PreGE2025 Tundu lisu na CHADEMA yake wasipokuwa makini wanaenda kuandika historia mbaya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
1,222
Reaction score
2,912
Sababu ziko nyingi lakini kwa uchache tu haya ndio yanayooneka waziwazi:

1. Wameshindwa kuvunja makundi waliyoyatengeneza kipindi cha kampeni za uchaguzi wao wa ndani. Makundi yanazidi kukomaa na athari yake itakuwa kubwa wakati wa uteuzi wa wagombea. Kuna timu wagombea wake watakatwa hata kabla ya kukatwa na tume

2. Viongozi wa juu bado wanachochea makundi badala ya kuunganisha watu

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

3. Zamani adui wa CHADEMA alikuwa CCM, Serikali na Polisi lakini kwasasa wamejiongezea adui mwingine wa ndani anayeitwa "Timu Lisu na Timu Mbowe". Huyu ni adui hatari sana kwani mara nyingi ni bora familia ipigwe na adui wa nje kuliko kuwa na adui ndani ya familia. Wanafamilia wakiwa na adui wa nje ni rahisi kuungana kumkabili kuliko kuwa na adui ambaye ni mwanafamilia mwenzao. Huyu ni rahisi sana kuigawa familia na kufanya kila upande ujione uko sahihi na bora kuliko upande mwingine. Hiki ndicho Lisu na wenzake wameshindwa kukibaini

4. Wameshindwa kudhibiti wafuasi wao wa mitandaoni wanaopingana na baadhi ya wanachama au maelekezo ya viongozi wao. Hii inawataarifu maadui zao wa nje kuwa hawa watu hawaelewani ndani
 
Kuhusu makundi na Blaa blaah kama hizo.

Ni mbwembwe za walopoteza, walotaman Ubunge, na ambao wake zao ni COVID-19 , Hawa wote watapoteza Kila kitu .

Nmewah kusema, Kuna chama watahamia ili wakagombe ubunge.

Ikn mwendo ni ule ule, NRNE
 
Sababu ziko nyingi lakini kwa uchache tu haya ndio yanayooneka waziwazi:

1. Wameshindwa kuvunja makundi waliyoyatengeneza kipindi cha kampeni za uchaguzi wao wa ndani. Makundi yanazidi kukomaa na athari yake itakuwa kubwa wakati wa uteuzi wa wagombea. Kuna timu wagombea wake watakatwa hata kabla ya kukatwa na tume

2. Viongozi wa juu bado wanachochea makundi badala ya kuunganisha watu

3. Zamani adui wa CHADEMA alikuwa CCM, Serikali na Polisi lakini kwasasa wamejiongezea adui mwingine wa ndani anayeitwa "Timu Lisu na Timu Mbowe". Huyu ni adui hatari sana kwani mara nyingi ni bora familia ipigwe na adui wa nje kuliko kuwa na adui ndani ya familia. Wanafamilia wakiwa na ugomvi mara zote ugomvi huwa haushii pazuri

4. Wameshindwa kudhibiti wafuasi wao wa mitandaoni wanaopingana na baadhi ya wanachama au maelekezo ya viongozi wao. Hii inawataarifu maadui zao wa nje kuwa hawa watu hawaelewani ndani
Mbona sababu yako ni moja, lakini umeweka nne?
 
Kundi la Mbowe linahujumu uongozi mpya, ni kama bado lina gubu ya uchaguzi.
Wajinga hao, team Mbowe hawapost habari yoyote ya chama, na wala hawamasishi michango ya tonetone. Lakini wamesikia habari hasi inayoratibiwa na ccm wote wamejitokeza. Cdm wasipoteze muda na hao team Mbowe, wana support ya kutosha ya wafuasi wake.
 
Heche atagombea,uwenyekiti,kumuondoa Lissu. Na Lissu atagombea ,uwenyekiti,kutetea nafasi yake!
 
Hatakama iweje,muhimu kuwe na reforms ili CCM na CHADEMA washindane wenyewe,vyombo vya ulinzi na usalama vifanye majukumu yao,yaliyoainishwa kwenye KATIBA.Mtu yeyote asemaye TUINGIE kwenye uchaguzi na hii tume,ambayo ina mapungufu tele,huyo ni adui wa DEMOKRASIA ya kweli.
Tufike mahali tufanye vitu vya akili,tuachane na huu ujinga wa kuzugana,ambapo tunapanga foleni tokea asubuhi hadi jioni,tukijua tunachagua viongozi,na mwishowe machaguo yetu yanakuja yanakuwa compromised.Mi binafsi naona kwangu haina tija,halikadhalika kwa mtu yeyote ambaye ana akili timaru,haina tija.
 
Heche atagombea,uwenyekiti,kumuondoa Lissu. Na Lissu atagombea ,uwenyekiti,kutetea nafasi yake!
Yeyote kati yao,ajitahidi kuongoza kundi la watu wengi,linalotaka REFORMS ili kura ya kila mwananchi IWE na maamuzi.
 
Kundi la Mbowe linahujumu uongozi mpya, ni kama bado lina gubu ya uchaguzi.
Ni kazi ya Tundu Lissu na Heche na kamati kuu kupigana kufa na kupona kuvunja makundi hayana maslahi tena kwa chama chenu. kiongozi mzuri hana kundi.
 
Katika watu ambao upinzani ukiingia madarakani inabidi uwafanyie fitna kuu ni hizi media zinazoshindwa kuwasapoti leo BALILE et al Yani ........
 
Taratibu taratibu yanaanza kutimia. Hii minyukano inayoendelea hadharani haiwezi kuwaacha salama. Nguvu ya ziada inahitajika kunusuru hali hii haraka iwezekanavyo
 
Sababu ziko nyingi lakini kwa uchache tu haya ndio yanayooneka waziwazi:

1. Wameshindwa kuvunja makundi waliyoyatengeneza kipindi cha kampeni za uchaguzi wao wa ndani. Makundi yanazidi kukomaa na athari yake itakuwa kubwa wakati wa uteuzi wa wagombea. Kuna timu wagombea wake watakatwa hata kabla ya kukatwa na tume

2. Viongozi wa juu bado wanachochea makundi badala ya kuunganisha watu

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

3. Zamani adui wa CHADEMA alikuwa CCM, Serikali na Polisi lakini kwasasa wamejiongezea adui mwingine wa ndani anayeitwa "Timu Lisu na Timu Mbowe". Huyu ni adui hatari sana kwani mara nyingi ni bora familia ipigwe na adui wa nje kuliko kuwa na adui ndani ya familia. Wanafamilia wakiwa na adui wa nje ni rahisi kuungana kumkabili kuliko kuwa na adui ambaye ni mwanafamilia mwenzao. Huyu ni rahisi sana kuigawa familia na kufanya kila upande ujione uko sahihi na bora kuliko upande mwingine. Hiki ndicho Lisu na wenzake wameshindwa kukibaini

4. Wameshindwa kudhibiti wafuasi wao wa mitandaoni wanaopingana na baadhi ya wanachama au maelekezo ya viongozi wao. Hii inawataarifu maadui zao wa nje kuwa hawa watu hawaelewani ndani
Chama kinaongozwa kitapeli sana siku hizi.Kwa mara ya kwanza naenda kuipigia kura CCM
 
Si ndio vizuri ili nyie kijani kibichi mpate kupumua au we unasemaje?
 
Back
Top Bottom