Uchaguzi 2020 Tundu punguza kunadi sera ya mishahara kwa wafanyakazi mbele ya watu masikini

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Hongereni kwa kampeni.

Twende kwenye hoja moja kwa moja,binafsi Sina tatizo na watumishi kuongezwa mishahara hiyo ni haki yao lakini ni vyema hoja Kama hii ikachagua majukwaa ya kuizungumzia.

Wafanyakazi hususani wa serikali wa kada zozote ni moja ya kundi ambalo jamii kubwa inaliona kuwa na maisha mazuri au ya nafuu maana ukiacha huo mshahara Hawa Wana fursa za mikopo kwa dhamana ya kazi zao na vimapato vya hapa na pale,ambapo kwa upande wa Pili wa shilingi Kuna kundi kuubwa Sana la vijana hawana kazi,wakulima,wavuvi,machinga na makundi mengine ya jamii wasio na kipato maalumu.Ni rai yangu kwa kua kundi hili la pili ni kubwa Sana na ndio kundi muamzi wa uchaguzi ni vyema sera zako zingejielekeza zaidi kwa Hawa kuliko watumishi.

Sio sawa kuzungumzia mishahara kwa kamii ambayo inaona mtu kuajiriwa ni kulamba bingo regardless of how much one is paid.Jikite kwenye sera za kulainisha ugumu wa maisha na kurahisisha biashara za watu wa kawaida,binafsi hata kwa observation yangu watu wa kawaida Wana Hali mbaya za maisha kuliko kuzungumzia wafanyakazi ,watu wataona Bora huyu huyu aliopo,narudia kusema Chadema msaidieni mgombea wenu kunadi sera kwa lugha rahisi Kama wafanyavyo wagombea wengine wa Upinzani maana kwa sasa anapata muitikio mkubwa zaidi kadiri siku zinavyosogea, Ila sio Kama wanasisiemu huwa wanasoma risala.Nawatakia kampeni yenye mafanikio
 
Unasahau kuwa mtumishi mmoja ana wategemezi wasiopungua 10 nyuma yake, ndio maana tatizo la vyeti feki limeleta mtikisiko mkubwa kwenye jamii hata kama waliobainika ni wachache compared to watumishi waliopo...

Unasahau wasio na kazi wengi tegemeo lao ni wale wenye ajira rasmi na zisizo rasmi. Hao graduate wengi ni tegemezi kwa wenye ajira, think twice, think big
 
Hata mfanyakazi akiongezwa mara mbili ya mshahara wake,hawezi kuwatosheleza hao wategemezi. Kila mtegemezi anahitaji mafanikio yake binafsi..
 
Unasahau kuwa mtumishi mmoja ana wategemezi wasiopungua 10 nyuma yake, ndio maana tatizo la vyeti feki limeleta mtikisiko mkubwa kwenye jamii hata kama waliobainika ni wachache compared to watumishi waliopo...

Unasahau wasio na kazi wengi tegemeo lao ni wale wenye ajira rasmi na zisizo rasmi. Hao graduate wengi ni tegemezi kwa wenye ajira, think twice, think big
Sawa lakini ni wajibu wa mgombea kueleza atafanya nini ili hao wasio na kazi wasiendelee kuwa tegemezi,afu nimezungumzia mtizamo wa jamii kubwa kwa waajiriwa vs wasioajiriwa na serikali
 
Kweye formula ya uchumi[economies of scale] , ukiboresha maisha ya watu kwa kuwaongezea kipato inakuwa directly proportional na maendeleo ya watu wengine... Ukibana kipato cha watu/watumishi hata hao wengine wasio na ajira wataumia zaidi, very simple.
 
Nijuavyo watanzania huwa wanafurahia wanaposikia fulani katumbuliwa kwenye kazi yake. Watanzania wengi wanapenda ile hali Mbaya waliyonayo na wengine wawe nayo pia.
Uzi wako nimeuelewa kuna watu wananuna kusikia wafanyakazi watalamba mishahara minono.
Kweli iongelewe hoja ya mishahara Lakini sio kwa kurudia Sana kila siku na kila Mahala.
 
Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
Na ndio mantiki yangu,Kuna mengi ya kuongelewa mfano tunaambiwa bajeti za dawa imeongezeka ukienda hospital ni yaleyale ya kununua dawa.Bora sera ya bima ya afya akaiongelea kila mahala ataeleweka Ila sio Hilo la wafanyakazi,hawana dhiki Kama kundi kubwa la wanajamii.
 
Tundu Lisu karudia mambo ya mishahara ya watumishi tena akiwa Bunda huku wananchi wakimshangaa,hii itazidi kuonesha kwamba yeye anaguswa na mambo ya watumishi tu na sio machinga au wakulima nk nk,natoa tafadhari msije sema hamkuambiwa.
 
Hongereni kwa kampeni.

Twende kwenye hoja moja kwa moja,binafsi Sina tatizo na watumishi kuongezwa mishahara hiyo ni haki yao lakini ni vyema hoja Kama hii ikachagua majukwaa ya kuizungumzia.

Wafanyakazi hususani wa serikali wa kada zozote ni moja ya kundi ambalo jamii kubwa inaliona kuwa na maisha mazuri au ya nafuu maana ukiacha huo mshahara Hawa Wana fursa za mikopo kwa dhamana ya kazi zao na vimapato vya hapa na pale,ambapo kwa upande wa Pili wa shilingi Kuna kundi kuubwa Sana la vijana hawana kazi,wakulima,wavuvi,machinga na makundi mengine ya jamii wasio na kipato maalumu.Ni rai yangu kwa kua kundi hili la pili ni kubwa Sana na ndio kundi muamzi wa uchaguzi ni vyema sera zako zingejielekeza zaidi kwa Hawa kuliko watumishi.

Sio sawa kuzungumzia mishahara kwa kamii ambayo inaona mtu kuajiriwa ni kulamba bingo regardless of how much one is paid.Jikite kwenye sera za kulainisha ugumu wa maisha na kurahisisha biashara za watu wa kawaida,binafsi hata kwa observation yangu watu wa kawaida Wana Hali mbaya za maisha kuliko kuzungumzia wafanyakazi ,watu wataona Bora huyu huyu aliopo,narudia kusema Chadema msaidieni mgombea wenu kunadi sera kwa lugha rahisi Kama wafanyavyo wagombea wengine wa Upinzani maana kwa sasa anapata muitikio mkubwa zaidi kadiri siku zinavyosogea, Ila sio Kama wanasisiemu huwa wanasoma risala.Nawatakia kampeni yenye mafanikio
Anachofanya TL ni kutetea haki za watu wote. Maumivu yakikuzidi kunywa simu
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Ushauri wako ni mbovu kupita kiasi

Katika vitu ambavyo Lissu anapaswa avizungumze kila wakati ni hilo la mishahara ya wafanyakazi. Maana hilo ni fact ambayo wananchi wanaielewa vizuri kuwa ni mfano halisi wa serikali isiyojali watu bali vitu.

Labda mimi ambacho ningemshauri ni kuwa siku hizi za karibuni naona kama amekuwa akitumia muda mwingi kutoa ufafanuzi wa mwenendo wa kampeni na madhaifu ya Magufuli kitu ambacho ni kizuri lakini ameanza kujisahau kutozungumza masuala ya wananchi kwa msisitizo sana kulinganisha na wiki kadhaa zilizopita alipokuwa anatumia muda mwingi zaidi kuongelea masuala ya yanayogusa ugali wa wananchi.

Nimkumbushe tu aanza kubalance tena kati ya kuzungumzia udhaifu wa serikali ya Magufuli na Masuala yanayogusa wananchi hasa ya kiuchumi.

So far kwa maoni yangu kuna issue lazima azizungumze kila wakati

1. Katiba mpya
2. Sekta binafsi
3. Micro economy hapa ndo kuna wananchi wengi (machinga, mama Ntilie etc)

4. Ajira kwa vijana
5. Sijui kwa nini Lissu hazungumzii suala la Maji, hapa ndo kuna kura za wanawake hapa
6. Bima ya Afya kwa wote
7. Elimu bora siyo bora elimu (Lissu anapaswa kuicritic elimu bure ya Magufuli kwa nguvu kubwa kama alivyofanya kwenye vitambulisho vya wamachinga kwa sababu, Elimu bure ni kiini macho tu, watu huko wanachangishwa michango kibao, kuna sehemu nyingine hadi mzazi anaambiwa aende na dawati la mwanae akichaguliwa kuanza sekondari, sasa hiyo elimu bure gani?)

Hivyo vitu ni lazima Lissu avizungumze Kila mahali, Asitake for granted kuwa ameshaeleweka na kwa hiyo eti kazi yake iwe akifika mahali ni kupunga mikono tu na kuongea na wananchi dakika tatu na kisha kwenda kituo kingine, hapana, umma uko very senstive na masuala yanayowahusu hasa ya ugali mezani, watu wa huko kwenye viunga vya miji wanataka kusikia atawafanyia nini.

So far Best Speech ya Lissu ni ile aliyoitoa Arusha, kwenye Ile speech aliongea masuala mengi muhimu na kwa delivery nzuri sana.

Sasa Sambamba na kumpiga Spana Jiwe kwa mapungufu ya serikali yake Lissu arudi tena kwenye kuzungumzia masuala kama alivyokuwa kipindi cha phasebya Kanda kwa kanda
 
Wafanyakazi wakiongezewa mishahara watatoa huduma bora sababu watakuwa na amani ya moyo na utulivu wa akili.

Ukitibiwa na mtumishi mwenye msongo wa mawazo ndio unakuta daktari anakuandikia panadol halafu nesi au mfamasia wanakupa phenergan au unaumia mguu unafanyiwa operation ya kichwa.

Kwa upande wa elimu utakuta watoto wetu shule za kayumba(elimu bure) madaftari hakuna mwalimu anaye sahihisha wala hawapewi homework.
 
Anahutubia mishahara minono kwa wavuvi,wakulima na wafugaji-hawamwelewi
Tundu Lisu karudia mambo ya mishahara ya watumishi tena akiwa Bunda huku wananchi wakimshangaa,hii itazidi kuonesha kwamba yeye anaguswa na mambo ya watumishi tu na sio machinga au wakulima nk nk,natoa tafadhari msije sema hamkuambiwa.
 
Anahutubia mishahara minono kwa wavuvi,wakulima na wafugaji-hawamwelewi
Wewe umenielewa Ila wenye akili finyu wameshindwa kunielewa na bahati mbaya wasikilizaji wengi miongoni mwa hao uliowataja wako kwenye kundi la wenye akili finyu.
Sasa utamsikia mtu akisema eti ukiwaongezea wafanyakazi pesa kwamba zitawafikia na hayo makundi,ni kweli lakini hamjui kwamba tafsiri itakoyokuwepo ni upendeleo kwa wafanyakazi unless hamuwajui wabongo nyie wanavyiwachukulia wafanyakazi wa serikali .
 
Nijuavyo watanzania huwa wanafurahia wanaposikia fulani katumbuliwa kwenye kazi yake. Watanzania wengi wanapenda ile hali Mbaya waliyonayo na wengine wawe nayo pia.
Uzi wako nimeuelewa kuna watu wananuna kusikia wafanyakazi watalamba mishahara minono.
Kweli iongelewe hoja ya mishahara Lakini sio kwa kurudia Sana kila siku na kila Mahala.
Waache wanaobisha mgombea asishauriwe kuongelea mishahara kwa mama ntilie,machinga,wavuvi,wakulima nk atapata majibu yake oktoba,hiyo sera ni ya kuongelea kwenye press tu Kama ya Jana ambayo watazamaji na wasomaji wengi ni tabaka la wasomi Ila sio specific rally eti unazungumzia kuongeza mshahara watu hawana ajira
 
Back
Top Bottom