Na tumeona matokeo ya yanayoendele Msumbiji kwa sasa.

Kazi kwa chama dola kilichodhibiti mihimili ya Bunge, Mahakama, mfumo wa haki jinai na mchakato wa uchaguzi kufanya maamuzi magumu sasa, kwa ajili ya kudumisha sifa ya taifa letu sote watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…